Miaka 4 ya Rais Magufuli, Wananchi Wawazodoa BBC

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
Na Mwandiwshi Wetu, DarBlog

Ni Miaka Minne imetimia tangu Jemedari Rais John Pombe Magufuli aingie madarakani.

Ni kishindo cha aina yake cha Serikali hii ya Awamu ya Tano ambayo iliabidi maboresho mbalimbali katika utoaji wa elimu bure, uboreshaji wa miundombinu,ufunguaji wa mahakama ya mafisadi,ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, meli katika maziwa makuu, uboreshaji wa sekta ya anga, kumtua mama ndoo kichwani, kuimarisha sekta ya umma n.k.

Haya yote yametekelezwa kwa aina yake kabisa ingawa kumekuwa na sintofahamu kutoka kwa chombo cha habari cha BBC ambacho moja ya habari yake iliyodai "Minne ya Magufuli yawa Gumzo, Watu Watofautiana Maoni" ni kama imewatokea puani!

Habari hiyo ambayo ilinukuu zaidi wabunge wa upinzani nchini na baadhi ya wachambuzi kutoka Kenya, imekumbana na upinzani mkali kutoka kwa wananchi mbalombali si tu wa Tanzania bali hata wa nchi jirani kutokana na baadhi ya wachambuzi kuonekana kuongozwa si na uhalisia wa mageuzi makubwa anayoyafanya Rais Magufuli bali hisia binafsi na mitazamo ya kisiasa.

Mmoja wa wasomaji Pendaeli Ulanga anasema kuhusu habari hiyo ya BBC: "Mimi binafsi BBC huwa naona mmetumwa na wazungu, Waingereza. Nyie hamuwezi kuisemea mazuri Tanzania, ingekuwa Kenya mngesema maana wao ni ma puppet wa wazungu."

Naye Baraka Transport anasema: "Lol jamani sisi twafurahi uhuru tuliokuwa nao na viongozi wetu. Nyie mnachunguza Tz na kuona kama kuna mabovu huko mlipo ni mbinguni mpaka mnawashwa kuongelea mambo ya Tz. Demokrasia ni uchaguzi wetu na mapenzi yetu hata muongelee vipi Tz twajiamini na chaguzi letu sote ni Magufuli mtindo mmoja."

Naye JF ramess Jcombo Box anasema: "For me its YES Magufuli even though there are economic challenges but Magufuli is the best".

Aidha nae As Ras anasema "BBC Swahili ni Tv ya udaku.Siku zote mnavutiwa na mambo HASI".

Kwa upande wake Geofrey Kajengile aliandika:
"Huyo ndio Baba wa Taifa letu namkubali sana aliabidi kutusaidia na amesaidia makubwa.. mwacheni mzee wetu afanye kazi sina mengi mungu katupa zawadi watanzania"

Naye Miltone Stephano amesema "Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni,hongera sana Rais Magufuli hakika tumeziona juhudi zako katika miaka minne ya uongozi wako."

Ndugu J.F.K amesema "Hao Amnesty International na wengine wanajidanganya Tumewazoea."

Emmyd Zoo anasema "Hao watu wa haki za binadamu waende Iraki, Sudani, Burundi, South Afrika ambapo watu wanauana sisi Tanzania hatujadili habari wala wanahabari sio mahitaji yetu, shida yetu ni maendeleo ambayo hatujayaona miaka yote".

Dr GFRANKESTEIN anasema: "Sasa hivi kodi hatusumbuki tena kama zamani halafu yanajitokeza majuha na kusema kuna ukandamizaji wa haki yaani mimi ukijitokeza mbele yangu unampinga rais napita na sikio."

Maoni haya na mengine zaidi ya 300 .yanaonesha kuwza vyombo vya habari vina safari ndefu sana ya kuhakikisha vinaakisi maoni na matarajio ya watu badala ya kila siku kunukuu wanasiasa ambao kila jambo hulitazama kisiasa na kimaslahi binafsi.

"Uchambuzi wa kisiasa wa BBC kumhusu Magufuli ni funzo kubwa kwa tasnia ya habari kuwa kwa sasa wananchi wanajionea wenyewe mambo yanayowagusa na vyombo vya habati visipobadilika vitajikuta vinazidi kukosa uhahalali," anasema mtaalamu wa mawasiliano kwa umma John Japhet ,Mashaka.
 
Bora na hao jamaa nao wapewe za uso, wamezidi.

Huyo aliyewauliza kwani huko ni Mbinguni , kawauliza swali zuri sana.
 
Ninaamini Akitoa nafasi za ajira kada zote, akiongeza mishahara kwa waliopo kazini....
Hatokuwa na mpinzani tena....
Uhuru Wa habari tunao,

otherwise tusingekuwa nyuma ya keyboard, democracy tunayo, otherwise tusingejiandikisha kupiga kura...

Magufuli is the best katika kujenga miundombinu na kulinda rasilimali zetu, I appreciate you.
 
Ninaamini Akitoa nafasi za ajira kada zote, akiongeza mishahara kwa waliopo kazini....
Hatokuwa na mpinzani tena....
Uhuru Wa habari tunao,

otherwise tusingekuwa nyuma ya keyboard, demcha ocracy tunayo, otherwise tusingejiandikisha kupiga kura...

Magufuli is the best katika kujenga miundombinu na kulinda rasilimali zetu, I appreciate you.
Bwana mdogo mbwa kumlamba miguu bwana wake aliyemfuga si jambo la ajabu ila mwenye mbwa akimlamba miguu mbwa hiyo ni habari kubwa,,simama kwenye nafasi yako vizuri...ni wakati wenu huu ila mbegu ya udhalimu ina tabia ya kumea hadi kwenye kizazi cha nne cha aliyeipanda, ipo siku nawe utakuwa victim hapo utaingia google utafute matamshi yako haya na utamani siku uliyoyawaza kabla ya kuyanena ipunguzwe kwenye siku zako
 
Mkisema hayo pia muongelee gharama za matibabu, dawa na upatikanaji wake. Maana haya yanamgusa mwananchi yoyote yule kuliko SGR au flyover za Dar es Salaam na Tanga.
Kingine kinachowagusa wananchi lkn hakiongelewi ni ajira kwa wahitimu wa vyuo. Hili halionekani kwamba litakuja kua bomu
 
Na Mwandiwshi Wetu, DarBlog

Ni Miaka Minne imetimia tangu Jemedari Rais John Pombe Magufuli aingie madarakani.

Ni kishindo cha aina yake cha Serikali hii ya Awamu ya Tano ambayo iliabidi maboresho mbalimbali katika utoaji wa elimu bure, uboreshaji wa miundombinu,ufunguaji wa mahakama ya mafisadi,ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, meli katika maziwa makuu, uboreshaji wa sekta ya anga, kumtua mama ndoo kichwani, kuimarisha sekta ya umma n.k.

Haya yote yametekelezwa kwa aina yake kabisa ingawa kumekuwa na sintofahamu kutoka kwa chombo cha habari cha BBC ambacho moja ya habari yake iliyodai "Minne ya Magufuli yawa Gumzo, Watu Watofautiana Maoni" ni kama imewatokea puani!

Habari hiyo ambayo ilinukuu zaidi wabunge wa upinzani nchini na baadhi ya wachambuzi kutoka Kenya, imekumbana na upinzani mkali kutoka kwa wananchi mbalombali si tu wa Tanzania bali hata wa nchi jirani kutokana na baadhi ya wachambuzi kuonekana kuongozwa si na uhalisia wa mageuzi makubwa anayoyafanya Rais Magufuli bali hisia binafsi na mitazamo ya kisiasa.

Mmoja wa wasomaji Pendaeli Ulanga anasema kuhusu habari hiyo ya BBC: "Mimi binafsi BBC huwa naona mmetumwa na wazungu, Waingereza. Nyie hamuwezi kuisemea mazuri Tanzania, ingekuwa Kenya mngesema maana wao ni ma puppet wa wazungu."

Naye Baraka Transport anasema: "Lol jamani sisi twafurahi uhuru tuliokuwa nao na viongozi wetu. Nyie mnachunguza Tz na kuona kama kuna mabovu huko mlipo ni mbinguni mpaka mnawashwa kuongelea mambo ya Tz. Demokrasia ni uchaguzi wetu na mapenzi yetu hata muongelee vipi Tz twajiamini na chaguzi letu sote ni Magufuli mtindo mmoja."

Naye JF ramess Jcombo Box anasema: "For me its YES Magufuli even though there are economic challenges but Magufuli is the best".

Aidha nae As Ras anasema "BBC Swahili ni Tv ya udaku.Siku zote mnavutiwa na mambo HASI".

Kwa upande wake Geofrey Kajengile aliandika:
"Huyo ndio Baba wa Taifa letu namkubali sana aliabidi kutusaidia na amesaidia makubwa.. mwacheni mzee wetu afanye kazi sina mengi mungu katupa zawadi watanzania"

Naye Miltone Stephano amesema "Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni,hongera sana Rais Magufuli hakika tumeziona juhudi zako katika miaka minne ya uongozi wako."

Ndugu J.F.K amesema "Hao Amnesty International na wengine wanajidanganya Tumewazoea."

Emmyd Zoo anasema "Hao watu wa haki za binadamu waende Iraki, Sudani, Burundi, South Afrika ambapo watu wanauana sisi Tanzania hatujadili habari wala wanahabari sio mahitaji yetu, shida yetu ni maendeleo ambayo hatujayaona miaka yote".

Dr GFRANKESTEIN anasema: "Sasa hivi kodi hatusumbuki tena kama zamani halafu yanajitokeza majuha na kusema kuna ukandamizaji wa haki yaani mimi ukijitokeza mbele yangu unampinga rais napita na sikio."

Maoni haya na mengine zaidi ya 300 .yanaonesha kuwza vyombo vya habari vina safari ndefu sana ya kuhakikisha vinaakisi maoni na matarajio ya watu badala ya kila siku kunukuu wanasiasa ambao kila jambo hulitazama kisiasa na kimaslahi binafsi.

"Uchambuzi wa kisiasa wa BBC kumhusu Magufuli ni funzo kubwa kwa tasnia ya habari kuwa kwa sasa wananchi wanajionea wenyewe mambo yanayowagusa na vyombo vya habati visipobadilika vitajikuta vinazidi kukosa uhahalali," anasema mtaalamu wa mawasiliano kwa umma John Japhet ,Mashaka.
Mbona hujaweka wapinzani wamesema nini? Una upendeleo kama bbc.
 
Back
Top Bottom