Miaka 50 ya uhuru wa wadanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya uhuru wa wadanganyika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Averos, Jun 28, 2011.

 1. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Tunapokaribia miaka 50 ya Uhuru wa Taifa letu CHANGA, hebu tuangalia sekta za huduma za jamii kwa kufanya assessment ndogo tu,

  Elimu: Hivi kuna shule japo moja ya serikalli ambayo Wizara ya Elimu inaweza kutolea mfano kuwa ni shule bora kwa maana ya kuwa na miundo mbinu bora na walimu wa kutosha na inatoa huduma bora kwa wanafunzi wake?

  Afya: Hivi kuna japo hospitali moja ya serikali hapa Tanzania ambayo IMEKAMILIKA kwa kuwa na miundombimu yote stahiki na wafanyakazi wa viwango na yenye vifaa vyote muhimu vya kitiba?

  Nishati: Hivi kuna wilaya yoyote hapa Tanzania ambayo haina tatizo la umeme kwa aslimia 100

  Maji: Hivi kuna Wilaya japo moja hapo Tanzania ambayo maji yanapatikana kwa asilimia 100, nazungumzia maji safi na salama

  Usafiri: Je wadau kua japo wilaya moja hapa Tanzania ambayo haina adha ya usafiri, yaani ina barabara murua, magari safi, hakuna msongamano wa magari, n.k?

  Mawasiliano: Hivi wajameni kuna japo Wilaya moja ambayo hawana tatizo la mawasiliano kwa 100, simu, fax, net, n,k kwao si tatizo?

  Makazi: Hivi hapa kwetu Tanzania tuna japo wilaya moja ambapo raia wetu wanaishi katika nyumba zao, zilizo imara na madhubuti?

  Lishe: Hivi hapa kwetu Tanzania kuna Wilaya japo moja ya mfano ambapo watu wake wanajitosheleza kwa aina zote za vyakula na hawa na tatizo la lishe?

  Kama zipo hizo samples naomba mnisaidie.
   
Loading...