miaka 3.5 haongei

Ndeonasiae

Senior Member
Aug 15, 2011
102
49
Msaada wapendwa,

Mwanangu wa miaka 3.5 haongei, alianza kutaja maneno kama dada na mama akiwa na umri wa miaka 2 lakini hajaimprove mara kadhaa nimemuona akiniita mama lakini ananiita kwa wiki then mwezi mzima haongei tena. hili ni tatizo gani? kusikia anasikia aunachomwambia anafanya ila kuongea haongei. naombeni msaada tafadhali. nimempeleka hosp, wanasema hana tatizo eti ataongea tu, kinachonishtua ni hiyo kuanza kuonge then ananyamaza kabisa
 
Tatizo lako liliwahi kumkumba son wangu, aliwahi kuota meno akiwa na miezi mitatu!! Akaanza kutembea akiwa na miezi nane lakini mpaka miaka mitatu na miezi mitano haongei hata kidogo zaidi ya kuita mama hata hivyo kilichokuwa kinanifurahisha ni utaalamu wake wa kuongea kwa ishara na utundu wa kimya kimya!!!

Nilimpeleka hospitali wakamchunguza masikio na koo wakasema hana tatizo nimtafutie watoto wenzie wa kucheza nae, akiwa na miaka mitatu na miezi saba nilimpeleka chekechea ambako ndiko alijifunza kuongea kwa bidii ili aweze kujichanganya vizuri na wenzie. Mpaka sasa ni mwaka mmoja tangu aanze kusoma anaongea vizuri kila kitu
 
Mkuu jaribu uwe unamchemshia Supu ya ulimi wa mbuzi awe anakunywa kila siku kwa muda kama siku 3. Au pia waweza

kutumia Dawa hii Umsugue kwenye ulimi wake, kila siku changanya Asali na chumvi umsuguwe kwenye ulimi wake kila siku asubuhi kabla ya kupiga mswaki au

tafuta Dawa hii inaitwa Udi karaha usage huo mzizi kishaa msuguwe kwenye ulimi wake kila siku asubuhi kwa muda wa siku 7

kisha njoo hapa utupe Feedback.@Ndeonasiae Pia waweza kumpeleka shule awe pamoja na watoto wenzie anaweza kuongea.
 
MziziMkavu Daktari wangu uko kila kona. Ushauri utamsaidia ila pia kwa maika 3.5 haendi shule? Shule inasaidia sana wale slow speech taker kids. Cha msingi kama anasikia na daktari anasema hana tatizo la maskio mengineyo basi fanya kama ulivyoshauriwa na mpeleke shule mtoto.
 
Huna haja ya ku paniki wala kuogopa, ni hali ya kawaida sana hiyo. Ataongea tu. Cha msingi uwezo wa kuongea anao ila hataki tu.

Kuna baadhi ya watoto huwa na aina fulani ya 'ukiburi' hivi hasa hasa wakiwa watoto wa mwisho, hii inaisha tu. Kama ulimpeleka hospitali wakaona hamna tatizo, acha Mungu afanye kazi yake tu na atakuwa sawa soon.

Kama ni wa mwisho mtafutie mdogo wake!
 
Waambie wamwangalie chini ya ulimi huwa kuna kinyama kinaunganisha ulimi na sehemu ya chini ya kinywa kikiwepo hicho kinasababisha mdomo kuwa mzito kuongea kuna mtoto alikuwa nako wa miaka 3 kakakatwa hospital ndo anajaribu kuongea mrudishe hospital watu wengi hawakijui hata mie sikuwa nafahamu
 
Mkuu jaribu uwe unamchemshia Supu ya ulimi wa mbuzi awe anakunywa kila siku kwa muda kama siku 3. Au pia waweza

kutumia Dawa hii Umsugue kwenye ulimi wake, kila siku changanya Asali na chumvi umsuguwe kwenye ulimi wake kila siku asubuhi kabla ya kupiga mswaki au

tafuta Dawa hii inaitwa Udi karaha usage huo mzizi kishaa msuguwe kwenye ulimi wake kila siku asubuhi kwa muda wa siku 7

kisha njoo hapa utupe Feedback.@Ndeonasiae Pia waweza kumpeleka shule awe pamoja na watoto wenzie anaweza kuongea.
MziziMkavu unanipaga raha sana nisomapo koment zako
 
Tatizo lako liliwahi kumkumba son wangu, aliwahi kuota meno akiwa na miezi mitatu!! Akaanza kutembea akiwa na miezi nane lakini mpaka miaka mitatu na miezi mitano haongei hata kidogo zaidi ya kuita mama hata hivyo kilichokuwa kinanifurahisha ni utaalamu wake wa kuongea kwa ishara na utundu wa kimya kimya!!!

Nilimpeleka hospitali wakamchunguza masikio na koo wakasema hana tatizo nimtafutie watoto wenzie wa kucheza nae, akiwa na miaka mitatu na miezi saba nilimpeleka chekechea ambako ndiko alijifunza kuongea kwa bidii ili aweze kujichanganya vizuri na wenzie. Mpaka sasa ni mwaka mmoja tangu aanze kusoma anaongea vizuri kila kitu

Tabia zake zilikuwaje? huyu ana afya nzuri kabisa na ukuaji wake haukuwa na shida hata kidogo, ana dada yake wa miaka 6.5 ambaye alikuwa na shida kwenye ukuaji ila anafanya vizuri sana shuleni, anaongea sana japo ni mwembamba sana, huyu wa miaka 3.5 hapendi kucheza na watoto wenzie na ikibidi kucheza anapenda kucheza na watoto wakubwa au watu wazima. wenzake wakichezea toys yeye ataenda kuchezea vitu kama gari, computer, tv radio etc na uchezeaji wake ni kama wa kuharibu huwa anapenda sana kuchunguza kila kitu ndani yake kuna nini kwa hiyo anavunja na kuharibu vitu. yuko shule tayari tanga April last year na malalamiko toka kwa walimu wake ni kuwa anakuwa kama anatafiti kila kitu yani hachezei vitu vya kawaida kama wenzie.
 
