Miaka 21 jela kwa kuvunja na kuiba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imewahukumu Hamisi Jilala Kwabi(22) na Mohamedi Kassim (22) wote wakazi wa mtaa wa stoo kata ya Igunga mjini, kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 21 jela baada ya kukiri makosa yao matatu yote ya kuvunja na kuiba kwa miezi tofauti.

Awali mwendesha mashitaka wa polisi wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba aliiambia mahakama mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Igunga, Lydia Ilunda kuwa katika mashitaka ya kwanza washitakiwa wote wawili walitenda kosa hilo Februari 6, 2021 majira ya usiku.

Ilidaiwa washitakiwa walivunja nyumba ya Onanis Jackson mkazi wa Mtaa wa Kamando kwa nia ya kuiba kinyume na kifungu 294(1) (a)(2) kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019.

Alisema baada ya kufanikisha kuingia katika nyumba hiyo ya Onanis Jackson washitakiwa waliiba televisheni moja aina ya Boss yenye thamani ya Sh 1,100,000, laptop moja aina ya HP yenye thamani ya 900,000, feni moja yenye thamani ya Sh 45,000, zote zikiwa na thamani ya Sh 2,045,000 huku akiongeza kuwa walitenda kosa kinyume na kifungu 265 na 258(1) kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019.

Majid alisema mashitaka ya pili ni kuvunja nyumba usiku kwa nia ya kuiba ambapo Februari 11, 2021 muda wa usiku katika Mtaa wa Masanga mjini Igunga washitakiwa wote wawili walivamia na kuingia kwenye nyumba ya Hanifa Thabit.

Majid alibainisha kuwa baada ya kuingia walifanikiwa kuiba televisheni aina ya Boss yenye thamani ya Sh 900,000 ambapo walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 265 na 258 (1) kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Mwendesha mashitaka huyo alisema mashitaka ya tatu kwa washitakiwa hao wawili ni kuvunja nyumba usiku kwa nia ya kuiba.

Majid aliendelea kuiambia mahakama kuwa Machi 27, 2021 majira ya usiku katika Mtaa wa Kamando mjini Igunga washitakiwa baada ya kufanikiwa kuvunja nyumba ya Khalfani Mohamed waliiba televisheni moja aina ya Samsung yenye thamani ya Sh 800,000.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashitaka hayo matatu mbele ya hakimu Lydia washitakiwa hao wawili walikiri mbele ya mahakama kutenda makosa matatu kwa miezi tofauti.

Aidha kabla ya kutolewa hukumu hiyo na hakimu wa wilaya, Mwendesha mashitaka wa polisi wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa kwa kuwa wamekuwa tishio kwa uvunjaji wa nyumba na kuiba katika mji wa Igunga kwa muda mrefu.

Akitoa hukumu kwa washitakiwa Hakimu wa Wilaya, Ilunda alisema kutokana na washitakiwa kukiri makosa yao matatu na upande wa mashitaka kuthibitisha vitendo vilivyofanywa na watuhumiwa hao, mahakama imeona pasipo ubishi washitakiwa wana hatia hivyo kwa makosa hayo matatu kila moja miaka saba hivyo kwa yote miaka 21 ili iwe fundisho kwa wengine.

Chanzo: HabariLeo
 
Duuh! Hatari sana. Mbona hao vijanaa ni wadogo sana na wanafanya ujambazi? Shida ni nini?
 
Hukumu hizi kali ndiyo zinatakiwa. Sijajuaga hawa watu wanawapaga nini police, maana mara nyingi wanakamatwa na kuachiwa. Hii naona labda mkuu wa upelele wa Igunga labda ni mgeni hapo.
 
Kumpata culprit wa matukio yaliyotokea vipindi tofauti tofauti na hawana signature move au known modus oparendi hua inakua risk as in mshukiwa anaweza angushiwa majumba mabovu hata yasiyomhusu.

Mfano kikundicha wizi kiwe kinajiita Moto Group kwamba kila kikiiba kinaacha njiti nne za kibiriti, moja inawaka mpaka imekua jivu na zingine zimewaka kidogo, hii signature inaweza saidia kujua mhusika ni Moto Group.

Now kama hawana signature inakua wanaangalia M.O yaani utekelezaji wa tukio unaendana? Mfano kama kila aliyeibiwa askari walipoenda kuchunguza waligundua starting point hua ni dirishani basi wanaweza hitimisha kwamba wote walioibiwa kwa M.O hii watakua wameibiwa na same culprit.

But these kids? Deducing ya kwamba wamehusika matukio yote matatu ilifanywa kweli au ni ile furaha ya askari kufunga jalada hata kama lina makosa? Nchi yetu ina shortage of manpower katika jeshi so it is understandable kwanini kunakua na makosa ya hapa na pale na wakati mwingine huamua kufunga jalada kwa kumpa kesi asiyehusika.

Mahakama ndiyo ilitakiwa ihoji vitu kama hivi ili hawa askari waende extra miles.
 
Maelezo ya mtoa mada ni kwamba hao culprits 'walikiri'.

Wewe unajua kabisa kosa la mhalifu kukiri kizembe zembe linavyomrahisishiaga hakimu 'kutiririsha mvua'.

Ninajua katika kukiri kwao huenda kukawa kwa kilaghai kwamba wasipoisumbua mahakama watapewa tuzo ya kuachiwa huru!

Lakini ndivyo hivyo wembe umekwisha kuwanyoa.
 
Back
Top Bottom