Miaka 15 Ijayo; Usishangae ............

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
127
Hivi umeshawahi kukaa na kufikiri miaka michache ijayo mambo yatakuwaje? Hebu kwa mfano mwaka 2022 twaweza shuhudia yafuatayo hapa Tanzania.

1. Wakati huo dawa ya ukimwi ishapatikana, mtu unaenda ofisini baada ya kutokuwepo kwa takriban majuma mawili. Bila shida unaongea na bosi wako huku ukimueleza..."Bosi, yaani ka-ukimwi kalinitandika vibaya sana last week" halafu sijui kwa nini mimi kananiandama hivyo.................

2. Bungeni napo tunakuwa na waheshimiwa kama Mr Ebo,Kingwendu, Bambo na wafananao na hao. Unasikia spika akisema....Mheshimiwa Bambo swali la nyongeza. Bambo, "Mheshimiwa spiko pamoja na majibu mazuri ya waziri wa michezo na utamaduni naomba kuulizi swali hivi kwa nini siku ya fiesto isiwe sherehe ya kitaifo ambapo raiso atato mapumziko nchi nzimooo???

3. Uswahilini nako kama Manzese kutakuwa na maghorofa ya kutisha...Majungu ya akina mama wa apartment zilizo jirani yatakuwa...Hause girl wangu siku hizi hapiki bila kutizama DSTV ili kuona wenzake wa Afrika Kusini wanavyotengeneza masalo. Wewe wako bado anatizama kipindi ya mapishi ya ITV na Clouds TV???? Tv ya Clouds wakati huo kama CNN

4. Nako maofisini itakuwa utata mtupu, haitokuwa jambo la ajabu kuongea na bosi wa kiume huku hereni zinamning'inia masikioni. Na si ajabu akipata taarifa ya ghafla kuwa kampuni yake imepata hasara suruali ikamdondoka manake uvaaji ni ule wa bila mkanda huku ikiwa imeegeshwa chini ya ******(kata-K)"au nusu mlingoti"

5. Ukipita Sinza ndo utatoa macho...watoto wa chekechea wamajipanga kwenye ATM mashines kuchukua pesa ya kununulia lambalamba shuleni kwao. Yaani itakuwa mtafaruku mtupu...Mara mtoto mmoja anamwambia mtoto mwenzie, baba kanidipositia cheki feki, imebaunsi hivyo leo ice cream nitachukua kwa overdraft.
 
Duh bro, ulikuwa unafikiria nini wakati unaandika hiyo kitu?...ila umesahau vituko vya kwenye "Nursing home" pale Nurse anapochikichia morphine or dilaudid ya mgonjwa kwenda jidunga mwenyewe...wauza samaki wa kukaanga uswahilini wanachukua visa,master card na nyinginezo. Daladala una-swipe card combo ya mwezi mzima...........
 
Miaka 15 ijayo kazi ya kupiga picha haitakuwa na ajira tena. Itabidi nitafute jembe and kununua kipande cha shamba.
 
Unajua unatakiwa kujiuliza inakuwaje issue kubwa ama hii alafu kichwa cha State kimetulia kunani wazee wa Forum tujuzane kulikoni?????????
 
Aisee, nakubaliana na wewe. Maana hivi sasa maisha ya Tanzaniayanakikimbia sana kwa maendeleo ingawa ni ya kuiga toka nje.

Kzi kweli kweli
 
Wakati huo ma dada pooa wa mabanda ya wahaya watatangaza biashara kwa kurusha matangazo tbc
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom