mapesa yamejaa
JF-Expert Member
- Dec 29, 2021
- 1,412
- 3,403
Kipindi stendi kuu ya mabasi Mbezi inafunguliwa na mzalendo namba moja wa karne ya 21 Mh dk John Pombe Joseph Magufuli alitoa maelekezo ya kwamba barabara kutokea stendi hiyo kwenda mpigi magoe ianze kujengwa kwa kiwango cha lami pamoja na maji yapelekwe huko jimbo la kibamba lote
Na kweli kesho yake tu pilikapilika zikaanza.
Magari yakawa yanapishana tayari kwa ujenzi. Dawasa nao hawakuwa nyuma. Mabomba yakaanza kutandazwa sehemu mbali mbali za jimbo la kibamba kuelekea maeneo ya mbezi misumi,msakuzi na mpigi magoe ambako watu hawajawahi kuona maji toka Nchi ipate uhuru mwaka 1961.
Bahati mbaya haikuchukua mda mrefu mzalendo katutoka.zile shughuli zilizokuwa zinaendelea zikaanza mwendo wa kobe na hatimaye zikafa kabisa hadi leo watu wa kibamba maeneo ya Mpigi Magoe, Msakuzi na kwingineko huduma hizi wanazisikia tu. Inawalazimu kununua maji kwenye visima vya watu binafsi kwa unit shilingi 5000-6000 kwa usawa huu kweli?
Hivi ninyi viongozi mliopewa dhamana mnataka tuwasimamie kwa mijeredi ndo mpeleke hizo huduma? Kama pesa hazitoshi muuze hizo V8 zenu mnunue Vitz. Haiwezekani huduma hizo muhimu zikosekane ndani ya jiji la kibiashara Dar es Salaam. Wananchi tunataka maji, hatutaki V8.
Sent using Jamii Forums mobile app