Regnatus Cletus
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,114
- 959
Mheshimiwa Rais, Shkamoo.
Pole na majukumu, lakini pole pia kwa msiba mzito uliotuchukulia ndugu zetu zaidi ya mia mbili.
Ndugu Rais, natambua una uchungu na hamu ya kuinyanyua nchi yetu iende kwa kasi kubwa, lakini wakati huo huo tunahitaji rasilimali watu, yaani wasomi, tena wasomi imara sio wa kubangaiza.
Taifa lisilo na wasomi, au lenye wasomi dhaifu ni taifa mfu.
Sheria inayounda TCU, yaani tume ya vyuo vikuu Tanzania, inaipa mamlaka tume hiyo kudhibiti ubora wa vyuo vikuu, kusimamia udahili wa wanafunzi, kutengua, kufuta na kusimamisha taasisi legevu. Hilo ni jambo jema kabisa.
Mheshimiwa Rais, nchi hii ilishageuka genge la walanguzi, kama ambavyo unapenda kusema kuwa nchi ilikuwa shamba la bibi. Kila mmoja alipojisikia kuunda chuo chake alikiunda tu wakati wowote kwa malengo ya kupiga na kuchuma pesa.
Mheshimiwa Rais, kwa kuwa TCU ndiyo yenye mamlaka ya kusajili vyuo vikuu kwa kuzingatia vigezo stahiki, ninatumai kabisa maofisa wa tume hiyo waliofanya mchezo wa KUHARIBU elimu yetu kwa kusajili vyuo dhaifu watawajibishwa kikamilifu kwa kupelekwa mahakamani na kuvuna wanayostahili.
Mheshimiwa Rais, natambua umeshachukua hatua kadhaa za kuiwajibisha tume kama vile kuvunja bodi, lakini kwa uzito wa uhalifu, ukengeufu, na uharibifu walioufanya, natumai hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao bila huruma.
Mheshimiwa Rais, leo hii vyuo vikuu kadhaa vimefutwa. Hilo ni jambo jema kabisa. Lakini unaweza kujiuliza ni nani aliyethibitisha usajili wa hivi vyuo?
Unaweza kujiuliza ni nini hatima ya vijana waliokwisha kuhitimu katika vyuo hivyo?
Unaweza kujiuliza ni ipi hatima ya taswira ya wahitimu wa vyuo hivyo katika soko la ajira?
Unaweza kujiuliza ni upi mustakabali wa wanavyuo wanaohamishwa hamishwa chuo kimoja mpaka kingine kila mwaka?
Mheshimiwa Rais, kwanini TCU inavilea vyuo dhaifu kwa muda wote huu? Kuna rushwa? Kuna ubabaifu? Kuna maslahi binafsi? Kuna ushirika haramu?
Nilitegemea mpaka sasa VYUO VYOTE DHAIFU VIWE VIMESHAFUTWA KABISA na hatimaye tukapata suluhu ya kudumu.
Huu utaratibu wa kufuta leo, kufuta kesho, kusimamisha, kufuta usajili, kuhamisha wanavyuo nk.. utaisha lini?
TCU imeshindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo?