Magufuli shujaa, ataka 68 wa madawa wanyongwe! Kikwete alikuwa dhaifu mno, aliomba wasinyongwe!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,689
119,326
Wanabodi,
Declaration of interest.
Huu ni msimamo wangu binafsi kuhusu adhabu ya kifo.

Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo
Adhabu ya Kifo: Jee kweli bado inahitajika?

Unajua anaetekeleza adhabu ya kifo hufikishwa Mahakamani baada ya kazi hiyo?
https://www.google.com/url?sa=t&source=web&rct=j&url=/amp/www.jamiiforums.com/threads/wana-jf-tuungane-kusema-no-hukumu-ya-kifo.48620/%3Famp%3D1262299130&ved=0ahUKEwju5feRjY3SAhXqDsAKHf7aB6YQFggYMAA&usg=AFQjCNE5hYjBow7hOaZbNvP6acQ0p3bANw&sig2=OypLb7y4n7sf6a94khysUA

Jana katika kutaja idadi ya Watanzania waliofungwa magarezani nje ya nchi, kuna Watanzania 68 waliohukumiwa kunyongwa nchini China.

Rais Magufuli ameonyesha ushujaa mkubwa kutaka Watanzania hawa Wanyongwe tuu na kuzitaka balozi zetu zisishughulike na wahalifu hawa.

Rais Kikwete alikuwa dhaifu sana, wakati wa utawala wake, badala ya kuwaacha wahalifu hawa Wanyongwe, yeye ndio kwanza aliwahurumia.

Wakati wa ziara ya rais wa China, akawaombea msamaha Watanzania hao wasinyongwe na badala yake wafungwe vifungo vya maisha.

Huu ni udhaifu wa hali ya juu. Huruma ya Kikwete kuwaombea msamaha ni kufuatia baadhi ya hao wanaokamatwa they are genuine innocent hawakujua wamebebeshwa nini, after all wanaokamatwa ni wabebaji tuu, ambao ni vidagaa vikanyongwe huku mapapa wakiendelea kupeta na kutafuta vidagaa wengine.

Wakati nikihudumu Ubalozi wa Uingereza, kitu chenye thamani na umuhimu nambari moja kwa ubalozi huo ni maisha ya raia wa Uingereza. Hakuna kitu Uingereza inathamini kama haki kwa raia wake. Raia yoyote wa Uingereza akikamatwa kwa kosa lolote, kitu cha kwanza kufanywa ni kwa Consular Officer wa ubalozi huo kwenda kumtembelea mtuhumiwa huyo na kuhakikisha anahudumiwa vizuri ikiwemo kumpatia huduma ya kwanza ya wakili, kisha kuwasiliana na jamaa zake. Haki hizo hupewa kwa British subjects wote hata Watanzania waliorejea nyumbani Tanzania, wazazi wao na ndugu zao wote wako Tanzania lakini as long as ana hold a British passport, anahudumiwa.

Naamini ombi la rais Kikwete kuwaombea msamaha Watanzania wasinyongwe China kulifuatia makubaliano fulani ya maandishi, hivyo kwa amri mpya ya Magufuli ya jana, Wizara ya Mambo ya Nje itawabidi watume Note Verbale nchini China ili kuulifuta lile ombi la Kikwete, ili kuruhusu Watanzania hao sasa Wanyongwe rasmi.

Kiukweli huruma na upendo ikizidi sana hugeuka udhaifu, Rais Kikwete alikuwa Dhaifu sana, lakini Rais Magufuli ameonyesha ushujaa wa hali ya juu kutaka waliohukumiwa kunyongwa Wanyongwe tuu! .

Maamuzi kama haya ndio yanaweza kulisaidia taifa kusonga mbele, hongera sana Magufuli kwa kujivua udhaifu wa Kikwete. Na Pole sana Rais Mstaafu Kikwete, ulikuwa na upendo sana, utu sana na huruma sana ulipalekea kushamiri sana kwa biashara hii. Huu ni udhaifu, kama angeachwa Wanyongwe, saa huzi hata idadi ya wafungwa ingepungua maana wengi wao wangekuwa wameisha nyongwa.

Paskali
Rejea
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa hakuna muuza unga yeyote ataweza kunyongwa kwa kosa la kuuza madaya ya kulevya bali ataishia kufungwa jela.
Update.
Kwa vile mimi ndio mwanzisha mada, na kuna mada mtu unaanzisha with the motive behind, amini usiamini, japo hazisemwi, lakini mada kama hizi zimesaidia sana kuleta mabadiliko chanya ya the desired changes, sasa imebaki kufutwa tuu rasmi kwa adhabu ya kifo, toka kwenye vitabu vyetu vya sheria.


Thanks for changing for the better.

Paskali

========
China haitawanyonga Watanzania
Ni wale waliokamatwa na dawa za kulevya na kuhukumiwa nchini humo.
By Pamela Chilongola, Mwananchi
Dar es Salaam. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imesema watu 15 waliokamatwa na dawa za kulevya nchini China, hawatanyongwa na badala yake watafungwa maisha nchini humo kutokana na mawasiliano mazuri ya kidiplomasia baina ya Tanzania na China.

Kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo mtu yoyote anayekamatwa na dawa za kulevya adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.

Akizungumza jana na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya watu wa China nchini mwaka jana, Xi jinping, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Haule alisema nchi hizo mbili zina uhusiano wa muda mrefu na wa kidugu katika nyanja za siasa, uchumi, usalama na jamii.

Haule alisema kutokana na uhusiano mzuri kwa nchi hizo mbili kwa kushirikiana mambo mbalimbali, hivyo wafungwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa hawatanyongwa na badala yake watafungwa maisha.

“Tunaushirikiano mkubwa sana ndiyo maana Watanzania waliohukumiwa kunyongwa sasa hivi hawatanyongwa tena na badala yake watatumikia kifungo cha maisha gerezani,” alisema.

Haule alisema mwaka huu nchi hizo mbili zinajivunia kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano ya kidiplomasia ambayo imekuwa na mafanikio katika nyanja mbalimbali.
alisema Haule.
 
kuna tatizo!baba mwenye nyumba anakuwa mkali bila kufikiri mara mbili,matamshi,matamko yake yanajuwa na ukakasi sana siku hizi .
Baba mwenye nyumba anakosa huruma kwa watoto wake,sio wote wanao hukumiwa wanakuwa na hatia,nakumbuka miaka ya nyuma kidogo hapa JamiiForum kuna member alitoa ushuhuda kuwa akiwa kwenye ndege kuna jamaa mnigeria alimzoea ghafla,wakiwa wanashuka malaysia aiport ,mnigeria akamuomba amsaidie begi lake dogokwa kuwa anamabegi mengi,jamaa hakumuamini akakataa kwa kuwa alikuwa hawaamini wanaigeria,alipofika kwenye ukaguzi yule mnaigeria alidakwa ana madawa kwenye lile begi dogo la mkononi.Wote tunajua Malaysia dawa za kulevya ni death penalt hamna mjadala.Je hapo utasema wote wanaokamatwa ughaibuni na dawa za kulevya wanamakosa?

serikali isikwepe kusaida wanachi wake waliopo nchi za nje sio wote wana kuwa na hatia.Jambo kubwa linalotakiwa kwenye hii vita ni Elimu ya kutosha kuhusu madhara ya madawa ya kulevya,kiukweli kama hujawai kuwa na ndugu addicted huwezi kujua madhara yake kwa familia.
Kitu kinacho nishangaza madawa yakikamatwa polisi wanakimbilia kutaja dhamani ya madawa badala ya kutaja madhara,utasikia wanataja haya madawa yana dhamani ya billion 10 badala ya kutaja yakiingia sikoni yataleta madhara gani. KWANINI vijana wasio na ajira wasishawishike kubeba hayo madawa tumboni?
nawasilisha.......
 
Hivi na wewe siku hizi umeanza kupotoka...katika masaibu ya Dunia ya leo kuna kusingiziwa..kupachikiwa kesi...kuzushiwa ..chuki...fitina...na mengine mengi wajua kabisa kuna watu wanaweza kuwa wameonewa nashauri kufanyike vetting tu ili wachukuliwe hatua kali.
 
Kama kweli Kikwete alikuwa na hizo tabia basi hakuwa mdhaifu, mtu mwenye utu na hizo sifa nyingine ulizotaja kamwe haziwezi kuwa udhaifu ndugu.

Kiufupi hizo sifa unazompa Kikwete hata hakuwa nazo.

Halafu kunyonga binadamu wenzako hata siyo ushujaa, ukimnyonga huyo mhalifu unafaidika na nini?
Tunapigania hiyo adhabu ya kunyongwa/kifo ifutwe kote duniani sasa wewe unampamba kwa ushujaa anayeamrisha watu wanyongwe!

Fikiri angekuwa ndugu yako mmoja kule amefungwa ungefurahia anyongwe?
Au ndiyo wewe upo gerezani ghafla unaskia mtu anataka unyongwe hapo vipi?
KUNYONGA WAHALIFU SIYO SULUHISHO LA KUZUIA WATU KUTENDA UHALIFU.

"WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA".
 
Unasoma uzi maudhui yake yanakufanya kila unapoingia aya mpya unalaani kimoyo kimoyo, kama si posts kuondolewa na kuhaririwa kuna wahusika wengine kwenye maudhui wanastahili kulaaniwa tu.
 
Kwahiyo wakinyongwa tutafaidika kwa lipi? Kwanini wasinyongwe waliokwapua mabilioni ya Escrow,radar,meremeta,meli mbovu? Huu ni unafiki uliokithiri.
Kwani hao wakinyongwa tunafaidika na nini?Bora haya mafisadi kuliko wanaoharibu vijana kwa uzezeta!Unajua Zanzibar Valium huuziwi hata kama unaumwa?jamaa wanazisaga kama 200 wanatia maji kidogo unakuwa kama uji wanakunywa!
 
Back
Top Bottom