Mhe. Kikwete Hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Kikwete Hii imekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GAGL, Apr 17, 2011.

 1. G

  GAGL Senior Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli nashindwa kuelewa serikali yetu chini ya mhe Kikwete inaelekea wapi. Kwa sasa mafuta ya aina zote namaanisha dizeli, petrol na mafuta ya taa ni sh. 2000 kwa lita. Sasa najiuliza anakuwa na ujasiri gani wa kuwaambia wauza sukari washushe bei wakati gharama za kusafirisha ni kubwa kiasi hiki. Mhe. serikali yako haina mpango wowote wa kuwawezesha vijana wengi wasio kuwa na ajira japo hata kwa kuwapa mitaji, sasa unategemea katika hali ya kupanda kwa gharama za maisha hivi waishi vipi bila ajira? Akitokea mtu wa kuwashawishi waingie mtaani kuandamana kudai unafuu wa maisha utawaambia wanahatarisha amani? Maana nashindwa hata kuona faida ya hiyo amani kama watu hawana amani moyoni tena wale walio nguvu kazi ya taifa. juzi naibu waziri wa fedha ameongea juu ya kutunisha mfuko wa mkopo kwa wabunge na wafanyakazi wa serikali, lakini hakuzungumzia kuhusu mfuko wa kuwawezesha wahitimu wa vyuo wanaotaka kujiingiza katika ujasiriamali. Hii inasikitisha sana, sijui kama unaelewa kuwa ukosefu wa ajira ni bomu zaidi ya yale ya gongo la mboto. Tukimbilie kwa mjomba gani kumpelekea shida zetu wakati wewe unaelewa na hauchukui hatua? Mnatuambia tuunde vikundi ili tuwezeshwe, mimi ni mwanakikundi, lakini ukweli ni kwamba hakuna hata ofisi moja ya serikali yako ambapo watu wanaweza pewa fedha za kuendesha miradi waliyobuni, sana utajibiwa kuwa, ofisi inafanya kazi ya kuwa-recomend kwa wafadhiri tu. kama mimi muongo, tazama kazi inayofanyika idara ya vijana chini ya wizara ya habari na pia tume ya uwezeshaji ya taifa, hakuna kitu pale, kulipana mishahara tu. Kali nikikaa na kufikiri naona elimu niliyopata imefanya kazi ya kuwafirisi wazazi wangu kwa kunilipia karo na bado hadi leo bado wanaendelea kunisaidia fedhe ya matumizi, ajira za kuajiriwa hakuna wakati tunaambiwa uchumi unakua, kuwezeshwa kijasiriamali pia hakuna, zimebakia siasa tu, manataka tufanyeje?
   
 2. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Rejea tungo za Mzee Mwanakijiji za sujui
   
 3. G

  GAGL Senior Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani haya ni maisha yanayozungumzwa hapa, inakera sana mtu unaweka vitu vya maana hapa halafu mtu anajibu upuuzi, kwani lazima ujibu? kama **** kuna grammatical error na haujaelewa, uliza ueleweshwe na siyo kuandika mabo yasiyo kuwa na maana. Ni tatizo sana kwa vichaa kuwa sehemu ya jamii ya watu wenye akili timamu.
   
 4. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu unamaanisha nini?..

  Mbona sinza madukani sukari kilo sh. 1600 tena ni kwenye min-supermarkets za sinza.
   
 5. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Swali: Mheshimiwa Rais je unawajua wamiliki wa kampuni ya Dowans?


  Jibu:
  Nasema mimi sijui, ni kina nani sijui,
  Wanatoka wapi sijui, walifikaje sijui,
  Kama nawafahamu sijui, kama wananijua sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Mheshimiwa Rais, lakini waliingia nchini na kupata Mkataba wa Richmond na kuleta majenereta katika kutekeleza mpango wako wa kupunguza tatizo la umeme nchini kweli huwajui?


  Jibu:
  Nasema mimi sijui!, kwanini walikuja sijui,
  Uhusiano wao siujui, Kama nao Richmond sijui,
  Waliingia kwa lipi sijui, na walirithishana vipi sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini ulisema kuwa Richmond ni kampuni Hewa kama Kamati ya Mwakyembe ilivyoonesha na kudai, na ukatoa pongezi! Unawaeleza vipi Watanzania kuwa Taifa liko tayari kuheshimu mkataba wa kampuni ya kitapeli?


  Jibu:
  Nasema tena sijui!Kama kampuni hewa sijui,
  Kama ni matapeli sijui, Kama walibebwa sijui,
  Wahusika kina nani sijui, Mwakyembe alijuaje sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!
  Tulikoanzia sijui, tumefika vipi sijui,
  Nahusika vipi sijui, nimuulize nani sijui,
  Niwaridhishe vipi sijui, nianzie wapi sijui!
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini Rostam Aziz ametajwa kuhusika kuanzia mwanzo wa sakata hili na yeye mwenye amekiri kuhusika na hili kwanini usimuulize ili ujue?


  Jibu:


  Nitamuanza vipi sijui, Rostam huyu sijui,
  Kama mwingine sijui, anahusika vipi sijui
  Nimuamini nani sijui, kama ni kweli sijui!
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini, inawezekana vipi usijue wakati una vyombo vingi vya usalama ambavyo vingeweza kukupata taarifa mbalimbali za kiinteligensia kama walivyoweza kuzipata kule Arusha na kuvunja maandamano ya Chadema? Kwanini hujapatiwa taarifa za kiinteligensia kuhusu Dowans?


  Jibu:


  Intelligensia mimi sijui, nani anipe sijui,
  Kwanini wanipe sijui, nifanye nayo nini sijui,
  Wasiponipa sijui, kama nadaganywa sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Nani awaagize sijui, kama nini mimi sijui,
  Au makamu sijui, Waziri Mkuu sijui,
  Wajitolee tu sijui, au ni Bunge mimi sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Sasa msimamo wako wewe binafsi kama Rais ni upi, Dowans walipwe au wasilipwe?


  Jibu:


  Msimamo gani sijui! Kama ninao sijui,
  Nilikuwa nao sijui, nitakuwa nao sijui,
  Kama walipwe sijui, na wasilipwe sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Wizara ilipe sijui, Au Tanesco sijui,
  Au huko hazina sijui, au hapa Ikulu sijui,
  Bunge litenge fedha sijui, au Mahakama sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Sasa mheshimiwa inaonekana hujui mambo mengi tu; kuna mambo mengine yoyote unayoyajua?


  Jibu:
  Kwanini masikini sijui, Kagoda ni nani sijui,
  Meremeta nani sijui, Dipu Grini nani sijui,
  Mbona elimu duni sijui, wanagomea nini sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Sijui mimi sijui, mengine mengi sijui,
  Ya kilimo siyajui, ya Sayansi siyajui,
  Mambo ya maji sijui, umeme ndiyo sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!
  Kama napendwa sijui, kama nachukiwa sijui,
  Nafurahiwa sijui, au nakejeliwa sijui,
  Kama ninachekewa sijui, au nakebehiwa sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Mheshimiwa swali la mwisho; asante sana kwa kutupa nafasi hii na kwa hakika umetuelewesha na tumeelewa kuwa hujui mambo mengi sana. Labda uwaambie Watanzania, je wewe ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?


  Jibu:


  Sijui mimi sijui, ninarudia sijui,
  Kama miye sijijui, mtajuaje sijui
  Kama najua sijui, kama sijui sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji -BGM)
   
 6. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Nimecheka sana leo.
   
 7. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,237
  Trophy Points: 280
  qwi qwi qwiqi qwi qwi qwi qwi! Teh he he hehe hehe! Daaaah, kazi kweli kweli
   
Loading...