Ukiacha gharama ulizotaja, zipo nyingi ambazo mara nyingi watu hatuzitilii maanana. Kwa mfano:
1. Mwezi Juni kulikuwapo maonyesho ya utumishi hapo Mnazi mmoja. Kila idara ya serikali na kila shirika la umma lilikuwapo. Ukiacha gharama za kukodi mahema na kuyapamba kuna gharama nyingine km kukodi meza na viti, posho ya watumishi wote wanaoshiriki na kwa siku zote za maonyesho, gharama za vipeperushi na public address system, takrima kwa wazito wanaotembelea vibanda, n.k. Lakini muhuimu zaidi, kila mshiriki lazima awe na uniform...T-Shirt na kofia vya bei ya juu.
2. Baada ya Juni, Julai kulikuwa na maonyesho ya 77. Gharama ni kama za hapo juu, bila kusahau chakula na usafiri kwa kila mshiriki. T-Shirt na kofia za 77 lazima ziwe za 77.
3. Mwezi Agosti kuna sherehe za 88...sijui wapi. Gharama hivyo hivyo na per diem ya kuwa nje ya kituo cha kazi. T-Shirts na kofia...kama kawa.
4. Sasa kuna maonyesho pale Mnazi mmoja ya kila wizara...miaka 50 ya uhuru. Huenda hata mioani yapo. Gharama za kila idara na kila wizara kuwa na uniform yake nk inachefua. Hivi majuzi Wizara ya Afya 'painted red' Mnazi Mmoja grounds! By the time tunamaliza maonyesho ya miaka 50, gharama hizo na zile za maonyesho mengine kwa mwaka huu peke yake zingepunguza kwa kiasi kikubwa adha ya mgao. Kwa hiyo napendekeza hatua ya kwanza, umma uhamasishwe kuzuia maonyesho hayo...tubaki na maadhimisho ya Desemba ingawa hata hayo ni mzigo usio na tija!