Mhe. Zitto Kabwe katika picha akiwa Colombo, Sri Lanka

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Ukweli husemwa:

Kwa wale wanaomtafuta Mbunge Zitto Kabwe, anapatikana hapa akiwa ametanguliza uzalendo kwanza itikadi za kisiasa baadaye.....






Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika ukumbi wa MNelum Pokuna Mahinda Rajapaksa kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofunguliwa leo na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Aliye pembeni yake ni Mjumbe wa CPA Tawi la Tanzania na Mbunge wa Kigoma Mhe. Zitto Kabwe.


Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akifuatilia kwa umakini ratiba ya ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) kabla ya ufunguzi rasmi leo Mjini Colombo Sri, Lanka, aliye kushoto kwake ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho na Mhe. Zitto Kabwe na aliye kulia ni Mhe. Mussa Azzan Zungu. Mkutano huo umefunguliwa rasmi leo na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Mahinda Rajapaksa.

Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akiteta jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho pamoja na Mhe. Zitto Kabwe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) leo Mjini Colombo, Sri Lanka. Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Wa Kwanza kulia ni Afisa dawati wa CPA tawi la Tanzania Ndg. Said Yakubu.

Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mbunge toka Uganda (hakufahamika jina mara moja) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Henry Chimundu Banda (katikati) mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka. Kulia ni Mhe. Hamad Rashid Mjumbe wa CPA tawi la Tanzania.


Wajumbe wote wa Mkutano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi leo.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.


Picha Kwa hisani ya Issamichuzi.blogspot.co.uk
 
naona kambebea mzigo wake huyu mama
nina swali eti why most people hate Zitto?
 
Kwa wale ambao hamjawahi toka nje ya bongo (yaani wale mliozoea kwenda moshi na kwingineko mikoani) kwa taarifa yenu msione hawa waheshimiwa wakiwa huko wanatanua! La hasha kwanza sehemu kubwa ya watu duniani wana tamaduni tofauti. Hivyo ukiwa huko wala hakuna atakaye kupenda (kama tulivyo watanzania na upendo wetu wa 100%). Kwa hiyo mchukulieni Mh Zitto alienda kuwakilisha wala siyo eti kajipendekeza kwenda kutanua.
 
picha bila kutuambia faida za hiyo safari binafsi naona ni kujaza server..
 
1.JPG


"unaonaje Kamati ya Bunge ya Nishati na madini ukaniacha kidogo km hawatanipigia kelele unawazima kabisa"

" hawawezi mm nilishakataa Mwongozo wa kila mara nani atathubutu wee?
 
Huu ni upuuzi hizi picha zipo kwenye blogs kibao, sasa sijaona what is the meaning of this photos here, hii siyo habari, na wala thread hii haikidhi vigezo kukaa hapa jukwaa la siasa labda jukwaa JF Photos au jukwaa la celeb. pls mods move this.
 
Wapiga picha ni watu wabaya sana yaani wameona kupiga begi la Madame speaker ndio.kitu sahihi duh sina neno hata hivyo Bi Makinda ni kama Mama kwa Zitto so amemsaidia
 
Haya Na wale wanaomtafuta JK huyu hapa.
Naona sasa hili Jukwaa la siasa limevamiwa.


[h=3]RAIS KIKWETE KATIKA ZIARA RASMI YA KISERIKALI YA SIKU TATU NCHINI KENYA[/h]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake wakiingia Ikulu ya Nairobi Jumanne, 11 Septemba , 2012, alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar na kuhsoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Olive Mugendi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na ujumbe wake na wenyeji wakiongea na wanahabari na kisha kupiga picha ya pamoja baada ya Mazungumzo yao Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.PICHA NA IKULU.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom