Mhe. Rais Magufuli, Anza na Kusaini Hati za Wote Waliohukumiwa Kifo, Wanyongwe Haraka Haraka Mpaka..

hivi, ungekuwa na mtoto wako amehukumiwa kunyongwa, au hata amekamatwa china alafu unamsikia kiongozi wako uliyempigia kura anasema wanyongwe haraka, utajisikiaje? uchungu wa mwana anaujua mzazi. wakati mwingine mtu akiwa madarakani watoto wake wanasoma ulaya, wanakula vizuri, wanalindwa na mabodigadi hawapati shida yeyote anasahau kuwa kuna watu wameugua hadi bp kwasababu ya watoto.alafu leo unatangaza kwamba wanyongwe, si ndo wazazi wao bp zitapanda zaidi? tuwe wakweli tusipepese macho.

yatupasa kupigana vita hii kwa kukata mzizi. hao mapunda sio target kubwa sana na walitakiwa hata adhabu wapunguziwe, ila hao matajiri ndio wabaya. hata hivyo, hata kama angekuwa tajiri, kuamuru mtu anyongwe ni ukatili wa hali ya juu sana and i hope legal and human rights centre wanaopambana kupinga adhabu ya kifo kwamba ni ya kikatili watalisemea hili. badala ya kuokoa maisha ya mtu unaamuru anyongwe, halafu akinyongwa yule aliyedhurika atarudi kwenye hali yake?
 
Magufuli anataka waliohukumiwa kifo China wanyongwe naye tunamuomba amnyonge ACP Bargeni aliyewaua wafanyabiashara wa madini wa morogoro tuone ujasiri wake
 
Sidhani Huko Yuko Sana Pascal Ila Kuna Kitu Zaidi Ya Hiko Haiwezekani Kama Propaganda Hii Kiboko
Wakati anaambiwa mayalla maana yake ni "njaa"nadhani ulikuwa ujumbe mzito.
 
Huyu nadhani kati ya hao kuna mmoja anamdai
 
Hata kama ni ndugu yako kahukumiwa kunyongwa WACHA maneno WEKA kamba kwa shingo
 


Yaani wewe tangu ulipomwuliza rais swali na akakujibu kwa utani basi umekuwa ukiandika vitu vya hovyo na vyenye mwelekeo wa kujipendekeza kwenye huu utawala,sio kwamba marais ambao hawakusaini utekelezaji wa adhabu hyo walikuwa dhaifu,hapana ,bali wanajaribu kwendana na dunia ya leo na hasa shirika la haki za binadamu ambalo kwa mda mrefu lipo kwenye kampeni ulimwenguni kote kuzitaka nchi wanachama na wale ambao sio wanachama kufuta adhabu ya kifo,na pia hao walikamatwa China na nchi mbali mbali how sure kama wanamakosa tajwa kweli,je kama wamebambikiwa ama kusafirisha bila kujua?
Mungu anasamehe na kutoa nafasi ya pili iweje binadamu tushindwe hata kuwafunga maisha na kazi ngumu?
yote haya unayafahamu ila kwa makusudi unayaacha na kuandika yale yanayowapendeza wakubwa,si bure huenda kuna kitu unakitafta
 
Demokrasia iko kwa wenzetu huko ambako mahakama inaweza kutengua agizo la raisi bila kujali kama yeye ndio anawapa pesa ama vp. Mr Trump chalii.
 
rudia kusoma kwa makini hili umuelewe mwandishi
 
Pasco mbona hii inshu ya kunyonga umeikomalia sana?
Huu ni uzi wa pili ama wa tatu kama sikosei
 
Wakati anaambiwa mayalla maana yake ni "njaa"nadhani ulikuwa ujumbe mzito.


πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Hilo Siwezi Kulisemea Ni Wa Kwetu Huyo, Ni Upepo Mbaya Tu Umempitia Ila Akipata Hewa Safi Atarudi Kwenye Hali Yake Ya Kawaida Shaka Ondoa​
 
@Pasco tufautisha kati ya ujasiri na ukatili please,mfano Mkwawa alikua ni jasiri na fulani utawala wake ulikua wa kikatili na kupandikiza chuki
Bye bye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…