Mhe. Joseph Selasini na CHADEMA kuweni makini na huyu mtu

Ni Mimi Msiogope

JF-Expert Member
May 28, 2012
352
200
Muda mrefu sasa tumekuwa tukishuhudia meneno ya chinichini kuwa Mhe.Joseph Selasini kuwa ameshindwa ku deliver kwa Wananchi kama alivyoahidi,au amekuwa 'upande wa serikali'.

Mimi Kama mwananchi waMahida Rombo ambaye nilitumia nguvu na muda wangu kuhakikisha kuwa CHADEMA tunalinyakua jimbo kwa kishindo naona sasa kuna vitu vinavyoendelea ambavyo ni hatari kwa CHADEMA Rombo na pengine Taifa mwaka 2015.

Kuna kijana mwenzetu anaitwa Edward Kinabo ambaye aliangushwa kwenye kura za maoni ambaye huyu yupo karibu sana na Viongozi wa CHADEMA ngazi za juu na amekuwa akimchongea wazi wazi Mhe. Selasini maneno ya Uzushi na uongo uliopitiliza. Kwa ushahidi wa E.Mails ambazo amekuwa akizituma kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA hasa John Mrema, Basil Lema na Mhe. Freeman Mbowe ni wazi kuwa lengo lake halikuwa zuri wakati akionyesha nia ya kugombea nafasi hiyo ya Ubunge. Badala yake sasa baada ya kukosa amekuwa akitekeleza mbinu zifuatazo;

1. Amekuwa akiwapigia simu Baadhi ya Wananchi wa Rombo (Mimi nikiwa Mmoja wao) akimponda Mhe. Selasini na kuwa eti "Alijua tu".
2. Amekuwa akisambaza E.Mails kwa wanachama wa CHADEMA akimpaka matope Mhe.Selasini (Ushahidi upo Zaidi ya 168mails)
3. Amekuwa akishirikiana na Mtu mmoja anayeitwa Emmanuel ambaye naye alibwagwa kwenye kura za maoni kwa CCM na kupanga njama kadhaa za kumsemea vibaya Mhe. Selasini ndani na nje ya CHADEMA.

Kwa ujumbe huu nawatahadharisha Mhe. Selasini na Viongozi wengine wa CHADEMA kumuangalia kwa jicho la tatu huyu mtu mwenye Tamaa ya Ubunge tangu 2010 hadi sasa ameukosa lakini bado anamchafua kiongozi aliyechaguliwa na wananchi bila sababu ya Msingi.
 
Selasini mwambie aendelee kutoa shukruani... maana list ilikatishwa kutokana na muda....
 
Selasini mwambie aendelee kutoa shukruani... maana list ilikatishwa kutokana na muda....

Natambua uwepo wenu humu mnaotumiwa na Masalia ya Kura ya maoni lakini mngeonekana wa Maana kama mngetumia uwezo wenu wa kufikiri Kumshauri Mhe.Selasini Badala ya kumchafua... Hiyo haiwasaidii ever!.

Badala ya Kujenga chama mnaanza kutengeneza makundi ambayo kimsingi ndiyo yanayokiua Sisiemu!... What a shame!:shetani:
 
kwenye namba moja hapo kuna kauli hii ' nilijua tu''

naomba ufafanuzi hapo maana simu hiyo alipiga kwako....alijua nini....funguka
 
Wassira alisema...CHADEMA haifiki mwisho wa mwaka itakuwa imesambaratika!kaanza Zitto...Dah
 
kwenye namba moja hapo kuna kauli hii ' nilijua tu''

naomba ufafanuzi hapo maana simu hiyo alipiga kwako....alijua nini....funguka

Anadai kuwa Alijua kuwa Mhe.Hawezi kuongoza Rombo kitu ambacho si kweli... Anacho Deliver Mhe.Selasini Huku Rombo tunakiona tunaoishi humu.. Yeye Mwenyewe anaishi Dar mbona haji huku kuona kinachoendelea? Kama ana nia njema na Mhe. Selasini kwanini asimpe ushirikiano watekeleze ilani ya CHADEMA na kutimiza ndoto za wengi Rombo???
 
Natambua uwepo wenu humu mnaotumiwa na Masalia ya Kura ya maoni lakini mngeonekana wa Maana kama mngetumia uwezo wenu wa kufikiri Kumshauri Mhe.Selasini Badala ya kumchafua... Hiyo haiwasaidii ever!.

Badala ya Kujenga chama mnaanza kutengeneza makundi ambayo kimsingi ndiyo yanayokiua Sisiemu!... What a shame!:shetani:
Tumshauri nini? mwambie atekeleze ahadi zake tu... kazi kutoa shkruni dk10
 
Tumshauri nini? mwambie atekeleze ahadi zake tu... kazi kutoa shkruni dk10

Kama huna Ushauri kwa mtu basi huna sababu ya kumkosoa
"Ikiwa unajua tatizo, na hujui namna ya kulitatua tatizo basi wewe ni sehemu ya Tatizo"
 
Selasini ni mtu mnafki ndani ya chama na amekuwa akitetea posho waz waz nani asiemjua hata ukimsafisha na jiki asafishiki tena ni mchumia tumbo nambari one na si mpambanaji wa kweli hana tofauti na kaka yake lamwai
 
Jamani eeeh kama anaboronga kipimo ni 2015 mbona unamsemea kwa mdomo wakati sasa hivi kazi na vitendo tu
 
Back
Top Bottom