Miaka miwili ya Rais Samia na mageuzi sekta ya elimu Arusha

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,032
Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2022/23 chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu madarakani Mkoa wa Arusha umepokea zaidi ya shilingi bilioni 24.4 kutoka vyanzo mbalimbai: kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya elimu.

Mkoa umepokea fedha za UVIKO 19 kiasi cha shilingi bilioni 10.42 kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa 417 wya sekondari na vyumba vya madarasa 96 kwa shule shikizi.

Katika fedha hizo pia walipokea kiasi cha Tsh milioni 200 kukamilisha vyumba 13 vya madarasa ya sekondari katika kata

Pia mkoa umepokea fedha za SEQUIP kiasi cha sh. bilioni 4.7 kwa ujenzi wa shule mpya kumi za sekondari za kata kuwaondolea adha wanafunzi kutembea umbali mrefu na kupunguza masongamano katika vyumba vya madarasa

Jumla ya vyumba vya madarasa 810 vyenye thamani ya shilingi bilioni 16.2 vimejengwa na kuufanya mkoa kuwa na jumla ya vyumba vya madarasa 3,093 ya sekondari huku idadi ya shule za sekondari za serikali ikiongezeka kutoka 152 mwaka 2020/21 hadi kufikia shule 172 mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la shule mpya 24 huku shule za msingi zikiongezeka kutoka 820 mwaka 2020/21 hadi kufikia 857 mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la Shule 37.

Idadi ya mabweni katika shule ze Sekondari imeongezeka kutoka mabweni 205 mwaka 2020/21 na kufikia mabweni 230 mwaka 2022/23, sawa na ongezekc la mabweni 25.
 
Back
Top Bottom