Miaka 30 bado tumefunga mikanda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 30 bado tumefunga mikanda!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by vukani, Mar 4, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35

  Juzi katika pekua pekua yangu katika maktaba yetui, nikakutana na Gazeti moja la Zamaani sana, ukilinganisha na umri wangu, linaitwa Mzalendo.
  Ni gazeti la mwaka 1979.
  Kweli baba yangu alikuwa ni mtunzaji, maana gazeti lenyewe ukiliona bado lina hali nzuri tu na linavutia kulisoma.
  Basi katika mojawapo ya habari iliyonivutia ni ile ya Aliyekuwa Rais wa kwanza wan chi hii Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aka Mzeee wa Mwitongo.
  Ukweli ni kwamba nampenda sana huyu mzee. Huwa sikosi kusikiliza zile hotuba zake za alfajiri kupitia TBC1.

  Hotuba hiyo ilikuwa ni ya kututaka sisi Watanzania tufunge mikanda kwa muda wa miezi 18, ili serikali iweze kurekebisha uchumi baada ya vile vita va Kagera.
  Wakati wa Vita hivyo mimi nilikuwa sijazaliwa, na hata wakati hotuba hiyo ya kulihutubia taifa ikitolewa nilikuwa sijazaliwa pia, lakini kinachonifurahisha ni kwamba, kama kuna kitu ambacho kitakuja kutuhukumu basi ni maandishi, maana kauli inaweza kupingwa lakini maandishi, ni vigumu sana.

  Haya Kiranja wa wakati huo Mwalimu nyerere kwa unyenyekevu kabisa akawaambia watanzania, "Jamaniee tunawaomba mfunge mikanda maana vita hii imetufilisi, na baada ya miezi 18, mutaifungua hiyo mikanda"
  Ni kauli ambayo mzee yule aliitoa kwa unyeyekevu kabisa na kutokana na Imani waliokuwa nayo Watanzania kwake yeye watu, wakjifunga mikanda.

  Lakini la kushngaza mpaka leo takribani miaka 30 tangu vita ile iishe bado asilimia kubwa ya Watanzania tumefunga mikanda huku wengine wakiwa wameilegeza na kuongeza Papi ili iwe kubwa zaidi.
  Hali inazidi kuwa ngumu, kila kukicha, asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi katika ulitima wakishindia mlo mmoja kwa siku, na pengo kati ya mwenye nacho na asiye nacho linazidi kukua.

  Juzi nimeenda kununua Dola kwenye duka la kubadilishia fedha pale Posta, nimekuta Dola inazidi kupaa, hadi jana dola moja imefikia kuuzwa kwa shilingi 1330! Sijui wachumi wetu hapa watatueleza nini?
  Ukisikiliza Hotuba za kisiasa na takwimu zao zisizo na mshiko utacheka, utawasikia "Uchumi wetu unapanda kwa asilimia 0.0000001" sasa hii inamnufaisha nani?
  Wakati tunapolilia kupunguziwa bei tunapofanya manunuzi, wengine wananunua bila hata kuuliza bei.

  Mwalimu Nyerere alikuwa na vision, ingawa kuna wakati alifanya makosa, na hilo aliwahi kulikiri, pale aliposema, haiwezekani akae miaka 23 Ikuli halafu asifanye makosa, ni lazima atakuwa alifanya makosa kama binadamu kwani hakuw malaika. Lakini aliwalaumu viongozi wetu wa leo kuwa badala ya kuchukuwa yale mazuri aliyoyaacha wao wanachukuwa mabaya na kuyatupa mazuri, akili gani hii!

  Wakati tunapata Uhuru Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, ili tuendelee, yaani tuondokane na umasikini , tunahitaji mambo makuu matatu,
  1.Watu
  3.Ardhi
  4.Siasa safi na uongozi bora.


  Kwa upande wa watu, wapo wa kutosha kabisa na tena ikiwezekana tuongezeke zaidi, kwa mujibu wa takwimu ya hivi karibuni tuko milioni 38,
  Ardhi nayo iko ya kutosha, naambiwa kuwa karibu asilimia 60 ya ardhi ya nchi hii haijatumika inavyopaswa,
  Kwenye siasa safi na uongozi bora, hapa ndio nina shaka napo, Mwalimu nyerere aliona kwamba ili tuwe na siasa safi ni lazima viongozi wawe waadilifu na hakutaka hilo liwe ni jambo la kupita, na ndio sababu mwaka 1967 wakakutana kule Arusha na kututangazia Azimio la Arusha.

  Mwalimu alikuwa akililinda na kulitekeleza Azimio la Arusha kwa vitendo na ndio sababu alikufa akiwa ni mtu wa kawaida sana, akiwa amejikita kule Butiama Mwitongo akijilimia.
  Alipong'atuka katika uongozi wa nchi hii, kama alivyowahi kusema mwenyewe, viongozi wetu wakakutana kule Visiwani Zanzibar na kulivunja Azimio la Arusha, bila hata kuwatangazia Watanzania na waliporudi, kimya kimya wakaanza kujilimbikizia ukwasi kwa kufuru.

  Kutokana na kuvunjwa kwa Azimio la arusha ndio maana sasa tunashuhuidia kashfa kama za EPA, Kiwira, Richmond, Dowans, Maliasili, TRA, na nyingine nyingi tu.

  Mimi ni msomaji wa Biblia kidogo, katika Wagalatia kuna mahali Mtume Paul aliwambia wagalatia, nitanukuu "Enyi wagalatia, hivi ni nani aliyewaloga ninyi?, nami labda niulize, hivi sisi Watanzania ni nani aliyetuloga?
  Nadhani Mchawi aliyetuloga alishakufa zamaaani….
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...