Ndiyo wewe ni mnafiki, na hayo maneno sio ya kwangu bali ni maneno ya Yesu mwenyewe. Kwanini unaniita mimi mzinifu? Ina maana dhambi ya uzinzi ndiyo unaiona ni kubwa kuliko dhambi uzifanyazo wewe?
Pia naendelea kukupa vifungu as follows:-
"Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa anawafundisha. Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. Wakamwambia Mwalimu, mwanamke huyu amefumabiwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao walipozidi kumhoji, alijiinua akawaambia YEYE ASIYE NA DHAMBI MIONGONI MWENU NA AWE WA KWANZA KUMTUPIA JIWE. Akainama tena akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao waliposikia wakashtakiwa kwa dhamiri zai, wakatoka mmoja mmoja wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake na yule mwanamke amesimama katikati" Yohana 8:2-9.
Haya wewe usiye na dhambi.