Mheshimiwa Rais, tumia ndege ili kunusuru maisha ya askari

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,692
Sunday, February 7, 2016

Askari polisi watatu wamefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya gari lao lililokuwa kwenye msafara wa Rais John Magufuli kutoka Singida kwenda Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka.

Rais Magufuli alikuwa mjini Singida alikokuwa amekwenda kushiriki maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Hiyo ni mara ya pili kwa askari kufariki wakiwa kwenye msafara wa Dk Magufuli baada ya aliyekuwa akiongoza msafara wake wakati wa kampeni kugongana na dereva bodaboda katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari huyo alikuwa kwenye pikipiki maalumu iliyokuwa ikiongoza msafara wakati Dk Magufuli akitoka katika Hospitali ya Lugalo kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka alisema ajali hiyo ilitokea saa 9.40 alasiri, katika Kijiji cha Isuna, Wilaya ya Ikungi mkoani humo baada ya moja ya matairi ya gari hilo kupasuka na dereva kushindwa kulimudu.
Aliwataja waliofariki kuwa ni Mkaguzi Mwajelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerard.

Dr. JPM tumia ndege utaendelea kuhatarisha maisha ya askari, kwa wadhifa wako kutumia ndege haikwepeki
 
Hiyo ni kweli haina ubishi. Dr. JPM `If you are really serious in cost reduction measures' ni vyema ungetumia usafiri mbadala, maisha ya hao walio angamia ni gharama kubwa sana kwa taifa na familia zao wanao wategemea. TZ hatujafikia hatua ya Mh. Rais kusafiri na gari kwa zaidi ya 150kms. Ni uzembe na umasikini kwa gari iliyo kwenye msafara wa Mh. Rais kupasuka tyre, hiyo ni ishara tu, kuna vitu vingi havipo sawa kwenye hayo magari ya msafara. Tusiharakishe wala tusilazimishe, hatua hiyo tutaifikia pindi mambo yakiwa mazuri. Hivi tumesahau ajali ya Dakawa iliyo muhusisha hayati SOKOINE (RIP). Rais wetu Dr. JPM tunakupenda na tunaendelea kukuombea kwa ALLAH akupe maisha marefu ya kutu-tumikia sisi wananchi wako INSHALLAH.
 
NA waendlee kufa tu...hela za service wananywea viroba kona bar wahuni Hawa!! Mbona huofii kua JPM nae atapoteza maisha au tairi za gar anayotumia yeye ni za chuma ? Au anatumia the Beast??
 
Hata kwenye ndege kunaweza kuwa na ajali. La msingi ni kuweka mazingira ya kuepuka ajali kwa usafiri wa aina yoyote.
 
Sunday, February 7, 2016

Askari polisi watatu wamefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya gari lao lililokuwa kwenye msafara wa Rais John Magufuli kutoka Singida kwenda Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka.

Rais Magufuli alikuwa mjini Singida alikokuwa amekwenda kushiriki maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Hiyo ni mara ya pili kwa askari kufariki wakiwa kwenye msafara wa Dk Magufuli baada ya aliyekuwa akiongoza msafara wake wakati wa kampeni kugongana na dereva bodaboda katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari huyo alikuwa kwenye pikipiki maalumu iliyokuwa ikiongoza msafara wakati Dk Magufuli akitoka katika Hospitali ya Lugalo kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka alisema ajali hiyo ilitokea saa 9.40 alasiri, katika Kijiji cha Isuna, Wilaya ya Ikungi mkoani humo baada ya moja ya matairi ya gari hilo kupasuka na dereva kushindwa kulimudu.
Aliwataja waliofariki kuwa ni Mkaguzi Mwajelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerard.

Dr. JPM tumia ndege utaendelea kuhatarisha maisha ya askari, kwa wadhifa wako kutumia ndege haikwepeki
Singida hakuna uwanja wa ndege,uliza wenyeji utaambiwa!!
 
Sidhani kama hiyo ajali ina uhusiano na kutumia ndege au gari. Kama ajali ipo ipo tu hata katika ndege inaweza kutokea
 
Hiyo 110 ya RTO sidhani Kama Ina uwezo wa kwenda speed ya zile kilimo kwanza za rais au za BMW na pia sidhani Kama ni special order ya kuhimili mbio za msafara wa rais ukiacha hayo matairi kupasuka ndio ishara kubwa zaidi maana gari ya magufuli sidhani kama tairi yake ni hata inajazwa upepo.

Unakuta hata hiyo 110 wameomba tairi za kichina kwa muhindi ili watekeleze majukumu halafu unaiingiza kwenye rally. Acha kabisa. Hata mie nasapoti atumie ndege msafara uwe kutoka airport kwenda RV kwisha.
 
Sidhani kama hiyo ajali ina uhusiano na kutumia ndege au gari. Kama ajali ipo ipo tu hata katika ndege inaweza kutokea

Ila kuna mambo mengine ni contributory na yanaongeza risk kubwa zaidi. Ukiangalia Kama ndio mwanzoni tu wanakufa namna hii je, ikifika miaka mitano itakuwaje?

Rais anasafiri now and then, all over the world inatambulika ya kwamba usafiri wa ndege ni safe zaidi na usafiri kwa gari una risk kubwa sana sasa kwaa nini tusichague usafiri wenye risk ndogo?

Risk sio kwa Mkuu wetu ila hao wanaokuwa kwenye hiyo convoy. Gari ya Waziri au Kama hiyo ya RTO ni za kawaida kabisa kuingizwa kwenye msafara wa rais wakati yeye ana special order na hadi zile tyre sio za kariakoo. Achilia mbali tu ile pikipiki ya sweeper si unaona Ina 240 speed? Lete baja yako halafu iingie kwenye msafara uikaange engine.

So binafsi naunga mkono hoja ya mleta mada
 
Hii inadhihirisha hata police wako rough sio raia pekee. Dereva makini anatakiwa kuwa tayari kwa lolote awapo kwa speed kali
 
Back
Top Bottom