Miaka 10 ya Kashfa ya Richmond bila ya Lowassa kufikishwa mahakamani!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,305
33,924
Siku tano zilizopita yaani tarehe 7/2/2018 ilitimia miaka kumi kamili tangu Edward Lowassa ajiuzulu uwaziri Mkuu tarehe 7/2/2008 kutokana na kuhusishwa na Kashfa ya utoaji Tenda kwa kampuni ya kufua umeme ya richmond.

Lakini mpaka leo mbali ya kutuhumiwa tu na mahasimu wake wa kisiasa Lowassa hakuwahi kufikishwa mahakamani iwe ya kawaida ama ile ya "mafisadi" iliyoanzishwa kwa minajili ya kazi hiyo. Ifutayo ni hotuba yake aliyoitoa siku ya kujiuzulu kwake:

Nakushukuru mheshimiwa Spika kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili nimpongeze Dr. Harrison Mwakyembe Mwenyekiti wa Kamati teule,kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri sana.Kwa kazi nzuri kwa maoni yao na wameiwasilisha vizuri.Lakini Mheshimiwa Spika, nimesimama kuweka kwenye Kumbukumbu kutokuridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.

Mhesimiwa Dr. Harrison Mwakyembe ni mwanasheria tena daktari alikuwa anafundisha wanafunzi Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni Natural justice. Wewe pia Mheshimiwa Spika ni Mwanasheria, unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba katika Kamati Teule, imesikiliza watu wengine wote, pamoja na waliowaita minong’ono ya mitaani. Wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja!

Mheshimiwa Spika. Nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya bunge mpaka ofisini kwangu hata wangeniita ningeenda kwa mguu kama hamna gari. Na nilikuwa tayari kufanya hivyo.Hawa ni watu makini sana, siwezi kuamini kwamba wanaweza kufanya Oversight kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga, walisema Waziri Mkuu ilikuwa hivi, kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza, Waziri Mkuu wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano Mheshimiwa Spika, kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema, wenye Richmond ni fulani uka- table Record na ushahidi kwamba ni fulani?

Mheshimiwa Spika Taifa letu ni taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa Demokrasia pa kubwa katika nchi yetu pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendendeka, Mheshimiwa Spika nchi haitakwenda vizuri.

Hapa ndipo tunategemewa kuonyesha umakini, umahiri wetu katika mambo ya Demokrasia. Kwa hiyo nilichofanyiwa Mheshimiwa Spika napenda kuweka kumbukumbu sahihi…sawa. Kwamba naona si sahihi, na nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana na nimeonewa sana katika hili. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja kuelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo, mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani kuniuliza. Kwa nini muamini minong’ono ya mitaani kuliko maelezo yangu?

Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong’ono ya mitaani, niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi… Tume wamepewa muda wa kutosha kabisa, lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Lakini mheshimiwa Spika, hata pale uliponinong’oneza ukaniambia “una ushahidi wowote”? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Ofisi ya Waziri Mkuu, hata mmoja! Lakini kitabu cha Majedwali kimejaa majedwali meengi pamoja na Magazeti mpaka ya Udaku, lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika. Mimi naamini ingekuwa ni heshima wangeliweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii na hii na hii. Mimi nadhani ingejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni, tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki, amefanya hiki bila kumsikiliza, nachelea kuuliza, hivi watu wa chini itakuwaje?

Lakini Mheshimiwa Spika nimetafakari kwa makini sana jambo hili, nikajiuliza, hivi hasa kulikoni. Mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu, wenye heshima zao. Mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo, kulikoni?

Mimi nadhani, they have a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, ionekane Waziri Mkuu amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe. Mheshimiwa Spika. Nimetafakari sana, kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.

Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa, kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini na kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge wa kunisingizia.

Mheshimiwa Spika nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili, namshukuru sana mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Mawaziri, nawashukuru waheshimiwa Wabunge, na wanachama wa CCM tuliosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama chama Mapinduzi. Baada kusema hayo nakushukuru Mheshimwa.

Mkazo ni wa kwangu mimi.
 
Hapo mashishiemu ni makofi tu, pwaa pwaa pwaaaa...! yamesahau tatizo ni uwaziri mkuu! aisee.. umenikumbusha, kumbe hakuhojiwa na kamati ya mwakyembe.!? basi watamwogopa mpaka mbinguni, na wakifika peponi mwenyezimungu atashangaa jamaa wakitimua mbio wakielekea motoni kwa kumuogopa lowassa!
 
Naona hata mahakama ya ufisadi nayo wameianzisha kisiasa.

Eti hadi leo hakuna mtu yeyote aliyeburuzwa kwenye mahakama hizo!

Wao wanadai Lowassa ndiyo fisadi mkubwa

Sasa najiuliza wanamwogopa nini kumburuza kwenye mahakama hiyo??

Tunajua kuwa CCM ndiyo "makazi" ya mafisadi nchini

Ninashangaa hiyo mahakama ya mafisadi "haijawapokea" mafisadi wakubwa wa CCM ambao wamekiri wenyewe na wengine wametajwa na hawajakanusha, ambao ni akina Chenge, Tibaijuka na Ngeleja.....

Lakini nashangaa kuwa bado hadi Leo hiyo listi yote niliyoitaja hapo juu, hakuna hata mmoja wao ambapo serikali.yetu imepata ujasiri wa kuwaburuza maakamani
 
Siku tano zilizopita yaani tarehe 7/2/2018 ilitimia miaka kumi kamili tangu Edward Lowassa ajiuzulu uwaziri Mkuu tarehe 7/2/2008 kutokana na kuhusishwa na Kashfa ya utoaji Tenda kwa kampuni ya kufua umeme ya richmond.

Lakini mpaka leo mbali ya kutuhumiwa tu na mahasimu wake wa kisiasa Lowassa hakuwahi kufikishwa mahakamani iwe ya kawaida ama ile ya "mafisadi" iliyoanzishwa kwa minajili ya kazi hiyo. Ifutayo ni hotuba yake aliyoitoa siku ya kujiuzulu kwake:

Nakushukuru mheshimiwa Spika kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili nimpongeze Dr. Harrison Mwakyembe Mwenyekiti wa Kamati teule,kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri sana.Kwa kazi nzuri kwa maoni yao na wameiwasilisha vizuri.Lakini Mheshimiwa Spika, nimesimama kuweka kwenye Kumbukumbu kutokuridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.

Mhesimiwa Dr. Harrison Mwakyembe ni mwanasheria tena daktari alikuwa anafundisha wanafunzi Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni Natural justice. Wewe pia Mheshimiwa Spika ni Mwanasheria, unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba katika Kamati Teule, imesikiliza watu wengine wote, pamoja na waliowaita minong’ono ya mitaani. Wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja!

Mheshimiwa Spika. Nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya bunge mpaka ofisini kwangu hata wangeniita ningeenda kwa mguu kama hamna gari. Na nilikuwa tayari kufanya hivyo.Hawa ni watu makini sana, siwezi kuamini kwamba wanaweza kufanya Oversight kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga, walisema Waziri Mkuu ilikuwa hivi, kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza, Waziri Mkuu wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano Mheshimiwa Spika, kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema, wenye Richmond ni fulani uka- table Record na ushahidi kwamba ni fulani?

Mheshimiwa Spika Taifa letu ni taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa Demokrasia pa kubwa katika nchi yetu pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendendeka, Mheshimiwa Spika nchi haitakwenda vizuri.

Hapa ndipo tunategemewa kuonyesha umakini, umahiri wetu katika mambo ya Demokrasia. Kwa hiyo nilichofanyiwa Mheshimiwa Spika napenda kuweka kumbukumbu sahihi…sawa. Kwamba naona si sahihi, na nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana na nimeonewa sana katika hili. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja kuelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo, mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani kuniuliza. Kwa nini muamini minong’ono ya mitaani kuliko maelezo yangu?

Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong’ono ya mitaani, niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi… Tume wamepewa muda wa kutosha kabisa, lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Lakini mheshimiwa Spika, hata pale uliponinong’oneza ukaniambia “una ushahidi wowote”? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Ofisi ya Waziri Mkuu, hata mmoja! Lakini kitabu cha Majedwali kimejaa majedwali meengi pamoja na Magazeti mpaka ya Udaku, lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika. Mimi naamini ingekuwa ni heshima wangeliweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii na hii na hii. Mimi nadhani ingejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni, tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki, amefanya hiki bila kumsikiliza, nachelea kuuliza, hivi watu wa chini itakuwaje?

Lakini Mheshimiwa Spika nimetafakari kwa makini sana jambo hili, nikajiuliza, hivi hasa kulikoni. Mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu, wenye heshima zao. Mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo, kulikoni?

Mimi nadhani, they have a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, ionekane Waziri Mkuu amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe. Mheshimiwa Spika. Nimetafakari sana, kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.

Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa, kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini na kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge wa kunisingizia.

Mheshimiwa Spika nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili, namshukuru sana mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Mawaziri, nawashukuru waheshimiwa Wabunge, na wanachama wa CCM tuliosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama chama Mapinduzi. Baada kusema hayo nakushukuru Mheshimwa.

Mkazo ni wa kwangu mimi.
Tupeni ushahidi tumpeleke. Mmeisha nyie. Rudini kwenye nepi maana siku hizi ni pampas au rudieni migomba kuchambia
 
Attachments

  • FB_IMG_1492698982281-1.jpg
    FB_IMG_1492698982281-1.jpg
    6.2 KB · Views: 45
Nasari amepeleka ushahidi TAKUKURU mtuhumiwa mkampandisha cheo takukuru wakapotezea tuhuma
Hata hao wakipeleka ushahidi wa wizi huo wa Lowassa hamtampeleka mahakamani hata kama yuko chadema haimaanishi hana makosa
Mbona
Lema
Msigwa
Sugu
Bulaya
Lissu
Mdee
Mnawapeleka palisi mahakamani
Ugumu wa Lowassa uko wapi?

Chadema walistuka kuwa Lowassa alisingiziwa huo ufisadi
Mulikuwa munawapenyezea taarifa na wasiri wenu ili kummaliza Lowassa
Mungu sio Athumani wala sio faru John

Leo watu wanaojielewa kama Mimi nimegundua ule ulikua uzushi mbona mahakama ya mafisadi haijampeleka Lowassa kolokoloni?

Wapumbavu wanaimba wimbo uleule wa fisadi Lowassa

Hata mtu niliemuamini slaa
Kaiacha chadema kisa fisadi Lowassa
Huko ccm kuna mafisadi wangapi au hao anataka kutuaminisha kuwa wanapambana na ufisadi mbona

Kila siku wanambembeleza fisadi Lowassa arudi ccm?

Wapuuzi tu hawawezi kunielewa
 
Nina ushahidi wa kutosha kuhusiana na wizi na ufisadi wa Lowasa na Rostam ~ John Mnyika
Sasa Mnyika ana uwezo kumpeleka Lowassa Mahakamani? Halafu kwani nyie CCM ufisadi wa Lowassa ni wa kweli ama mnamwita fisadi kwa kuwa tu hao kina Mnyika walisema ni fisadi kutokana na taarifa walizokuwa wanapewa na kina Mwakyembe?

Kinara wa kusema kwamba anao ushahidi wa ufisadi wa Lowassa Dr. Slaa si keshakuwa mwanachama wenu kwa nini msiutumie ushahidi alio nao kumfikisha Lowassa Mahakamani?
 
Back
Top Bottom