Miaka 20's tu status za 'relationship-complicated'

livewise1

JF-Expert Member
May 25, 2019
837
952
Nilikuwa napitia kwa ukaribu sana status zilizowekwa katika page za wasichana as per say! Nimekuta wengi wameandika kwenye kipengele cha relationship "Complicated".

Wale ambao umri wao unaonekana umesogea nikawa sishangai ila kuna vibinti kama 12 hivi vya umri chini ya 20's au 20's yenyewe vimeandika hiyo, nikawa nawaomba urafiki kisha nawatafuta inbox tunaongea kidogo nikiwauliza kuhusu hizo relationship, duuh nashushiwa stori za majonzi hizo hatari.

Wengine wametelekezwa na waume za watu, wengine wamekimbiwa kisa walibeba mimba, wengine waliachwa na wapenzi, vikasepa kusikojulikana, tafraani.

Ila wengine wakaishia kuniblock, wengine wakanitukana kisa nawakumbusha majanga yaliyosahaulika. Sasa mtu anakupa stori ya kupigwa matukio kama 4 hivi hapo ana miaka 19 au 20! Akifika 30's kule itakuwaje aisee?

Vimoyo vya hivi visichana ni kichaka asee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom