Mheshimiwa Lipumba wewe ni jabari timua wote.

Mheshimiwa Lipumba wewe ni jabari timua wote.

leonaldo

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
2,584
Reaction score
3,185
Kwanza napenda kukupongeza kwa juhudi zako za kukijenga chama na kukirejesha mikononi mwako.
Pili sina shaka kuwa kwa sasa unajipumzisha kidogo baada ya kukamilisha kazi abayo imewaacha hoi wapinzani wako kwa ushirikiano wa haja ulioupata toka pande zote zilizotakiwa kutoa ushirikiano"well done" lakini nakuomba jambo moja, katika hilo waombe radhi wanawake wa Tanzania kwa kuwabagua kwa nini hatua yako haikutamalaki hadi kwa wabunge wanaume? Ulipaswa kusafisha wote kwani kuanza upya sio ujinga na haki sawa kwa wote ipate maana,hapo tu ndio ulisahau. Nimewasikia mamluki wakidai eti oh hutathubutu kwa kuwa unapenda sana ruzuku kweli hiyo? Mbona wakati tunaanza haikuwepo na CUF ikamea mikononi mwako.
Mwisho tu kwa msisitizo naomba baba timua na waliosalia ili tuende kwenye uchaguzi nakuhakikishia hawataona ndani utashinda kwa kishindo kwani sapoti yako kwa sasa ni hawa raia, sasa hivi wanataka maendeleo tu na si vinginevyo nakwambia mpaka pemba tutapeta ni wewe tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom