TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,947
- 10,809
SERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa una miamba dhoofu iliyonyonya maji ndio chanzo cha maporomoko yaliyoleta maafa katika eneo hilo la Hanang mkoani Manyara.
Maporomoko hayo ya matope yamesababisha vifo vya watu 65 na majeruhi zaidi ya 100 huku mamia ya wanachi wilayani Hanang wakipoteza mifugo, mashamba na makazi yao kwa ujumla.
"Sehemu iliyonyonya maji ilizua mgandamizo na sehemu ya Mlima ikashindwa kuhimili mgandamizo na hivyo kusababisha kumeguka kwa sehemu hiyo na kutengeneza tope ambalo ndio lilianza kuporomoka kufuata mkondo wa mto Jorodom uliozoa mawe na miti na kushambulia makazi ya binadamu yaliyokuwa pembezoni mwa mto huo," - Msemaji wa Serikali, Mobhare Matinyi