Mhe Rais kama unavyokumbuka sakata la Escrow ni sakata la UFISADI lililowahi kulitikisa Taifa hili. Sasa hivi mbivu na mbichi zimeanza kuanikwa HIVYO sisi Watanzania tuliokuchagua kama mkombozi wetu tunakuomba wahusika wote wafikishwe mbele ya sheria. Awe ni kigogo wa aina gani wafikishwe Mahakamani. Kamwe hatuwezi kukubali,Wagonjjwa wanakosa madawa mahospitalini, watoto wetu hawana madawati, Miradi ya maendeleo haitekelezwi kule ngazi chini sababu ya watu wachache ambao hata hawafiki kumi ndiyo wanachota fedha zote hizo. Serikali ya awamu ya nne ni Serikali iliyotuangusha sana sisi Watanzania.