Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Nikiri kuwa naunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha maisha ya watu wake na kulinda amani na utulivu. Naunga mkono juhudi zote za Serikali za kuboresha na kuimarisha miundombinu na nyanja nyingine za kimaisha.
Lakini,najua hata watawala wanajua kuwa maisha ni uhalisia. Maisha ya watanzania hayapo kwenye makaratasi ya kiserikali wala tovuti; yapo mitaani na watanzania wanayaishi. Tangu shule za msingi,tumefundishwa kuwa mahitaji makuu ya mwanadamu ni chakula,malazi na mavazi.
Mhe. Rais,mtanzania yeyote akiyapata mahitaji hayo hata yale ya hadhi yake,mtanzania huyo huona nafuu ya maisha yake. Mhe. Rais,mfumuko wa bei za bidhaa ni mkubwa na wananchi wako walio wengi hawawezi kumudu. Wananchi hawali vya kutosha,hawanunui mavazi mapya wala kujenga makazi mapya au bora.
Mfumuko wa bei unasababisha maisha magumu kwa wananchi. Mhe. Rais tafadhali tusaidie katika hili. Bidhaa muhimu kama unga,sukari,maharage,mchele na mafuta zimepanda bei katika hali ya kuogofya. Wananchi wako,kupitia mimi,tunawasilisha ombi letu. Wategemewa tunakiona cha mtema kuni!