Mheshimiwa Kikwete

NasDaz

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
11,307
Likes
1,611
Points
280

NasDaz

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
11,307 1,611 280
Mheshimiwa Rais wangu, lazima nielze wazi kwamba angalau hadi hapa ulipofikia, nimeridhishwa na utendaji wako haidhuru kwamba kuna mapungufu ya hapa na pale! Wapo wanaukupinga, na wapo wanaokuponda, lakini huo ndio uongozi-ama kwa tafsiri nyingine, ndivyo binadamu alivyo! Hata hivyo, lengo la andiko hili fupi sio kuelezea mapungufu hayo wala mafanikio, bali kutoa taadhali ili nawe usije ukairejea historia! Mimi si msomaji mzuri wa historia, lakini nasikia kwamba pamoja na Mwalimu Nyerere kushindwa vibaya kwenye sera zake za uchumi, lakini alianza vizuri sana wakati wa mwanzo wa uongozi wake! Nahisi ni kweli, dalili ya jambo hilo hadi leo zinaonekana kwavile kama kuna chochote ambacho tulikiuza kwa wawekezaji basi kitega uchumi hicho kiliwekezwa na uongozi wa baba wa Taifa (p..bu.h)! Kuna sababu mbalimbali zinazoelezwa kwamba zilikuwa ndio chanzo cha kushindwa vibaya kwa Baba wa Taifa kwenye masuala ya uchumi, hata hivyo suala hilo si dhima ya andiko hili, na badala yake interest yangu ni kuonesha ni namna gani marais wetu wanavyoanza vizuri na kuishia kwa kuvurunda, ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya!
Baaada ya kung’atuka kwa Baba wa Taifa, Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi akapewa jukumu la kuongoza Jahazi! Ni bahati mbaya sana kwamba bado nategemea simulizi za hapa na pale kuhusu uongozi wa Mzee Mwinyi, kwavile wakati huo bado nilikuwa mdogo pia! Hata hivyo, pamoja na udogo niliokuwa nao wakati huo, ni kama nakumbuka kuna kitu kilikuwa kinaitwa FAGIO LA CHUMA!!! Kwamba, wakati Mzee Mwinyi anaingia madarakani, pamoja na mambo mengine vilevile alikusudia kufagia uchafu wa aina yoyote uliokuwa unaendelea serikalini na taasisi zake! Hapo ndipo lilipokuja suala la FAGIO LA CHUMA! Wale ambao wakati huo walikuwa wakubwa kiasi cha kuweza kufuatilia mustakabali wa taifa hili, bila shaka wanaweza kutukumbusha kama sio kutusimulia simulizi za FAGIO LA CHUMA LA MZEE MWINYI!! Inasemekana wakati Mzee Mwinyi anaaanza, ilikuwa ni fagio la chuma kwelikweli! Hebu tujuzeni wale ambao wakati ule bado tulikuwa vibwa-mdogo! Nasikia hata Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba nae alikuwa Waziri Mkuu wa Mzee Mwinyi kabla hajamvua madaraka!!! Ina maana Warioba nae alikumbwa na hilo FAGIO LA CHUMA, au yalikuwa ni mabadiliko ya kawaida ya uongozi?! Kwa maajabu ya Firauni, wakati wa msimu wake wa mwisho wa uongozi ulipowadia, FAGIO la Mzee Mwinyi likapoteza dira na badala yake likaanza kusomba matakataka kwenye madampo yote makubwa nchini na kuyarundika IKULU!!! Heshima yote ya IKULU ikapotea!!! Kaingia kwa mbwembe na katoka akiiacha Ikulu inanuka kwa kila aina ya uvundo!
Hauchi, kunakucha-Bravo Chinga Boy Benjamin William Mkapa akaingia madarakani! Ashukuriwe aliyeanzisha mbio za vijiti duniani! Hata kama wakati anaingia madarakani bado sikuwa mkubwa lakini angalau nilishaanza kuvutiwa na suala zima la mustakabali wa nchi yetu! Form III sio kidato kidogo ati! Sio siri kwamba Mheshimiwa Mkapa aliikuta nchi inachungulia kaburini! Pamoja na mambo mengine, akaanza kwanza kuondosha mauchafu yaliyopo Ikulu yaliyokuwa yameachwa na uongozi wa Mwinyi! Mkapa akaibua nidhamu ya matumizi ya serikali na mambo mengine kadha wa kadha! Akaunda Tume ya Jaji Joseph Warioba kwa nia ya kuchunguza mianya ya rushwa nchini! Miaka mitano ya kwanza, akafanya vizuri ile mbaya! Lakini historia ikajirudia, Mheshimiwa Mkapa nae alipokuwa anajiandaa kuondoka, akarudi dampo na kuzoa matakataka na kuyarudisha tena IKULU kama alivyokuwa amefanya Mzee Mwinyi! Akaondoka akiwa ametuachia vizungumkuti lukuki ambavyo vilihitimshwa na EPA!
Mheshimiwa Rais wangu, napenda kukumbusha kwamba tabia hii Watanzania tumeshaishitukia kwahiyo tusingependa nawe ufanye kama waliokutangulia! Tabia ya kuanza vizuri na kumaliza vibaya kwa makusudi haivumiliki mheshimiwa! Suala la kwamba hutapigiwa tena kura kwahiyo hamna cha kuhofia si uzalendo. Hofu yangu ni kwamba, uozo uliooneshwa na viongozi wawili waliokutangulia katika mihula yao ya pili ulitokana na ukweli kwamba walifahamu wasingesimama tena jukwaani kuomba kura za wananchi!! Nataka kushawishika kwamba wao hawakuwa wazalendo na badala yake, wewe nakuvika kofia ya uzalendo. Mzalendo wa kweli anajali maslahi ya taifa bila kujali endapo atasimama jukwaani kuomba kura au hapana! Mheshimiwa rais, nimeonelea kukumbusha mapema zaidi kwavile mipango yoyote yenye nia ya kuivuruga nchi huwa pia inaandaliwa mapema!! Naamini kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu utajitahidi kadri uwezavyo uonekane mtoto mzuri zaidi! Hivyo wenzako wote ndivyo walivyokuwa wanafanya! Lakini sitarajii kwamba baada ya kurudi tu Ikulu, nawe utaanza kusomba mauchafu toka kwenye madampo na kuyarudisha Ikulu kwavile ukishatoka hapo 2015 hutarajii kurudi tena! Ya ANBEN yanatosha haturajii tuyasikie ya JAKSAL! Nakutakia uchaguzi mwema!
 

Facts1

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Messages
308
Likes
5
Points
0

Facts1

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2009
308 5 0
Mheshimiwa Rais wangu, napenda kukumbusha kwamba tabia hii Watanzania tumeshaishitukia kwahiyo tusingependa nawe ufanye kama waliokutangulia! Tabia ya kuanza vizuri na kumaliza vibaya kwa makusudi haivumiliki mheshimiwa! Suala la kwamba hutapigiwa tena kura kwahiyo hamna cha kuhofia si uzalendo.
Waliomtangulia angalau walianza vizuri kipindi cha kwanza na kumaliza vibaya kipindi cha lala salama tofauti na Kikwete yeye ameanza vibaya ni vigumu sana kama atamaliza vizuri. Tutegemee kipindi cha pili ndio kitakuwa worse zaidi kwa sababu anajua hatagombea tena.
Tatizo la Kikwete ni very weak katika leadership has no commanding power which is a foremost tool in good governance sio kwamba hana washauri ila washauri wake wengi hawamtakii mema yeye na Tanzania.

Wote Kikwete na Mzee Mwinyi ni weak in leadership tofauti yake na Mzee Mwinyi ni kwamba Mwinyi alikuwa na wasaidizi wengi wazuri kama Mzee Warioba na hata bado alikuwa anabebwa na Mzee Kifimbo. Kwa hiyo maamuzi mengi ya Mwinyi yalitegemea ushauri toka kwa Kifimbo kitu ambacho Kikwete hana.

Chinga Boy ana-commanding power kubwa ila tatizo lake alikuwa hashauriki akiamua kitu hakuna wa kumzuia na yeye alikuja kuathirika na uhuru wa kipindi cha pili ndio maana hata akajiingiza kwenye biashara akijua hakuna atakayekuja muuliza, matokeo yake kavurunda kwenye dakika za majeruhi.

Kifimbo yeye alikuwa ndiyo serikali ndiye waziri mkuu ndiye waziri wa fedha nk maamuzi yote alikuwa akiyafanya yeye, nakumbuka siku moja waziri fulani wa fedha aliitwa na rais ikulu alitoka pale wizara ya fedha anakimbia kwa miguu aliona gari litamchelewesha, Kifimbo alikuwa kifimbo bwana kwa sisi tuliokuwa kipindi chake tunamjua.

Umegusia suala la uchumi, uchumi wetu ulianza kuteteleka nafikiri kuanzia mwaka 1973 mara tu baada ya vita ya kwanza na Uganda ikifuatiwa na sera ya vijiji vya ujamaa 1974/5 nao ulichangia kwa kiasi fulani, watu walitolewa kwenye aridhi zao za asili zenye rutuba na kurundikwa sehemu moja, mifugo mingi ilikufa kwa magonjwa na msongamano mazao pia yaliathiriwa na ukame wa 1975. Ufukara wa kutupwa ulianza kuongezeka. Uchumi ulikuja kuhitimishwa na vita ya pili na Uganda 1978.
 

NasDaz

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
11,307
Likes
1,611
Points
280

NasDaz

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
11,307 1,611 280
Unaweza kuwa ulikuwa na jambo la kusema ila uandishi wako bado dogo kazana!
Nilichotaka kusema nimeshasema, ulichotarajia wewe niseme sio changu mimi bali chako wewe kwahiyo unaweza kukisema!! Kuhusu suala la uandishi wangu bado sikuelewi labda kwavile bado dogo kama unavyosema ingawaje nahisi bado ulitarajia niandike kama vile ambavyo wewe unaandika!!
 

Forum statistics

Threads 1,191,691
Members 451,730
Posts 27,717,594