Wana JF habari za muda huu,
Kuna siku nilikaa na mzee mmoja akawa ananielekeza kuhusiana na miaka ya watu kuzaliwa ukilinganisha na maendeleo walio nayo, viwango vya elimu walizofikia na uwezo wa kifikra ukiwa unaongea nao akaweka katika makundi manne.
1. Waliozaliwa 1960s na kushuka chini mzee anadai watu wa kipindi hicho watafutaji na wenye maendeleo na walikuwa wakifika mbali sana kielimu wakiwezeshwa ingawa anasema kulikuwa na watu walevi sana na kusahau familia.
2. Waliozaliwa 1970s kundi hili mzee anazungumzia kama kundi la watu wanaojituma sana lakini hawana uwezo mkubwa sana kiakili na wengi wao wameishia kuunga unga sana elimu zao na wanamaendeleo ya kawaida hasa waliozaliwa 1977,1978,1979.
3. Waliozaliwa 1980s, mzee kalisifia sana kundi la vijana hawa anadai wengine wao wamefika mbali kielimu na ukizungumza nao wana fikra pana na wana maendeleo.
4. Waliozaliwa 1990s na mpaka sasa, mzee katika kundi hili anadai mzee ni nadra sana kupata kijana anaejielewa na wana uwezo mdogo sana wa kufikiri na wanakua haraka sana.
Je kuna ukweli wowote wana JF? Kuna sababu yoyote ya hizi tofauti?