Mheshimiwa Rais naomba unikabidhi Kontena 1 la mchanga nitimize ndoto zangu

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,830
4,726
Kwa nia njema kabisa naomba kukabidhiwa kontena 1 la mchanga wenye madini ili niuze then nifanye mapinduzi ya kilimo cha chakula ktk mikoa ya kusini. Nimeona uwezekano huo upo endapo eneo la Kitere litatumika ipasavyo.

Kwa muda mrefu mikoa ya kusini imekuwa nyuma katika kilimo cha chakula licha ya ukweli kwamba ardhi nzuri na maji yakutosha yanapatikana.

Endapo ombi langu litakubaliwa nitafanya mapinduzi makubwa na ntakuwa na uwezo wa kulisha mikoa ya Lindi na Mtwara, pia nitaajiri vijana wengi sana ikiwa ni pamoja na wataalamu wa kilimo ili kufanikisha project.

Nawasilisha ombi langu na endapo litafanikiwa mtegemee green revolution mikoa ya kusini.
 
Watanzania tunakaribia au tunafika milion 50 je hayo makontena yatatosha? Na ukiangalia wanaomezea mate sio wewe pekee yako.
 
Mkuu nadhani ushaamka kutoka katika ndoto yako

Pesa za rambirambi tuu zinapigwa sembuse ww kupewa contena moja la mchaga
 
Kwa nia njema kabisa naomba kukabidhiwa kontena 1 la mchanga wenye madini ili niuze then nifanye mapinduzi ya kilimo cha chakula ktk mikoa ya kusini. Nimeona uwezekano huo upo endapo eneo la Kitere litatumika ipasavyo.

Kwa muda mrefu mikoa ya kusini imekuwa nyuma katika kilimo cha chakula licha ya ukweli kwamba ardhi nzuri na maji yakutosha yanapatikana.

Endapo ombi langu litakubaliwa nitafanya mapinduzi makubwa na ntakuwa na uwezo wa kulisha mikoa ya Lindi na Mtwara, pia nitaajiri vijana wengi sana ikiwa ni pamoja na wataalamu wa kilimo ili kufanikisha project.

Nawasilisha ombi langu na endapo litafanikiwa mtegemee green revolution mikoa ya kusini.
Mkuu hujui kama eneo la kitere ameuziwa Rais mstaafu wa Marekani?
 
Back
Top Bottom