Mi Nimemueleza aisee

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Huyu shemeji yangu kaniita kando na kunieleza habari kibao kati yake na dada yake ambaye ni wife wangu,kwa umakini sana akiwa anataka mi nianze kumfuatilia wife ila bila kumueleza kama nafanya hivyo.hiyo ilikuwa jana.

Baada ya kukaa na kufikiria sana juu ya kazi ya kuanza kumfuatilia wife kwa siri,nimeona kama namsariti hivyo nimeamua kumueleza kila kitu alichoniambia kaka yake,sasa nina amani.

Najua kuna kasumba ya watu kutegemea kwamba mwanaume akipewa siri za mke wake anapaswa asimueleze mi nimeona kama huko ni kutaka kuniblackmail na kuingilia ndoa yangu hivyo nimeweka wazi na ninajua kesho wife atamchana sana hivyo akiamua kuacha kuniletea umbea wake aache nitaupata kutoka kwa watu wengine na hao wakiniletea namueleza pia.

Alaaaa
 

Anamjungukia dada yake?
Huyo mwanaume anafanya kazi au wewe ndo unamlisha?
Tena mie ningekuwa wife wako ningemnunulia na zawadi ya bikini mpya na cd niliyoburn wimbo wa wanaume kama mabinti wa lady Jaydee.
 
ila wanaume wa siku hizi wambea jamani. Dah dah.
Tena usiombe uwe na mtu wako mwenye pesa zake wakisha nunuliwa safari 2 watasema yaliyokuwemo na yasiyokuwemo.
Wapo wengine kazi yao kushinda kwenye mabar kupiga umbea na vibomu vya chipsi yai.
Nasema WANAUME HAWANA SIRI narudi tena WANAUME HAWANA SIRI.
Na wapenzi wanaolala kitanda kimoja usithubutu kupeleleka umbea utasutwaa na kina Gea habib
 
^^
Siku wakiacha kukuambia,,ukakuta mambo yalishaenda mrama,utawalaumu?
^^
 
dah wewe unaambiwa mke wako anafanya vituko,unaenda kumwambia wife?hakika limbwata linafanya kazi yake,sahau kupewa habari za wife na watu wakijua ndio watakutafunia vizuri
 

We utakuwa unalishwa na huyo Mkeo unaogopa kuachwa, ngoja akuzalie mchina sasa ndo utajuta!
 
Kama hii si ya kutunga basi nakuomba useme ni jambo gani shemeji yako alikuambia. kama ni kuhusu wakati wa makuzi yao na kabla ya ndoa yenu, poa. kama ni mwenendo usio mwema kwenye ndoa yenu, basi kajipange.
SP
 
ha ha ha ha haaaaaa kajisemea ngwair (alale mahala pema marehemu) wajinga ndio waliwao?
 
Kuna wakati mwingine Mungu hutumia wanadamu badala ya malaika kufikisha ujumbe kwa watu wake.
 
Kuna wakati mwingine Mungu hutumia wanadamu badala ya malaika kufikisha ujumbe kwa watu wake.

aiseee hapa ni kwa vile mwanaume kapeleka umbea.
Angekuwa mwanamke habari ingekuwa tofauti kabisa,
we utakubalije mwanaume mwenzako akuletee maneno
 
Utatuletea hapa stori za kumegewa utajifanya unaomba ushauri

"To know the enemy is half the victory"
 
sasa mi sikuelewi unajisifia ulichofanya!!!!!!!!

mbona ni kama ni jambo la ajabu kwa
mwanaume kufanya vitu vya hivyo
 

Sina uhakika kama ulichokifanya ulitumia hekima. Nafikiri ni bora ungekaa kimya kama hutaki kumchunguza mkeo au kusikia jambo baya kuhusu mkeo! Kwa mtu kukueleza tabia mbaya ya mkeo si jambo la kawaida na hivyo ulitakiwa kufanya uchunguzi kwa faida yako mwenyewe. Si kila kinachokuja kwako ni majungu yenye kuharibu familia yako, na ndiyo maana alisema uchunguze. Inawezekana kabisa, huyo shemeji yako ameona dada yake anafanya mambo ndivyo sivyo inhali wewe ni mtu mwenye msimamo. Cha kushangaza, badala ya kufanya uchunguzi, wewe umekimbilia kwenda kusema bila hata kuwa na fact!

Ningelikuwa ni mimi ningechunguza kwanza kupata ukweli. Baada ya kugundua ukweli ningefanya maamuzi. Kama ni kweli huyo kaka alimsingizia dada yake, then ningeweza kumkalisha chini nakumueleza mabaya yake. Na kama ni kweli dada yake ana tabia zisizo njema, pia ningeamua nini cha kufanya.
Binafsi naona umechemka kaka!
 
HorsePower umetumia nguvu nyingi kumpa ushauri. pole, hy jamaa ana matatizo.
He gotta be gay!
 
Last edited by a moderator:
----:yell:
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…