WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
TBC hapa kuna Waziri akutumia muda mrefu kweli kwenye majumuisho ya Wizara yake...
anataja waheshimiwa kibao waliochangia kwenye majadiliano, kwa majina...na kumalizia..Mheshimiwa ....."mbunge".Hii imefanya atumie muda mrefu sana wakati sisi wanancho tunachotaka ni kusikia hoja na siyo majina.
Najiulizayafuatayo:
Kuna ulazima gani kuwataja majina na ubunge wao?
Je mtu asiye mbunge angeweza kuchangia?
Nini mantiki ya orodha hiyo badala ya kujibu hoja?
Niwie radhi bibie Samawati.... nakutakia kila la kher!
Hivi huu mtindo wa kumtambulisha ama kumuita mtu kwa kutumia fani yake mbele ya jina lake umeanza lini? Manake siku hizi mtu ukiwa mhandisi basi utaitwa 'mhandisi' flani wa flani...ukiwa mhasibu utaitwa 'mhasibu' flani wa flani.
Labda mimi kumbukumbu yangu ni ndogo lakini hapo zamani wahandisi, wahasibu, n.k. hawakuitwa kwa fani zao. Ila sasa naona huu utaratibu umeshika kasi sana. Sijui kwa nini tu?
ninavyofikiri mimi ( naweza nisiwe sahihi), enzi za mwalimu, wanasiasa walikuwa wanasiasa na wenye fani zao walikuwa kwenye fani. Ni miaka ya sasa tu tunaona wenye fani wakipigana vikumbo majimboni kugombea ubunge! Na pia ni miaka ya sasa tunaona kila mwanasiasa akihangaika sana kupata shahada ya uzamivu (phd) na kufanya phd iwe kama cheti cha darasa la 12!
Huenda kuna sababu pia ya kujaribu kujitofautisha na wale wasiokuwa na shahada au "professions adimu"!
Ninavyofikiri mimi ( naweza nisiwe sahihi), enzi za mwalimu, wanasiasa walikuwa wanasiasa na wenye fani zao walikuwa kwenye fani. Ni miaka ya sasa tu tunaona wenye fani wakipigana vikumbo majimboni kugombea ubunge! Na pia ni miaka ya sasa tunaona kila mwanasiasa akihangaika sana kupata shahada ya Uzamivu (PHD) na kufanya PHD iwe kama cheti cha darasa la 12!
Huenda kuna sababu pia ya kujaribu kujitofautisha na wale wasiokuwa na shahada au "professions adimu"!
sababu yeyote ile lazima pia tufanane na dunia inavyokwenda......
Wewe umewahi sikia
mheshimiwa professa condoleeza rice....
Sisi ndo wasomi saaana wa dunia au?????????
sababu yeyote ile lazima pia tufanane na dunia inavyokwenda......
Wewe umewahi sikia
mheshimiwa professa condoleeza rice....
Sisi ndo wasomi saaana wa dunia au?????????
Boss,
Kama kuna kitu kinanifanya nione aibu mbele ya wenzetu ughaibuni ni hulka yetu watanzania (hata wanaijeria ) kupenda kujitukuza kwa "credentials' .Haishangazi kuona kila mtu akitaka kuitwa Dr tena kwa muda mfupi sana - miaka 2 !
Siyo siri PHDs siku hizi ni kitu cha kawaida na wengi wanazo tena wanazipata wakiwa na umri mdogo in their 30s na huwezi kuona mtu anajitutumua kujulikana ni Dr X,Y,Z! Na hata hawapendi kuitwa Dr.... kama ni doctoral degree..na wanapenda kujiita kwenye maandishi zaidi -mfano: The Boss..( Phd)!
Inabidia tuanze kampeni kupunguza matumizi mabaya ya "Dr".Wajiite madaktari wa binadamu tu ili tuwatambue kwa urahisi tunapotaka huduma!
Inabidia tuanze kampeni kupunguza matumizi mabaya ya "Dr".Wajiite madaktari wa binadamu tu ili tuwatambue kwa urahisi tunapotaka huduma!
Hii kampeni isianze na kuishia kwenye u-Dr. tu. Hata wahandisi, wahasibu, mawakili, na wengineo manake huko tunakokwenda sasa hata hakueleweki. Sitashangaa siku moja Michuzi naye akaanza kujitambulisha kama 'Photojournalist Issa Michuzi'.....au Kibonde kuanza kujiita 'Presenter Ephraim Kibonde'.
Mtu ni raisi wa nchi lakini bado unaitwa Dr. tena udokta wenyewe wa kupewa mezani. Sielewi kabisa mimi.

WOS..
I am sure ukisafiri umewahi pia kukuta kwa mfano mtu
ni ceo lakini hata kwenye bussiness cars yake unakuta jina tu na adress ya kampuni..
sasa ukija sisi....
unakuta ceo.director general,dr,shaaban malinyingi,.mjumbe wa nec ccm....
yaani aibu zingine bana....