Miaka 50 ya Uhuru kwa ajili ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya Uhuru kwa ajili ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Dec 9, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Haya maazimisho ya miaka 50 ya uhuru wa wadangayika hasa yanatoa tafsiri gani? Imekuwa kana kwamba Serikali ya CCM ndio inayojivunia miaka hiyo 50. Cha maana hasa ambacho kimeonekana ni Serikali kutuonyesha nguvu za kijeshi tulizonazo, maazimisho haya yanalalamikiwa na watanzaniawalio wengi.. (binafsi nipo mkoani) wananchi wanauliza hivi ni nini hasa tunachoweza kujivunia na kuwaonyeshwa wenzetu? ni zile siraha ana nguvu za kijeshi, ??......kwa nini hatujaweza kuonyesha kwa vitendo masuala ya kiuchumi?.... kwa nini yafanyike Dar Es Salaam tu? Kwa nini isingekuwa hadi mikoani, wananchi wakasherehekea kwenye viwanja vikubwa vya kila mkoa hapa nchini?

  Kwa nini baadhi tu ya watanzania waonekane wakivishwa nishani na wakila na kujichana pale IKULU wakatri wengine wapo hoi wayumbani hawana mlo, hawana fedha za kulipia mahospitalini, hawana ada wa wototo wao , hawajui kesho wataamkaje, na wengine hata mshahara hawajui watapokea lini??

  Wale wa kule Zanzibari wanahoji, Je ni kiasi gani cha Fedha zilizotumika na zimetoka wapi kama si katika kasma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo nao wapo (Kama ni uhuru wa Tanzania Bara, basi nao nahaki ya kupewa kasma ya kusheherekea kwa Kishindo siku ya maazimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi za Zanzibar) !...Wanauliza ninyi wadanganyika ambao mliiua nchi yenu Tanzanganyika kwa muungano wa 1964, inakuaje mnasherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Taifa la Tanzania ambayo bado haijatimiza miaka 50??
   
Loading...