Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, aweza kujiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, aweza kujiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ntamaholo, May 18, 2012.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,107
  Trophy Points: 280
  Wana jamvi salam.

  Waziri mpya wa nishati na madini, anaweza kujiuzulu kama kweli hatoendekeza siasa za CCM. Nasema siasa za CCM kwa kuwa yeye mpaka kuteuliwa kwake kuwa waziri wa wizara hiyo inayohesabu hasara kila mwaka, hakuwa kwenye siasa na wengi tulitarajia uwajibikaji uliotukuka.

  Bodi ya wakurugenzi TANESCO, ilikutana mjini dodoma kwa lengo la kuangalia namna ya kuwasimamia watendaji wa Tanesco ili wizara hiyo isiingie tena katika kashfa. kati ya wana bodi, yumo ROBERT MBOMA aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi.

  Ni kwa kutumia uzoefu wake, watendaji wa TANESCO waliamliwa kuwakatia wadaiwa sugu wa umeme na kwa kuanzia Jeshi la wananchi JWTZ na Jeshi la polisi, walikatiwa umeme tangu 16 may 2012 hadi 17 may 2012 umeme uliporudishwa majira ya saa nne usiku, na hili ni kwa jeshi la polisi, sijajua jeshi la wananchi ilikuwaje.

  Majeshi yote walifika tanessco na kuambia wameagizwa kukata umeme na viongozi wao kwani JWTZ wana deni la bilio 6, huku jeshi la polisi wana deni la bilion 5.

  kama umeme umerudishwa:-

  1. Je madeni hayo yamelipwa?
  2. Kama hayajalipwa, je waziri au watendaji wake wameamliwa kurudisha umeme kwenye taasisi hizo?
  3. Kama wameagizwa na mamlaka za juu, je si kuingiliwa?

  NB. Ikumbukwe kuwa majeshi yote huwa yanawasilisha bajeti, sasa kudaiwa hadi bilion tano, na sita fedha ya bajeti kwa matumizi ya umeme zilitumikaje?

  my take.

  Namshauri waziri, kama hawajalipa madeni hayo wakatiwe ili kuleta nidham ya matumizi ya fedha za walipa kodi na kama akilazimishwa kuwapa umeme, basi abwage manyanga kwani mda unakuja naye atatakiwa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia wizara yake
   
 2. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  mkuu ntamaholo, nimeshudia hapa mwanza wanajeshi na polisi wakiwa ofisi za tanesco mkoa wakiomba kurejeshewa umeme. lakini mwanamama ambaye ndiye meneja aliwakatilia kuwa wanatekeleza maagizo ya wakubwa wo na hawana jinsi.

  kati ya hizo bilioni tano za polisi, inasemekana kwa mkoa wa mwanza wanadaiwa milion 400/tsh. na sijui ni kwa mda gani.

  kama wangendelea kuwakatia, ingeleta adabu kwani inabidi uchunguzi ufanyike kubaini pesa zilitumika kwa matumizi gani, lakini naona wamewaogopa majeshi
   
 3. a

  arinaswi Senior Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  huu ulikuwa mwanzo mzuri lakini naona kulindana bado kupo palepale!
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kuhusu Prof muhongo nadhani tuzidi kumpa muda kwani ni mchapa kazi ingawaje tatizo linakuja ktk maamuzi ambayo huingiliwa na maamuzi ya siasa.

  lakini kikawaida majeshi yote hupewa bajeti ya maswala ya nishati,maji na n,k sasa kama deni limekuwa kubwa kiasi hicho hapo lazima kuna ulakini,ni vyema jeshi livae uhusika na walipe madeni yanayowakabili
   
 5. A

  AZIMIO Senior Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa uteuzi wa huyu waziri hapa Rais amenikosha sana tumpe muda.
   
 6. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,107
  Trophy Points: 280
  serikali ya J.K kulindana ni sera yao, kwenye nchi zinazoongozwa kwa matakwa ya sheria, Muhongo was right na angesaidia kuleta nidham ya matumizi yaliyotengwa kwenye bajeti. lakini naona kesha tishiwa.

  wakati tukijadili suala hili mtaani, tulifikiria na polisi waanze kufanya kazi zao na waanze na hao tanesco, magari yao yote yakamatwe, yakaguliwe, na kwa vile magari mengi ni mabovu kila gari likipatikana na makosa 10, kwa tanzania nzima wangeweza kuzikusanya hela zao na baada ya miezi sita wangelipa. hii ingesaidia kuwa na magari ambayo ni imara na mazima kabisa, nidham ingerejea
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,107
  Trophy Points: 280
  ninachokiona wamerejeshewa umeme bila kulipa deni. unadhani deni litalipwa hapo? na tanesco wanakiri mitambo ya downs na iptl ndiyo inayozalisha umeme, mitambo ya maji iko hoi kwa kukosa maji ya kutosha, hivyo zinatakiwa shekeli za kutosha kuwalipa wawekezaji wanao wauzia tanesco nishati
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,107
  Trophy Points: 280
  tumpe mda, lakini asije kuwa anapotezwa......
   
