Miaka ya neema, miaka ya uharibifu

Miaka ya neema, miaka ya uharibifu

Nimeamua kuandika hii mada kama nilivyoahidi baada ya kusoma hapa JF kuwa Lulu binti aliyepitia mitihani mingi katika maisha yake ya usichana anakaribia kuolewa! Nikasema inawezekana miaka ya uharibifu imekwisha!
Kuna neno linasema.... Natazama kutakuwako miaka saba ya neema na miaka saba ya uharibifu....! Hili neno lingali hai hata leo hii... Lakini lititafsiriwa kidunia zaidi kuwa kuna kupata na kukosa, maisha ni kupanda na kushuka nknk

Ni wachache mno... Nasema mno ambao maisha yao hawakupitia miaka ya uharibifu... Yani maisha yananyooka toka kuzaliwa mpaka kufa... Inaitwa good karma! Na hata wakipitia uharibifu ni mdogo ama wa kawaida usio na madhara makubwa
Rafiki uharibifu upo na neema ipo, ila kinachohubiriwa zaidi ni uharibifu kwakuwa ndio jambo baya! Kwa sehemu kubwa katika maisha lazima upitie miaka ya uharibifu....
. Inaweza kukutokea mwanzoni mwa maisha yako(maisha ya utotoni) ukanyanyaswa nakuteswa ama kuteseka hasa!
.Inaweza kukutokea katika maisha yako ya ujanani( maisha ya ndoto nyingi, kujituma na tamaa ya mafanikio) miaka ya uharibifu huonekana sana kipindi hiki....
.Inaweza kukutokea kwenye stage ya utu uzima mpaka uzeeni.. Hii ni mbaya sana. Na hapa ndio wengine kwa kutojua huwacheka watu na kusema eti walichezea maisha yao ujanani... MSIWALAUMU SIO WAO... kuna vitu hutokea bila uamuzi binafsi wa mtu...
Kuna wimbo mmoja wa Zanto ule wa kisiwa cha malavidavi.. Usikilize vizuri ule wimbo una ujumbe ulioshiba

Tumepitia, tunapitia na tutapitia hii miaka ya uharibifu... Ni muhimu KUONJA hii joto ya jiwe.. Uteleze lakini usianguke.. Na ni afadhali ikutokee sasa bado ukiwa na nguvu na muda wa kustahilimi... Wengi hatuna huu ufahamu kuwa katika maisha kuna kipindi lazima uyumbe... Keep on focusing, usitetereke na kuanza kuingizwa chaka kuwa eti umerogwa ama nyota yako imeibiwa nk... USIJARIBU asilani kwenda kwa wataalam wetu wale wa ramli chonganishi... Wamevuruga maisha ya watu wengi, mahusiano hata familia pia. Wamegombanisha ndugu na kuwaachia makovu ya visasi visivyoisha... Yaani wanaongeza tatizo juu ya tatizo... Miaka yako ya uharibifu ikiisha una kimeo kingine cha wataalam waliokuingiza kwenye laana na maagano yasiyokoma

Ndugu yangu mpendwa wangu... Magumu unayopitia ni ya muda tu... Unatengenezwa ili uwe imara zaidi mbeleni... Niamini KUTAPAMBAZUKA. TUU... hata usiku uwe mrefu kiasi gani KUTAPAMBAZUKA!
Basi inuka sasa neno hili likutie nguvu, neno hili likupe faraja.. Haijalishi unapitia magumu gani ya
Kipato
Ugonjwa
Kazi
Biashara
Mahusiano nk.... Simama imara kukichwa kutakucha..... Usikate tamaa wala usikatishwe tamaa na mtu.. Maisha hayana kuchelewa bali yana wakati wa kupata... Muda wako wa kupata ukifika utapata tuu..
Watu wengi sana (spot light) ikiwa ni wasanii wetu pamoja na sababu nyingine zozote wameangukia pua kipindi hiki cha miaka ya uharibifu... Uzoefu na kutoshauriwa vema! Vimewamaliza kabisa.... Wameteleza na kuanguka kabisa.....!!!

La mwisho na la muhimu sana... Miaka ya uharibifu haitokei kwa mtu mmoja mmoja tu bali hata katika familia, ukoo mpaka Taifa...

Barikiwa na neno hili.. Miaka ya uharibifu inapopita kifuatacho ni kicheko tupu... Tumia tiba ya chumvi tu katika kipindi uonacho unapitia magumu na mikwamo kwa muktadha wa mada! MIAKA YA UHARIBIFU!

Jr
Hivi Bro mshana, hii chumvi ukiogea chooni ni sahihi kweli,!?
Maana wengine vyoo vimeungana na bafu, au ndio inabidi niogee nje
 
Mnyama yeyote anayeishi ndani ya nyumba yako aliyetumwa kutoka shimo la kuzimu kukufuatilia... Kuchelewesha baraka zako, kuchelewesha nafasi zako za kazi, kuchelewesha utukufu wa watoto wako, kukufanya ulie kila siku na kuzuia baraka zako" hao wanyama Wasiishi kamwe kuuona mwezi wa Juni. Bwana Mungu wako atakupigania, Kwa maana wakati wako wa kusherehekea umefika Yatosha Yatosha,Hakuna maumivu Tena katika familia yako Katika Jina la Yesu kristo

Amen
FB_IMG_1656672929910.jpg
 
Hivi hii issue ya chumvi ukioga baharini kabisa kwenye chumvi lukuki IPO applicable?
Yeah Lakini haishauriwi sana utumie ile kwakuwa sometimes maji kupwa au maji kujaa huja ama huenda na vingi
 
Yoe 2:25 SUV​

Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
 
Yoe 2:25-27 SUV
Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
 
Back
Top Bottom