Miaka 50 ya tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya tanganyika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by doctorwasummary, Dec 7, 2011.

 1. d

  doctorwasummary Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mataifa yaliyoendelea ni matokeo, pamoja na mambo mengine, ya kusema ukweli na kusahihishana ikiwa ni pamoja na kuwajibishana. Sisi kazi yetu ni uongo na kuogopana. Hivi kweli tunasherekea miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania bara? Je tulipopata uhuru mwaka 1961 tulikuwa tukiitwa Tanzania bara? Je muungano wetu ni wa Tanzania Bara na Zanzibar? Kwa nini tunalazimisha mambo kwa kusema Tanzania bara na visiwani? Je wazanzibar wanajitabulisha kwa utanzania visiwani? Kama suala ni kuzingirwa na maji kwa nini Wakerewe na wengineo washio visiwani nao wasiitwe Tanzania visiwani? Tufikie wakati tuseme ukweli hata kama itaonekana kwamba tulikosea hapo awali. Hii ni miaka hamsini ya TANGANYIKA na kama baadhi yetu hatutaki, tusubiri miaka hamsini ya Tanzania ifikapo mwaka 2014, hapo itakuwa ni sahihi kuliko kudai na kuhararisha majina ambayo hayakuwepo na ambayo hayajatimiza miaka hamsini!
   
Loading...