 9. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli usiofichika kuwa madeni mengi ya serikali husababishwa na hazina yenyewe kwa kutoa fedha kidogo au kwa kuchelewa sana kwa wizara/taasisi na hivyo kusababisha kuwepo kwa madeni.

  Ni bora utaratibu ukabadilishwa ili bajeti kwa ajili ya huduma kama umeme, maji, simu nk kwa ajili ya serikali yenyewe na majeshi ibaki hazina na hazina iwajibike kulipia huduma hizo.

  Tatizo la msingi ni kuwa mara nyingi fedha iliyoidhinishwa katika bajeti ni nadra sana kutolewa yote kwa sababu lengo la makusanyo halifikiwi au serikali kufanya matumizi nje ya bajeti ya serikali iliyoidhinishwa!
   
 10. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  wadau hv tanesco haiwezi kufanya utaratibu wa kuweka mita za luku kwa kila wizara ili kuondokana na malimbikizo ya madeni
   
 11. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  wazo zuri
   
 12. M

  Mkira JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35


  itakuwa SUPA sana tena wawekewe LUKU hata katika shule zote sekondari za serikali na ofisi mbali mabli za serikali.
  PROF MUHONGO FANYA HIVYO KWANZA ITASAIDIA KATIKA KUPUNGUZA GLOBAL WARMING MAANA OFISI NYINGI ZA SERIKALI NA JUA LOTE LA BONGO HUWA ZIMEWASHA TAA NA KUOTEZA ERNGY BURE NA KUJIONGEZAE DENI LA TANESCO BUREE!!

  PIA itasaidiwa watu wawe conscious kuhusu matumizi ya umeme maana wengi ni kuwash taa tu! siku moja nilingia katika ofisi fulani mchana kweupe nikazima ta zao na kuwaeleze huo mwanga wa jua si unatosha? mmoja wao akaniuliza IMEKUUMA SANA KUONA TAA ZINAWAKA!
   
 13. papason

  papason JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Unaandika kitu usichokijua huyu jamaa sospeter muhongo yupo CCM tangu miaka ya 80s, tena ana ka nyazifa ka ujumbe ndani ya ccm ambako sikakumbuki vizuri! hivyo hilo ni gamba lililo komaa ndani ccm
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  TANESCO bwana mteja ni mteja anayedaiwa wekundu na mwingine billion 6 katia umeme hao.
  Na kwa kuanzia bajeti kwa ajili ya kulipia umeme huwa inaenda wapi kuna haja ya kuitrace
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  kamfedhehesha sana balozi wa marekani kwenye lift.
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Dr. Mwinyi anatakiwa atoe majibu kwa nini JWZ wana deni kubwa kiasi hicho? Hawakuwa na kifungu cha kulipia umeme kwenye bajeti zake? Hela zimeenda wapi na nani ameidhinisha matumizi tofauti na yale yaliyopitishwa na bunge?
   
 17. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,107
  Trophy Points: 280
  tatizo wao wenyewe mita ni sehemu wanapofanikisha wizi. kubambika bila ni zaidi ya polisi wanavyodhaniwa kubambika kesi. mfumo wa luku hawaupendi eti hauingizi mapato, halafu hawawaibii wateja
   
 18. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,107
  Trophy Points: 280
  nakushukuru kwa taarifa, laikini ameanza vizuri na tayari wameshamzingua. tusubiri tuone
   
 19. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,107
  Trophy Points: 280
  imebidi nijihakiki, na mimi nimekuta taa zinawaka, nimeamua kuzizima hapa kibaruan kwangu. kila mtu achunguze hilo
   
 20. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwenye Bajet walitengewa hizi pesa sasa wamepeleka wapi?.... Aliyekuwa Waziri wa Jeshi la wananchi na Mambo ya Ndani wanatakiwa kuwajibika...

  Hao mameneja wanatakiwa kukataa kurejesha umeme hadi malipo.
   
Loading...