masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,410
- 14,119
Uchu wa madaraka unapopitiliza kwa kujaribu hata kukwepa matakwa ya wananchi wenyewe waliowaweka wanansiasa madarakani, mwisho wake ni aibu.
Mh Sitta pamaoja na sifa yake ya "Speed and Standards" lakini spidi ya safari hii ilikuwa inaeleekea kuzimu.
Pamoja na maoni ya Tume ya Warioba , ambayo ni maoni ya wananchi, juhudi nyingi zimewekwa kuyaondoa maoni hayo na kuweka maoni ya wanasiasa.
Pamoja na UKAWA kuwa ni wa vyama vya upinzani, lakini katika hili wameonyesha kidogo uzalendo wa kupigania maoini ya wananchi.
Pamoja na hili tunamshukuru Mh JKikwete kwa kuliona hili ili nchi isiingie mtafaruku usio wa lazima.
Hata wana CCM kama Mwigulu Nchemba waliliona hili na mapema.
Hivyo basi ni aibu iliyoje kufikia sasa kuwa hela ya kodi za wananchi imeliwa , na muda mrefu sana umetumika na hakuna cha maana cha kuonyesha kwa matumizi haya ambayo yangeepukwa kwa kutikia maanani maoni ya wananchi.
Maoni ya wananchi mengi sana hayakuwa kichama wala kidini wala kwa manufaa ya kikundi chochote.
Ni mategemeo yetu kuwa walioshinikiza kuendelea na mchakato mufilisi wawajibike kisheria au kisiasa kwa hili.

Na Benedict Luhenga,MAELEZO Dodoma
VIONGOZI Wakuu wa Vyama vya siasa vyenye Wabunge
vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) wamekuwa katika mashauriano ya
zaidi ya mwezi mmoja tangu tarehe 2 Agosti mwaka huu huku wakishauriana juu ya
mwenendo wa mchakato wa Katiba Mpya na jinsi ya kuwa na uchaguzi ulio huru na
wa haki hapo mwakani
Akiongea kwa niaba ya viongozi wengine wa kituo hicho,
Mwenyekiti wa TCD, Mhe. John Cheyo amesema kuwa Katika mashauriano hayo
yaliyochukua sura ya Kamati ya Makatibu Wakuu, Kamati ya Wenyeviti wa Vyama vya
CCM, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi katika hatua tofauti.
Mhe. Cheyo ameeleza kuwa kamati zote zilitoa taarifa
zao kwenye vikao vya Viongozi Wakuu wa Vyama (Summit) ya TCD ambayo wajumbe
wake ni Wenyeviti, Makamu Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama wanachama.
< Mhe. Cheyo aliongeza kuwa katika kutafuta maridhiano,
Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama walifanya mashauriano na Mhe. Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete siku ya tarehe 31 Agosti mwaka huu, hivyo tarehe Nane
Septemba, 2014 hapa Dodoma wakatoa tamko lao
Pamoja na kazi ya msingi inayofanywa na Bunge Maalum
la Katiba, mchakato wa Katiba unaoendelea sasa hauwezi kutupa Katiba
itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kuwa muda hautoshi kukamilisha
mchakato na kufanya mabadiliko yatakayohitajika ya Sheria, Kanuni na Taasisi
mbalimbali zitakazohitajika", alisema Mhe. Cheyo
Mhe. Cheyo aliendelea kwa kusema kuwa, kwa mujibu wa
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mwisho wa mchakato ni kura ya maoni
itakayofanyika mwezi Aprili 2015
"Kama itabidi kura irudiwe kwa mujibu wa Sheria
iliyotajwa, kura itarudiwa mwezi Juni au Julai 2015, muda ambao Bunge la Jamhuri
ya Muungano linatakiwa livunjwe kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015 na
ili Katiba Mpya itumike katika uchaguzi Mkuu utakaokuja, itabidi uhai wa Bunge
na Serikali uongezwe zaidi ya 2015, jambo ambalo hatuliungi mkono", alisisitiza
Mhe. Cheyo.
Akiongelea juu ya Tangazo la Serikali GN Na 254, Mhe.
Cheyo amesema kuwa Bunge Maalum la Katiba kwa sasa linafanya kazi kwa mujibu wa
Tangazo la Serikali (Government Notice) Na 254 lililotolewa na Mhe. Rais
Kikwete tarehe 1 Agosti, 2014
"Tangazo hilo litatumika hadi tarehe 4 Oktoba, 2014
ambapo Katiba inayopendekezwa inategemewa kupatikana, Wajumbe walikubaliana
hatua hii iachwe ifikiwe", alisema Mhe. Cheyo
Kuhusiana na Kura ya maoni, Mhe. Cheyo ameeleza kuwa
kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Bunge hilo kumaliza
kutunga Katiba, ingefuata hatua ya kura maoni kuthibitisha Katiba
"Kwa kutambua kuwa hatua ya kura ya maoni italazimisha
uchaguzi mkuu 2015 kualishwa, basi hatua hii iailishwe, na mchakato wa Katiba
uendelee baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015", alisema Mhe. Cheyo
Sambamba na hayo, Mhe. Cheyo ameishauri Serikali
kuchukua hatua za kisheria ili matayarisho kwa ajili ya Uchaguzi wa Vijiji,
Vitongoji na Mitaa, yaanze haraka iwezekanavyo ili uchaguzi ufanyike mapema
hapo mwakani
Aidha, amegusia kuhusu Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 akasema kuwa, kwa vile Uchaguzi Mkuu wa
2015 utafanyika kwa kutumia Katiba ya 1977, kuna umuhimu kufanya mabadiliko
kidogo (minimum reforms) katika Katiba pamoja na sheria ya Uchaguzi
yatayowezesha nchi kufanya uchaguzi huru na wa haki
"Tayari mambo yafuatayo yamekubaliwa, kuwa na Tume
Huru ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi, Mshindi wa Uchaguzi wa Rais ashinde kwa
zaidi ya asilimia 50% (50%+1)", alisema Mhe. Cheyo
Viongozi hao Wakuu wa Vyama wamempongeza Mhe. Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa ujasiri wake na imani yake katika kuimarisha
demokrasia nchini na kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya nchi.