Mheshimiwa Upendo Peneza asisitiza amani akiwa ziarani na Waziri Mkuu

Komeo

JF-Expert Member
May 3, 2011
2,498
1,171

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo Peneza, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
upload_2017-7-14_10-14-16.jpeg
images
images
images

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Upendo Peneza amewaomba wananchi waliombee Taifa liendelee kuwa na amani pamoja na kuwaombea viongozi wa kisiasa, wawe na uvumilivu ili wazidi kusonga mbele kimaendeleo.

Alisema hayo juzi katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Likangara wilayani Ruangwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mkoani Lindi.

“Wananchi wa Ruangwa nawatakia maisha mema ili mzidi kusonga mbele, tuombee amani ya nchi yetu na mtuombee viongozi tuwe na uvumilivu wa kisiasa,” alisema mbunge huyo kijana kutoka mkoani Geita, ambaye bungeni anaongoza Chama cha Wabunge Vijana.

Mbali na Peneza, pia mkutano huo ulihudhuriwa na wabunge wengine ambao ni Hassan Masala (Nachingwea – CCM), Zubery Kuchauka (Liwale - CUF), Hassan Kaunje (Lindi Mjini – CCM) na Hamida Abdallah (Viti Maalumu – CCM).

Kwa pamoja, wabunge hao walisema lengo la kushiriki kwenye ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliwataka wananchi kuhakikisha wanaendelea kudumisha na kuilinda amani iliyopo kwa sababu ndiyo inayowawezesha kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

Alisema licha ya kuwepo kwa matukio machache ya uhalifu yanayojitokeza katika baadhi ya maeneo, vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na mikoa jirani, limejizatiti kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote kwa mtu mmoja mmoja au vikundi.
 
Peneza sio vitu maalumu kutoka kanda ya ziwa? Ruangwa alienda kufanya nini?

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Peneza sio vitu maalumu kutoka kanda ya ziwa? Ruangwa alienda kufanya nini?

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Ni kiongozi wa umoja wa wabunge vijana (wote bila kujali vyama). Kwahiyo alikuwa anawakilisha vijana wote kwenye ziara hiyo ya PM.
Na ni mwakilishi mzuri sana kwakweli.
 
Peneza sio vitu maalumu kutoka kanda ya ziwa? Ruangwa alienda kufanya nini?

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app

Mkuu hata mimi nashangaa sana.

Kama alikwenda kwa mwaliko wa Waziri Mkuu inatia shaka kama kweli viongozi wetu wa juu wanaheshimu na kuthamini demokrasia ya vyama vingi.
 
Ni kiongozi wa chama cha wabunge vijana (wote bila kujali vyama). Kwahiyo alikuwa anawakilisha vijana wote kwenye ziara hiyo ya PM.
Na ni mwakilishi mzuri kwakweli.
Ok sawa na asante sana kwa kunielewesha mkuu

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom