Miaka hii mitatu itangazwe ni kipindi cha mpito

Miaka hii mitatu itangazwe ni kipindi cha mpito

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
6,581
Reaction score
15,251
Kiuhalisia, wakati wa awamu ya 5 mifumo mingi ya utawala au ilivurugwa au iliuawa kabisa.

Moja ya taasisi zilizouawa ni Bunge. Wabunge walipatikana kwa kupitia uchaguzi bandia. Wabunge hawa bandia, wengi wao hawana uwezo na wala hawana baraka za wananchi.

Uvurugaji ulianzia kwenye kura za maoni ndani ya CCM ambapo robo tatu ya wagombea waliopitishwa na wajumbe, majina yao yalikatwa, na kisha kupachikwa majina kutoka mifukoni mwa mwenyekiti. Mfano mzuri ni pale Shinyanga ambapo bwana Masele aliyepata kura zaidi ya 300 za wajumbe, jina laki lilikatwa, akapachikwa Katambi aliyepata kura 3. Na hiyo ilifanyika kwa nchi nzima.

Hatua ya pili ya uvurugaji uchaguzi ilifanyika kwenye uteuzi wa wagombea, ambapo kupitia kwa bwana Mahera na tume yake bandia ya uchaguzi alikata majina mengi ya wagombea kupitia vyama vya upinzani.

Hatua ya tatu ilifanyika kwa kupitia wakurugenzi wa halmashauri ambao bila ya kujali kura zilizopigwa, waliweka idadi yoyote ya kura waliyoitaka na kisha kuwatangaza wagombea kupitia CCM.

Bunge linalitokana na wabunge wa namna hii, halina msaada wowote kwa yeyote isipokuwa aliyeliteua, na ambaye kwa sasa hayupo. Hii ndiyo sababu ya msingi kwa nini bunge hili bandia halijawahi kuihoji serikali kitu chochote, kwa sababu bunge lenye ni zao la uovu.

Ili kuokoa fedha za umma, na kwa vile Rais, kwa kiwango kikubwa (ukiacha uonevu dhidi ya Mbiwe) ameonekana kujali haki za wananchi kuliko taasisi zote zilizoharibiwa wakati wa awamu ya 5, hasa bunge na Polisi, ni aheri bunge hili bandia likafutwa, kukawepo kipindi cha mpito cha miaka mitatu. Katika kipindi cha mpito, maamuzi yote yafanywe na Serikali. Maana kiuhalisia, hili bunge bandia, hatuoni kazi yake yoyote yenye manufaa kwa umma zaidi ya kututia hasara.
 
Ili kuokoa fedha za umma, na kwa vile Rais, kwa kiwango kikubwa (ukiacha uonevu dhidi ya Mbowe) ameonekana kujali haki za wananchi kuliko taasisi zote zilizoharibiwa wakati wa awamu ya 5, hasa bunge na Polisi, ni aheri bunge hili bandia likafutwa, kukawepo kipindi cha mpito cha miaka mitatu. Katika kipindi cha mpito, maamuzi yote yafanywe na Serikali. Maana kiuhalisia, hili bunge bandia, hatuoni kazi yake yoyote yenye manufaa kwa umma zaidi ya kututia hasara.
Una hoja ya msingi Ila haitekelezeki.

Watawala wanafurahia ombwe la Bunge imara, maana Wana Uhuru wa kufanya chochote bila ukosoaji.

Kwa mazingira hayo, hakuna wa kulivunja hilo Bunge batili !
 
Back
Top Bottom