Michael Jordan vs. Len Bias

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,231
113,591
Kwa wapenzi wa kweli wa mpira wa kikapu hususan NBA basi jina la Len Bias litakuwa si geni masikioni mwao. Huyu bwana nina imani kabisa kama asingeendekeza uteja ambao baadae ulikuja kumgharimu maisha yake basi angeweza kumpa changamoto kubwa sana Michael Jordan na pengine sasa hivi mjadala ungekuwa ni nani kati ya Len Bias na Michael Jordan aliyekuwa bora zaidi ktk mpira wa kikapu.

Bias alikuwa na moves za ajabu bana. Alikuwa na uwezo wa kuruka kama Jordan. Alikuwa mrefu kwa kumzidi inchi mbili Jordan. Ukiangalia highlight reel zake utaelewa kwa nini Len Bias alikuwa na potential ya kumpa changamoto kali Jordan.

http://www.youtube.com/watch?v=SvyHXqJIxTw
 
NN labda ambacho kingemweka huyu jamaa na Michael Jordan apart ni determination kubwa aliyokuwa nayo Michael Jordan, kwanza ya kuongeza kiwango chake cha uchezaji alipokuwa mcheza na pia ushindani mkubwa aliokuwa nao hata Da Bulls ilipocheza na timu ambazo hazikuwa nzuri kiasi hicho.

Na kingine ndiyo hicho cha decision making zenye umuhimu mkubwa kimaisha. Maeneo aliyokulea Michael Jordan nayo yalikuwa na vishawishi vingi vya ajabu ambavyo vingeweza kabisa kumuingiza huyu jamaa katika njia ambayo hakuikusudia lakini aliweza kuviepuka na hatimaye dunia ikapata bahati ya kuona kipaji chake kikubwa alichojaliwa na Mungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom