maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,028
- 1,348
Kuna baadhi ya shule binafsi (English medium) hapa jijini Mwanza zimetoa masharti ya kulipa kati ya tshs 85,000 na 100,000 kwa ajili ya picha na usajili wa mitihani ya taifa ya kidato cha pili mwaka huu.
Kibaya zaidi baadhi ya shule zimeanza hata kuwafukuza wanafunzi ambao hawajalipa karibu wiki moja sasa.
Tunaomba maelekezo ya mheshimiwa waziri Ndalichako au ofisi ya Baraza la Mitihani la Taifa kama malipo haya ni ya halali kulipwa au ni mwendelezo wa kuwaibia wazazi.