Huna haja ya ku paniki wala kuogopa, ni hali ya kawaida sana hiyo. Ataongea tu. Cha msingi uwezo wa kuongea anao ila hataki tu.

Kuna baadhi ya watoto huwa na aina fulani ya 'ukiburi' hivi hasa hasa wakiwa watoto wa mwisho, hii inaisha tu. Kama ulimpeleka hospitali wakaona hamna tatizo, acha Mungu afanye kazi yake tu na atakuwa sawa soon.

Kama ni wa mwisho mtafutie mdogo wake!

Naomba mungu aongee tu, ila la kuongeza mdogo wake:confused2:
 
Waambie wamwangalie chini ya ulimi huwa kuna kinyama kinaunganisha ulimi na sehemu ya chini ya kinywa kikiwepo hicho kinasababisha mdomo kuwa mzito kuongea kuna mtoto alikuwa nako wa miaka 3 kakakatwa hospital ndo anajaribu kuongea mrudishe hospital watu wengi hawakijui hata mie sikuwa nafahamu
Hicho wameshamwangalia wataalamu, walimpima koo, masikio, wakacheki na ulimi hana tatizo kabisa.
 
Tabia zake ni kwamba alikuwa na utundu wa uharibifu kama mtoto wako, lakini unajua ni kwa nini??? Ni kwa sababu hajui kuongea, hawezi kuuliza akajibiwa so anaishia kutaka kujifunza mwenyewe ndo pale anapoharibu!!!

Pia mtoto wangu pamoja na umri mdogo alionao lakini ni mkali sana kwenye computer, anajua kucheza games mbali mbali kutumia programmes mbalimbali, kuwasha na hata kuzima pindi akichoka. Hiyo yote ilitokana na ukweli kwamba kutokuongea kulimfanya awe karibu na computer coz haiongei bali anai-operate tu na yenyewe inatii.

Kitu cha kunote ni kwamba; Mtoto kama huyo usimpeleke kwanza zile shule za gharama (English Medium) kwa sababu kule michezo ya watoto inakuwa inafuatiliwa sana na walimu kiasi kwamba wanakuwa limited na michezo yao hivyo kutokujichanganya vizuri, pia watoto wanakuwa wachache sana na analazimika ajue kuongea Kiingereza. Mie nilishauriwa nimpeleke uswazi, nikaangalia tu shule yenye uzio na usalama wa watoto wenyewe baasi!!!

Hii inamaana kwamba wakiachiwa break, michezo inayokuwepo pale na ule wingi wa watoto......!! mwanao hata awe mzito vipi kuongea ni lazima ataongea tu!!!

Tabia zake zilikuwaje? huyu ana afya nzuri kabisa na ukuaji wake haukuwa na shida hata kidogo, ana dada yake wa miaka 6.5 ambaye alikuwa na shida kwenye ukuaji ila anafanya vizuri sana shuleni, anaongea sana japo ni mwembamba sana, huyu wa miaka 3.5 hapendi kucheza na watoto wenzie na ikibidi kucheza anapenda kucheza na watoto wakubwa au watu wazima. wenzake wakichezea toys yeye ataenda kuchezea vitu kama gari, computer, tv radio etc na uchezeaji wake ni kama wa kuharibu huwa anapenda sana kuchunguza kila kitu ndani yake kuna nini kwa hiyo anavunja na kuharibu vitu. yuko shule tayari tanga April last year na malalamiko toka kwa walimu wake ni kuwa anakuwa kama anatafiti kila kitu yani hachezei vitu vya kawaida kama wenzie.
 
Tatizo lako liliwahi kumkumba son wangu, aliwahi kuota meno akiwa na miezi mitatu!! Akaanza kutembea akiwa na miezi nane lakini mpaka miaka mitatu na miezi mitano haongei hata kidogo zaidi ya kuita mama hata hivyo kilichokuwa kinanifurahisha ni utaalamu wake wa kuongea kwa ishara na utundu wa kimya kimya!!!

Nilimpeleka hospitali wakamchunguza masikio na koo wakasema hana tatizo nimtafutie watoto wenzie wa kucheza nae, akiwa na miaka mitatu na miezi saba nilimpeleka chekechea ambako ndiko alijifunza kuongea kwa bidii ili aweze kujichanganya vizuri na wenzie. Mpaka sasa ni mwaka mmoja tangu aanze kusoma anaongea vizuri kila kitu

Dah mkuu umenishusha pumzi kumbe hili tatizo ni kwa wengi eeh niliposoma uzi huu nikasema mtoa mada amenisemea, na mimi wa kwangu anaelekea 3.3 sasa lakini hawezi kuongea ila anaweza kwa ishara na pia ni mtundu sana. hopeful na yeye ataanza siku moja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom