Nimepokea habari ya kukamatwa kwa M/kiti wa CDM Bwana Freeman Mbowe kwa majonzi makubwa sana lakini, huku nikiendelea kutafakari nikasikia Pia Bwana Zitto Kabwe pia yupo rumande ya Polisi Singida na baadaye kuachiwa, ni vyema kila mmoja wetu hasa wana mapinduzi kutafakali hili swala kwa Pamoja na matukio ya kukamatwa kwa Bwana Tundu Lissu, Lema na wenzao wanne huko Tarime pamoja na watanzania wanaokamatwa kila siku katika kila kona za Tanzania bila kosa na kuonewa na polisi na hata kubambikiziwa kesi za uongo kwa ajili ya kuwakomo, kuwanyanyasa na kuwadhalilisha.
Ninachotaka kusema hapa leo siyo ujinga wa Jeshi la Polisi na jinsi wasivyojuwa hata kazi zao kwasababu ya ama kuendelea kupata mafunzo yenye mbinu walizorithi kwa mkoloni mzungu au kuwa Jeshi kubwa lenye wajinga wengi kwa maana kwa takribani miaka 50 sasa Jeshi hilo liliachwa kuwa la Form Four Failure na Darasa la Saba lakini hata hivyo Form Four wanaojiunga na hilo Jeshi wengi wao wamekuwa ni watu wanaotumia vyeti vya ndugu na jamaa zao huku wao kihalisia ni ama Form Two Failure au aliyeacha shule kwa kuogopa umande wakitokea katika katika mitaa iliyojaa kila aina ya lanaa za kubaka dada na mama zao.
Lengo langu kuu ni kuwe swali mezani! ili wana JF tupeane kumbukumbu sahihi na pia tujue umuhimu wa hawa viongozi wetu kukamatwa, kunyanyaswa na hata kudhalilishwa maana tukisha kujua hilo basi tutapiga moyo konge na tutajua umuhimu wa kuchagua viongozi ambao wapo tayari kunyanyashwa, kuonewa na kudhalilishwa kwa ajili yetu! Tutashagilia na tutakuwa makini katika kila chaguzi kuhakikisha kuwa hao ndio tunao wapa kura zetu zote maana wapo mbele yetu nasi tupo nyuma yao.
Swali langu kwa wana-JF ni kuwa "Nani anajua nchni yoyote katikia Bara la Afrika ambayo ilipata uhuru wa kweli kutoka kwa vyama na watawala waliorithi Ukoloni kutoka kwa Wazungu bila kunyanyashwa, kuonewa, kukamatwa na hata kufungwa jela kwa wapigania uhuru wa Afrika?" Kama hamna basi tujivunie kukamatwa kwa viongozi wetu kwa ajili yetu, tuwape moyo na tuombe Mungu atuongezee viongozi wengi zaidi kama hao.
Kwa wale wasiojua nini maana ya uhuru, ili mjadala husiwape tabu bure, nawapa kiashiria kuwa walichofanya wazungu katika karne ya kumi na tisa ni kukabidhi serikali za nchni za Afrika kwa waafrika na siyo kutoa uhuru kwa wananchni, hatua ya kutoa uhuru kwa wananchni ilipaswa kuanzishwa na wale viongozi waliopokea madaraka kutoka kwa Wazungu, kwa maana hiyo mimi naamini kuwa hata kama ingewezekana kuwapa wananchi uhuru bila wazungu kuondoka ingekuwa best scenario kwangu kuliko hili lililofanyika la kuwandoa wazungu wakati wananchni bado wanaendelea kukosa uhuru na kunyanyaswa pengine hata zaidi ya wakati wa serikali za Wazungu.
Tukijufunza na case za Kenya, Uganda, Malawi, Zimbabwe, Afrika kusini nk. Ni dhahiri kuwa mlango wa uhuru na haki umeanza kufunguka Tanzania, maana bila kukamatwa kwa hao viongozi wetu hatuta fika kunapotaka kwenda. Mfano: Kenya vuguvugu za kuwatoa wakoloni weusi zilianza siku nyingi sana lakini zilipamba moto mwanzoni mwa 1980 huko nyuma na hadi sasa mengi yamendikwa katika historia ya kenya kuanzia kuuwawa kwa Tom Mbuya, Dr. Ouko, kuwekwa kizuizini kwa Laila Odinga hadi vurugu za mauwaji ya 2007/2008 ambayo kwasasa kuna kesi za ICC, ikumbukwe kuwa miongoni mwa waliopo mbele ya ICC yumo Msomali mwenzie Saidi Mwema (ambaye naye kama Said Mwema ndiye alikuwa IGP wa kenya).
Katika hii case ya kenya tunajifunza kuwa wakati kama huu tuwe makini sana maana uhuru upo karibu kufika saa yoyote na dakika yoyote lakini sasa tusiruhu mamluki na vibaraka wa hawa wakoloni kuingia miongoni mwetu! Maana watakapo soma alama za nyakati na kujua kuwa jua halita zama bila ukombozi na uhuru kamili lazima watapandikiza miongoni mwetu watu wao ili baada ya ukombozi wapate ulinzi wa kudumu, hicho ndicho Moi alichomfanyia Raila baada ya kujua fika kuwa hata kwa wizi hawata weza kuiba kura za wakenya alimchomeka Kibaki kibaraka wake miongoni mwa wapigania uhuru ili kujiweka salama mbele ya hasira ya Umma, kutokufahamu kwa wakenya na wanamapinduzi wao kuwa wana mamluki miongoni mwao kumewapa hasara kubwa sana hata kuwafanya hadi sasa kuwa katika nusu uhuru nusu ukoloni.
Kesi ya Uganda imekuwa tofauti kidogo maana wao ilibidi kutumia mtutu ya bunduki kuwaondoa wakoloni weusi. Hii njia ni nzuri lakini pia ina madhara yake ambayo yaweza kuwa sawa kabisa na hii ya kutumia sanduku la kura. Nasema yaweza uwa sawa kabisa pale ambapo yamkini wapigania uhuru watakuwa wanauwawa na kufungwa kila kukicha ni bora kutumia vita ijulikane maana katika vita hata wao watakufa pia.
Madhara waliyopata Uganda kutokana kulazimika kuingia vitani dhidi ya wakoloni weusi ni kuwa nchi haiku stabilize mapema sana ukilinganisha na kesi ya Rwanda ambayo Kagame ameonyesha uimara mapema mno, yawezeka kesi ya Kenya tokea kuanzia kuuwawa kwa Tom Mboya hadi leo ni sawa kabisa na bora kama wangefanya vita na kuwatowa wakoloni hawa kwa vita kuliko njia ya sanduku la kura ilivyo wagarimu.
Kwa kweli mifano ni mingi sana, lakini naomba niliache swali lisimame kama swali, Ni nchni gani Barani Afrika ambayo ilipata uhuru kutoka kwa vyama na watawala waliorithi Ukoloni kutoka kwa Wazungu bila kunyanyashwa, kuonewa, kukamatwa na hata kufungwa jela kwa wapigania uhuru wao? Kama hamna basi tujivune kukamatwa kwa wapigania uhuru wetu.
Tuwe pamoja nao, kila mmoja kwa imani ya Dini yake afunge pamoja nao tuwaombee maana uhuru tunaoutaka hautapatika bila hayo kutokea, hayo yote hana budi kutokea ndipo tutashinda hii vita dhidi ya serikali za kidhalimu.