Miaka 50 ya tanganyika: Maamuzi tata ya watawala!!!

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,667
362
Tunaelekea miaka 50 toka uhuru wa Taifa letu pendwa Tanganyika.

Kwa faida ya kumbukumbu kwa sisi wa vizazi vya hapa karibuni na vile vijavyo, nakaribisha wakongwe na vijana kuchangia maada tajwa hapo juu....

Ni lipi unalokumbuka kama tukio tata kuwahi kufanywa na viongozi wa nchi yetu ambalo kwa namna moja au nyingine limechangia kupunguza hatua za maendeleo ya taifa letu na ambalo hakika unaona kama ni kioja kufanywa na kiongozi wa ngazi ya juu kwa taifa.

Nawasilisha kwa mjadala
 
Kwa mfano, najaribu kuvuta kumbukumbu miaka fulani hapa katikati kama sikosei awamu ya tatu ya Mzee Benja (mtanisahihisha) kuliwahi kutambulishwa ka-utaratibu ka kufidia sikukuu za kiserikali (public holidays) zinazotokea mwisho wa wiki kuhamishiwa kwenye wiki linalofuata.

Jambo kama hili kwa taifa LINALOTAFUTA kuendelea ni aibu kubwa sana na ambalo hata kwa vizazi vijavyo watakaposikia kuna wakati viongozi wa taifa hili katika uchanga wake waliwaza kufidia sikukuu za weekend kuwa weekdays watacheka sana.......TUNAOTAFUTA KUENDELEA tunatafuta kupumzika zaidi wakati wenzetu walioendelea wanatafuta masaa zaidi ya kufanya kazi

Viroja vya wakubwa
 
Back
Top Bottom