Miasha na watu wa Utaifa mwingine

Miasha na watu wa Utaifa mwingine

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,590
Reaction score
28,761
Wana MMU salam sana,

Nimekuwa najiuliza kwa muda mrefu kwa nini nashindwa ku-cope sana na watu wa mataifa mengine wanaoishi humu nchini kutokana na saikolojia yao na maisha yao, Ukiachilia mbali wazungu na watu wa Asia ambao unaweza kusema
kidogo tuna tofauti nao sana za kitamaduni lakini hawa waafika wenzetu wa mataifa jirani huwa nashindwa kuwaelewa kabisa.

Kwanza ni watu wa kujikweza sana, na hata kama kitu au uwezo hawana huwa wanajifaragua kwa hali yoyote ile
waonekane na wao wamo, unakuta mtu elimu mfano ni ndogo lakini atajitahidi kama kuna mjadala aonekane na yeye yumo tu hata kwa facts za uongo na ukweli ili mradi ama-intain status.

Pia ni watu wako very materialistic, yaani kama kuna kitu anataka a-gain kutoka kwako basi yuko radhi hata kutembea uchi au kama ni kitu mtu anacho atajitahidi hata kuwainamisha wengine na kuwapanda mgongoni ili akipate, kwake haoni hatari kabisa tofauti na wabongo wengi amabo utu kwao na aibu aibu zinawafanya wawe wastaarabu kidogo, hata kuku-snitch ana ku-snitch kwa wizi wizi.

Pia wana tabia ya ubinafsi sana, yaani wao ndio wao,na wakiwa wenyewe kwa wenyewe kuna "big fish" na "small fish" kati yao. Wanabaguana mno wao kwa wao na wana matabaka mno. Wengi wanashikamana si kwa sababu wanapendana ila kwa sababu wana common interest ambazo kama watasimama mmoja mmoja hawawezi kuzipata kabisa.

Kuna tabia ya Wakenya kidogo na Wazambia ya kuwa na papara katika kila jambo wanalolifanya na kuonekana wanajali sana muda hata kwenye ishu zisizo hitaji uharaka, utakuta hata kula yao tafikiri wanafukuzwa, au wamemambiwa kuna zawadi atapewa mshindi wa kula haraka, yaani ukila naye karibu hadi unahisi kinyaa.

Nimeishi na wakenya hapa Bongo, duh bwana usiombe bwana, waganda nao umimi sana, Wakongomani wazee wa mitoko nao kwa kujitutumua usiombe, Wanyarwanda usithubutu kabisa bora hata hao wengine, pia watu wa Zambia na Malawi ubabe uababe ndio staili zao.Nimejaribu kuwauliza watu wengine wanawaonaje hawa jamaa na life staili zao wao nao wanadai hawawaelewi elewi.


Huwa nashindwa kuelewa hawa jamaa, hizi ndizo culture za kwao au basi tamaduni zetu za kitanznia za udugu zinatufanya tushindwe kushi na watu wasio na udugu(cultural conflict)??

Ninyi wana MMU kuna mtu alishawahi kuishi na hawa jamaa akawa o-bserve life staili zao??

Kuna nini kiko tofauti na sisi??

Vipi wakiwa huko kwao wanaishigi hivi hivi au ndio kujichukua chukua wakiwa huku kwetu wakati kwao hawawezi ishi hivyo??
 
Hmm!
Ukiwaona wasomali wanakula kifamilia ni burudani tosha!
Tunawaona wengine katika hizi sheree zetu!
Uzuri wao ni kwamba wanajitahidi kubadilika wakitoka nje ya nchi yao.
 
Hmm!
Ukiwaona wasomali wanakula kifamilia ni burudani tosha!
Tunawaona wengine katika hizi sheree zetu!
Uzuri wao ni kwamba wanajitahidi kubadilika wakitoka nje ya nchi yao.

hawa ni wabinafsi sana
 
i'm sure hao wageni wan a good attributes. kama huoni any 'good side' kwa wengine then tatizo linaweza kuwa kwako. baki kuwa 'local person'
 
Back
Top Bottom