Mheshimiwa Rais wetu msaidie Mama yangu apate haki yake

galelee

Senior Member
Mar 5, 2019
109
348
Mheshimiwa Rais wetu Joseph Magufuli nakupa sifa kwa uongozi wako thabiti katika taifa letu la Tanzania.

Miaka 6 iliyopita mzazi wangu (Mama) alinunua ardhi kwa ajili ya ujenzi kule Chanika ambapo wakazi wa Kipawa walipohamishwa Kipawa kupisha utanuzi na ujenzi wa uwanja wa ndege.

Tulifuata taratibu zote kisheria katika kununua hilo eneo . Tulianza kwa mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo akamuita mmiliki wa kiwanja hicho tukaongozana mpaka halmashauri ya jiji pale Posta ili kujiridhisha kama kweli ni mmiliki wa eneo hilo tukaelekeza na receptionist kwenda kwa mwanasheria wa jiji ni mwanamke kwa bahati nzuri tukamkuta.

Huyo mwanasheria wa jiji akatuambia kuwa tuje kesho yake na kwamba muuzaji aliyetuuzia ardhi aje na documents original yaani hati ya eneo lile na pande zote zije na mashahidi wao, kesho yake tukaenda kama tulivyoambiwa na mwanasheria yule akaandaa mikataba palepale ofisini kwake tukamlipa pesa yake yule muuzaji mbele ya mwanasheria wa jiji tukasaini mikataba ile na mashahidi wa pande zote mbili .

Tukashikana mikono tukatawanyika tukijua kuwa tumekwenda sehemu husika na hatuna wasiwasi na kiwanja chetu tumekinunua hakina tatizo. Mzazi wangu akaanza ujenzi wa nyumba kubwa ilipifikia kwenye rinta akajitokeza mzee mmoja akidai kuwa lile eneo ni lake akafungua kesi mahakamani kesi ikaunguruma miaka kama 3 hatimae akashinda ile kesi kwamba sisi tumevamia eneo lake.

Tumehangaika miaka yote hiyo kujaribu kuupata haki yetu bila mafanikio tumekwenda mpaka kwa kamisha wa ardhi na wakakutana na watu wa mamlaka ya viwanja vya ndege wa hapa Dar kikao kikafanyika lakini hatuoni dalili za sisi kupata haki yetu kumbuka mheshimiwa Rais wetu mikataba ya mauziano imetayarishwa na mwanasheria wa jiji inakuwaje halmashauri ya jiji ikatuuzia kiwanja kumbe kilikuwa na mmiliki kabla? Inamaana mama yangu ni mmiliki wa tatu.

Mheshimiwa Rais sisi hatupingi hukumu ya mahakama na hatun'gan'ganii eneo hilo tunachoomba halmashauri ya jiji na mamlaka ya viwanja vya ndege wahusike kutulipa hasara tuliyopata tumetumia mamilioni kujenga na kununua eneo lile .watutafutie eneo jingine na watulipe hasara yote tuliyopata kuanzia kununua kiwanja na ujenzi wa nyumba ile mama yangu ni mzee analia kila siku kuwa atakufa hajapata haki yake na ni mgonjwa tunaomba msaada wako mheshimiwa Rais wetu asante.
 
Miongoni mwa watu waliopata shida ni hao waliohamishwa kutoka Kipawa na kupelekwa Chanika

Kwanza Chanika ni mbali, kisha viwanja walivyopata huko wengi vina migoro
pia walilipwa hela mbuzi na mabavu yalitumika
 
Mheshimiwa Rais wetu Joseph Magufuli nakupa sifa kwa uongozi wako thabiti katika taifa letu la Tanzania.

Miaka 6 iliyopita mzazi wangu (mama) alinunua ardhi kwa ajili ya ujenzi kule Chanika ambapo wakazi wa Kipawa walipohamishwa Kipawa kupisha utanuzi na ujenzi wa uwanja wa ndege.

Tulifuata taratibu zote kisheria katika kununua hilo eneo . Tulianza kwa mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo akamuita mmiliki wa kiwanja hicho tukaongozana mpk halmashauri ya jiji pale Posta ili kujiridhisha kama kweli ni mmiliki wa eneo hilo tukaelekeza na receptionist kwenda kwa mwanasheria wa jiji ni mwanamke kwa bahati nzuri tukamkuta.

Huyo mwanasheria wa jiji akatuambia kuwa tuje kesho yake na kwamba muuzaji aliyetuuzia ardhi aje na documents original yaani hati ya eneo lile na pande zote zije na mashahidi wao, kesho yake tukaenda kama tulivyoambiwa na mwanasheria yule akaandaa mikataba palepale ofisini kwake tukamlipa pesa yake yule muuzaji mbele ya mwanasheria wa jiji tukasaini mikataba ile na mashahidi wa pande zote mbili .

Tukashikana mikono tukatawanyika tukijua kuwa tumekwenda sehemu husika na hatuna wasiwasi na kiwanja chetu tumekinunua hakina tatizo. Mzazi wangu akaanza ujenzi wa nyumba kubwa ilipifikia kwenye rinta akajitokeza mzee mmoja akidai kuwa lile eneo ni lake.akafungua kesi mahakamani kesi ikaunguruma miaka kama 3 hatimae akashinda ile kesi kwamba sisi tumevamia eneo lake. Tumehangaika miaka yote hiyo kujaribu kuupata haki yetu bila mafanikio tumekwenda mpk kwa kamisha wa ardhi na wakakutana na watu wa mamlaka ya viwanja vya ndege wa hapa dar kikao kikafanyika lkn hatuoni dalili za sisi kupata haki yetu kumbuka mheshimiwa Rais wetu mikataba ya mauziano imetayarishwa na mwanasheria wa jiji inakuwaje inakuwaje halmashauri ya jiji ikatuuzia kiwanja kumbe kilikuwa na mmiliki kabla? Inamaana mama yangu ni mmiliki wa tatu . Mheshimiwa Rais sisi hatupingi hukumu ya mahakama na hatun'gan'ganii eneo hilo tunachoomba halmashauri ya jiji na mamlaka ya viwanja vya ndege wahusike kutulipa hasara tuliyopata tumetumia mamilioni kujenga na kununua eneo lile .watutafutie eneo jingine na watulipe hasara yote tuliyopata kuanzia kununua kiwanja na ujenzi wa nyumba ile .mama yangu ni mzee analia kila siku kuwa atakufa hajapata haki yake na ni mgonjwa tunaomba msaada wako mheshimiwa Rais wetu asante
Kesi za ardhi nchi hii ni changamoto sana...lazima itungwe sheria nzuri juu ya utaratibu mzuri wa uuzaji ardhi.
 
Mkuu kwenye masuala ya ardi kuna USIRIKINA mwingi sana hua unatumika, kuna mtu yeye alinunua kiwanja ila kila akienda anakumbuka tuu kua alinunua sehemu hii ila kiwanja hakikumbuki. Pole sana mkuu, ila kumlalamikia Rais umeweka jumper kubwa mno.
 
nyie endeleeni kumchagua makufuli tuu, mnacho kitafuta mtakipataga tuu……...na bado!
 
Back
Top Bottom