Mheshiwa Rais Dkt. Magufuli, Ukatibu Mkuu wa CCM mpe Abdallah Bulembo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Mheshimiwa Rais wangu mpendwa na ninayekukubali kama ninavyomkubali Yesu Kristo wa Nazareth Dkt. John Pombe Joseph Magufuli najua siku chache tu zijazo CCM tunaenda kukupa UENYEKITI wa Taifa cha Chama chetu.

Najua jukumu lako la kwanza kubwa ni kupanga safu yako na hasa hasa najua ungependa kuanza na nafasi ya KATIBU MKUU wa CCM.

Mheshimiwa Rais Mimi ni Nabii niliyeletwa hapa duniani na Mwenyezi Mungu kuweza kuwaongoza Wanadamu hivyo basi kama ambavyo nilikuchagua Wewe mapema sana kuwa ungefaa kuwa Rais wetu wa Tanzania na kweli UNABII wangu ukatimia sasa leo tena nakupa jina la Mtu ambaye najua atakufaa na kukusaidia Wewe hadi Chama chetu katika nafasi ya UKATIBU MKUU.

Majina yote achana nayo na mpe Mzee ABDALLAH BULEMBO nafasi hiyo ya UKATIBU MKUU na hutojutia kwani KIFALSAFA mnaendana sana na mnafanana pia KIMAAMUZI na KIUTENDAJI.

Usije kusema Nabii sijakuambia au kukumbusha na naomba niishie hapa. Na namalizia tena kusema na kusisitiza kuwa nafasi ya UKATIBU MKUU wa CCM inamfaa tu Mzee Abdallah Bulembo ukikosea hapo hao utakaowapa wengi wao wana " vimelea " vya CHADEMA kama siyo UKAWA.

Nabii naondoka zangu na nimemaliza.

Nikutakie tu majukumu mema Mpendwa Rais wangu na Mwenyezi Mungu akupiganie, akubariki na akufanikishie kila unalotufanyia Watanzania.

CCM juu juuu, CCM daima na sijaona kama CCM Afrika na dunia nzima!
 
Eti wewe ni nabii umeletwa na Mungu kuwaongoza watu dunia!! huoni hata Aibu?
Ni Mungu gani huyo ambaye unautani naye?

Hujui hata kazi za nabii na bado unajiita nabii!! anyway nisikatae sana unaweza kuwa ni nabii wa uongo msaka toke!

Eti wewe ndo ulimchagua hata aibu huoni kudanya umma asubuhi yote hii loo!!

achakujipambanua nafasi za kuteuliwa zimekwisha.
 
Haiwezekani katibu mkuu na mwenyekiti wote watoke kanda ya ziwa huko ni kukigawa chama. Hatutaki polirization

Mkuu kwani kinacho tafutwa ni kitu gani? Ufanisi wa kazi au UKADA, kwa nini siku hizi watu wanakuwa overly sensitive na masuala ya dini, ukanda ukabila nk - kama tunakumbuka vizuri Baba wa Taifa aluwahi kuonya nini kuhusu watu wanao tanguliza hoja za vices tajwa hapo juu kama silaha ya kuwajengea mizengwe watu fulani wasiteuliwe, tusijaribu kumfunga mikono Dk.Magufuli- mwacheni achague watu ambao anajua watamsaidia kwa nia safi kuendeleza Taifa letu bila ya kujali udini,ukanda na ukabila - tujali uwezo wa mtu kufanyakazi mengine ni secondary.
 
Kukosa elimu bwana ni janga, Bulembo ameona hana jinsi ya kujisogeza kwa Magu zaidi ya kuita waandishi wa habari na kujitapa kuwa yeye ana mkubali sana na wassio mkubali Magu eti wafukuzwe, tetheehee niche mie kaj.uaje kama yeye Magu anamkubali? Kweli awamu ya mwendo kasi. hii
 
Naona tumeanza kuelekea sehem mbaya sana ya kumwabudu mwanadamu ! siamini kama mtu mwenye akili timamu anaweza sema ulichokisema kwa kumlinganisha mwanadamu na Yesu Kristo ambaye ni Mungu! Mungu akusamehe na aizuie hasira yake juu yako! Hivi wajua kuwa Mungu akiamua hutapata hata hiyo nafasi ya kukomenti humu achilia mbali hicho cheo au nafasi unayoipigania kwa kujitoa akili hata kufikia kumlinganisha rais ambaye ni mwanadamu na Mungu .
 
Back
Top Bottom