Nianze kwa meseji hii niliyotumiwa na Mkuu mmoja wa shule. "Kaka wapi, naomba unirushie 20,000/=, nipo hapa Morogoro mjini nimetoka mlimani leo, nilifika kutoa pesa ya matumizi ya shule.
Afisa elimu nimemfuta anipitishie hundi yangu kaniambia nirudi tena bush niitishe Kikao cha Bodi kipitishe kwanza bajeti ya shule na pili bodi iridhie kufanya manunuzi.
Nimechanganyikiwa nauli kurudi kijijini 10,000 nikishuka napanda pkpk 10,000 tena. Jumla nauli 40,000/= kuja na kurudi. Kuitisha kikao cha Bodi wajumbe 10 nalipa kila mmoja 20,000/= bado sahani ya wali maharage.
Pesa niliyoingiziwa 360,000/ Katika pesa hii asilimia 35 ni uendeshaji wa shule (vitambulisho, shajala, maandalio,ulinzi, umeme, maji na fedha za kujikimu. Na fedha za kijikimu isizidi asilimia kumi ya fedha hizo za asilimia 35. Walimu wa sayansi wa kujitolea nimeshawaachisha.
Kwani mwongozo haujawazungumzia kabisa. Kwa hiyo hapa Fizikia,hisabati, biolojia na kemia vijana hawafundishi tena, nirushie tafadhari nataka nilipie chumba sasa hivi hakuna gari za kurudi bush mpaka kesho".
Huyu atatoa wapi pesa ya kuitisha kikao cha Bodi , bure bila posho watakuja kweli na maisha yalivyo magumu vijijini na mkwara wote wa Magufuli pesa zimeingizwa mabilioni ole wake Mkuu wa shule atakaye zipiga?
Mhe. Simbachawene usiogope kumwambia ukweli Magufuli elimu itakufia, potelea mbali akutoe uwaziri kwani ubunge si utabaki?.