Miafrika ndivyo tulivyo?

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Ikiwa imebakia siku moja tu kabla uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015, tumeshuhudia mengi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Na mengi yamejitokeza haswa baada ya uongozi wa rais Jakaya Meisho Kitwete kuchukua madaraka mwaka 2005. Tulishuhudia kashfa za kila aina kubwa na ndogo. Na kubwa zaidi ilochukua nafasi ya juu ni HUJUMA ZA UCHUMI ziloshindikana kiasi kwamba wananchi walio wengi walichoka na maisha huku kundi dogo la wachache wakifaidika.

Tulimlaumu sana JK, rais alokuwa madarakani tulimlaumu kwa mengi japo naye hakusita kufanya mabadiliko mengi tu ya baraza lake la mawaziri pengine kuliko kingozi yeyote alotangulia Afrika nzima. Nchi haiongozwi na mtu mmoja, Utawala wa nchi huwa na na mihimili mitatu na kama moja wa[po itakuwa na mapungufu basi serikali pekee haiwezi kufanikiwa. Inatakiwa vyombo vyote hivi vitatu vifanye kazi kwa Uadilifu na kuwajibika laa sivyo nchi haitatawalika. Na ndicho haswa kilichotokea katika miaka 10 ilopita. 1. Bunge lilikuwa bovu na dhaifu katika majukumu walokabiodhiwa, 2. Mahakama zetu ziliongoza kwa rushwa na 3. Serikali ilokuwa madarakani iliongozwa Kimtandao.

Leo ndio siku ya mwisho ya kujikumbusha yalopita na kesho ni mwanzo mpya, mwanzo ambao kwa mtazamo wangu utaonyesha jinsi gani sisi Waafirka Tulivyo!..Kwa maana kesho ndipo wananchi watachagua uongozi mpya kwa hiari yao wenyewe juu ya mustakabali wa nchi yao na sidhani kama kuna mgombea hata mmoja alojikumbusha na yalotokea nyuma ili kura yake iwakilishe mahitaji yake na sio chama chake au kundi lake.

Inanikumbusha tu Ndugu yangu Mzee Mwanakijiji na wenzake kama miezi miwili ilopita walipofanya ibada ya kufunga kwa siku 40 za maombi ili Mwenyezi Mungu awaongoze katika mstari ulonyooka na hatima yake Mwenyezi Mungu amejibu! Kawapeni mtihani mwingine mkubwa zaidi ambao kwamba ni nyie wanachi mloomba haya naye kawarejeshea. Kawapeni wakuu wa UFISADI kati ya wagombea. CCM kama Taasisi ya kifisadi na LOWASSA fisadi papa aloshindikana na upande wa pili kawapeni pia wagombea waadilifu wasojulikana.

Wananchi wengi hawaitaki CCM kwa sababu ya UFISADI wake na waliapa kutoipa kura zao mwaka 2015 lakini Kwa akili za kinafiki tumechagua kuenzi Ufisadi wa taasisi hiyo na upande mwingine tunampa nguvu ya ushindani FISADI PAPA aloshindikana kwa maana UKAWA sio taasisi. Kwa nini? kwa nini wananchi wamefikia maamuzi ya kuwapa kura wale wale walowalaani kwa miaka 10 iliyopita? Kwa nini wananchi wanaufanya Uchaguzi huu kuwa baina ya MAFISADI wawili wakubwa waloshindikana japokuwa kuna wagombea wengine watatu wa vyama wasokuwa na Umaarufu kwa Ufisadi. Msimlalamikie Mungu kwani Miafrika Ndivyo Tulivyo - sisi ni WANAFIKI..

Hiyo kesho, siku ya Uchaguzi msishagae tena kuona taasisi ya Kifisadi CCM ikirudi madarakani ama Fisadi Papa akiingia IKULU maghala patakatifu kwa mbwembwe kwani ndio walopewa nafasi kubwa ya Ushindi kuliko wale walotaka kuitumikia nchi yao kwa Uadilifu, Uwajibikaji, Usawa na Uzalendo maana hizi sio sifa wanazozitaka Wadanganyika! Huu ndio mtihani mlopewa baada ya sala zenu na msije mlalamikia Mungu miaka 5 ijayo maana mloyachagua ni kwa hiari yenu wenyewe!

Ujumbe wangu kwa Mwanakijiji na wengine wote wanajanvi hili la JF ya kwamba msiendelee kutafuta Mchawi wala kumlalamikia Mungu kwa sababu sisi wenyewe hatufahamu tunachokihitaji ila tunachokitaka. Imekuwaje leo CCM ya Mafisadi na Fisadi Papa ndo wawe wagombea wakuu wanaotazamiwa kushinda uchaguzi huu japo kuna vyama 22.

Ni kitu gani haswa kilichowavutia wananchi hadi kurudia CCM waloikana kwa Ufisadi ama kumkubali Fisadi aloshindikana ndani ya chama chake leo kawa ndiye mgombea mkuu wa Upinzani!. Ni nani wa kumlaumu hapa ikiwa kesho hiyo wananchi watachagua na kuwapa kura watu wale wale walowananga kwa miaka 10 iliyopita!

Ama kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo!
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,460
2,000
mbona taasisi ya ufisadi imehamia ukawa na walipinga ufisadi huko ukawani wakaondoka wewe umebaki na ukawaipi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom