Wadau wa michezo,
Nimejaribu kufuatilia kidogo harakati za huyu bwana katika medani za soka la bongo, na napenda kutoa pongezi kwake kwa moyo mkubwa alionao katika kutaka kuongoza soka la bongo katika nafasi mbalimbali.
Nakumbuka alikuwa FAT enzi zile na baadae kukatokea "msukosuko" kama sijakosea. Lakini huyu bwana anaonekana si mtu wa kukata tamaa. Kila nafasi inapotokea ni lazima aingie kwenye kinyang'anyiro.
Nakumbuka amefanya jitihada kugombea nafasi katika TFF lakini "akapigwa fitna".
Hakuchoka, mwaka mmoja au miwili iliyopita alitaka kugombea nafasi za juu katika chama cha soka cha mkoa wa Mara; nako akapigwa fitna kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu.
"Alivyo na roho ya paka", comrade hajakata tamaa. Mwaka huu tena amerusha kete kutaka nafasi katika TFF. Kama kawaida kapigwa zengwe kaondolewa.
Sasa najiuliza:
1. Ni nani/akina nani wanaompiga zengwe Wambura hadi kuondolewa katika kila kinyang'anyiro cha uchaguzi wa chama cha soka chochote nchini?
2. Je alifanya kosa gani hadi wakaamua ku-deal naye kiasi hiki, japo yeye ana moyo sana wa kuongoza soka la bongo?
3. Nini hatma ya hizi fitna wanazompiga na nini faida wanayoipata wafitini wake?
Binafsi napenda kumpongeza ndugu Wambura kwa jitihada zake licha ya kuwa anapigwa zengwe kwa kila hatua anayotaka kupiga. Namuomba asikate tamaa (anaonekana si mtu wa kukata tamaa) na ipo siku ndoto zake zitatimia tu.
Wakati huo huo nimesikitishwa na kitendo cha kuenguliwa ndugu Jamal Malinzi kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa TFF kwa sababu ambazo nazo zinaonekana kama ni fitna tu.
Kuna kila dalili kuwa tayari ameshaandaliwa mtu katika nafasi hiyo kwani kitendo cha kumwacha mgombea mmoja ni dhahiri shahiri kuwa mtu huyo ameandaliwa.
Sababu zilizotolewa hazitosha kumwengua ndugu Malinzi.
Tunalipeleka wapi soka letu kwa uongozi huu wa kuwekana?