Mhasibu ahukumiwa jela miaka 23 kwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh. 4.3 mil Ngorongoro

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Habari wanaJF,

Mhasibu wa Baraza la Wafugaji Wilaya ya Ngoongoro, Loserian Raphael Laizer, amehukumiwa kwenda jela miaka 23,baada ya kutiwa hatiani kwa kusababishia hasara serikali zaidi ya shilingi milioni 4.3 kwa kuandaa orodha hewa ya majina ya wanafunzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha, Juventus Baitu, amesema Mhasibu huyo alihukumiwa Machi 18 mwaka huu, mbele ya hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Ngorongoro Dimitrio Nyakunga.

Amesema mtuhumiwa huyo alitiwa hatiani kwa makosa manne ya matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri, hivyo kila kosa alihukumiwa kifungo cha miaka minne na kosa la kuisababishia hasara serikali alihukumiwa kwenda jela miaka saba.

Baitu amesema mtuhumiwa alikuwa Mhasibu wa baraza hilo ambalo liko chini ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na alifikishwa mahakamancha kwa mara ya kwanza na TAKUKURU Mkoa wa Arusha, kupitia wilaya ya Ngorongoro Juni 6 mwaka 2013.

Amesema shauri hilo lilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ngorongoro na kusajiliwa kwa ECC.Na. 4 ya mwaka 2013 mbele ya hakimu Mfawidhi wa Wilaya Dimitrio Nyakunga.

Amefafanua kuwa jumla ya makosa aliyoshitakiwa nayo ni matano, ambapo kati ya hayo manne yalihusiana na matumizi ya nyaraka zenye maelezo ya uongo kwa lengo la kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha sheria yakuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007.

Baitu amesema kosa la tano lilihusiana na kuisababishia hasara serikali kinyume na aya ya 10(i) kifungu cha 57 (1) na 62 (2) cha sheria ya Uhujumu uchumi kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Amesema mtuhumiwa akiwa kazini alitayarisha nyaraka za uongo akiwa mhasibu wa baraza hilo kwa kuandaa orodha ya majina ya wanafunzi wanaodhaminiwa na Baraza la Wafugaji na kuwalipa ada na posho za kujikimu, wakati ni hewa.

Baitu amewaasa watumishi wa umma na wananchi kutojihusisha na vitendo vya rushwa na wananchi wakatae vitendo vya rushwa.
 
Escrow B 320 hakuna aliyeguswa,Yona na Mramba 11 B wanafagia hospital pale sinza,huyu only 4m analabwa 23 years.kweli Tz kuna kwenye nchi na wasindikizaji
MHASIBU WA BARAZA LA WAFUGAJI WILAYA NGORONGORO LOSERIAN R. LAIZER , AMEHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 23, BAAADA YA KUTIWA HATIANI KUISABABISHIA HASARA SERIKALI ZAIDI YA MILIONI 4.3 KWA KUANDAA ORODHA HEWA YA MAJINA YA WANAFUNZI
 
Mbona wale waliokwapua mabilioni wamepewa kifungo cha nje???DUh pesa ndiyo sabuni ya roho,inasafisha hata adhabu za mahakama.Pole Laizer ungeiba kama wenzio ungepewa kifungo cha nje labda cha kufagia mazizi.:confused::confused::confused::confused:
AWAMU YA NNE , HAKI ILIKUWA NGUMU KUMEZA, AWAMU YA TANO MAHAKAMA ZIMEWEZESHWA,

KILA ZAMA NA KITABU CHAKE
 
Hivi Mramba and co. walihukumiwa miaka mingapi vile?
Na ni hela ngapi walipoteza?? Kwenye billion 11?
Na huyu masikini wa watu ( sio kwamba natetea wizi, hapana) amekwapua milioni mbili (2.3) eti anafungwa 23 YRS!!! Come on ndugu mahakimu kuweni serious...!!

Na kuna yule aliyekuwa mkurugenzi wa utawala BOT... more than 200Billion was wasted under his watch!! Kafungwa miaka mitatu.. na katoka kabla ya muda for good cunduct na anatafuna hela alizokwibwa!!

Where is fairness in this country?
Wote wameiba, mmoja anafungwa 23 yrs; wengine kwa kuwa walikuwa mawaziri na mwingine mkurugenzi wanafungwa miaka mitatu (3), baada ya mwaka unusu wanaachiwa!

Sheria zirekebishwe!!
 
Ndio tabu viongozi kuingilia muhimili mwingine Wa serikali wameambiwa wakiendesha kesi haraka haraka watapewa ela wanazotaka kesi za mfano siku zote ni kwa masikini siyo huyu tu kuna Yule Wa mirungi nae alikula 30 jela
 
Najiuliza huyu ni Hakim kweli.Au ni machine computer iliyotoa hukumu. Je yeye ni malaika?
 
AWAMU YA NNE , HAKI ILIKUWA NGUMU KUMEZA, AWAMU YA TANO MAHAKAMA ZIMEWEZESHWA,

KILA ZAMA NA KITABU CHAKE

Lakini wale wawili wametoka awamu ya TANO,tusitetee.Tujitahidi kuita Koleo ni koleo na si kijiko kikubwa
 
Huyo kaonewa, billions wanazokula watu wa juu serikalini mbona hawafungwi ata mwaka mmoja? Made in Tanzania
 
Ukitaka kupiga hela bora kuanzia mil 100.. kidogo hakimu anaweza kukuhurumia ukampoza badae, sa hiyo mil 4 hata ukimpa hakimu yote haimtoshi kwanini asikukomeshe
 
Nikweli kaonewa ila kipindi cha mlamba na yona nikipindi cha wapigaji kipiji cha huyu Ngosha nikipindi cha Kazi.so yeye kaanzia kutoa adhabu kipindi hiki cha kwake sijui kama am not wrong there.
 
Escrow B 320 hakuna aliyeguswa,Yona na Mramba 11 B wanafagia hospital pale sinza,huyu only 4m analabwa 23 years.kweli Tz kuna kwenye nchi na wasindikizaji
Hapo ndio hii nchi hua inaniacha hoi.... Kuna U$%#ge mwingi sana hii nchi aisee
 
Hivi Mramba and co. walihukumiwa miaka mingapi vile?
Na ni hela ngapi walipoteza?? Kwenye billion 11?
Na huyu masikini wa watu ( sio kwamba natetea wizi, hapana) amekwapua milioni mbili (2.3) eti anafungwa 23 YRS!!! Come on ndugu mahakimu kuweni serious...!!

Na kuna yule aliyekuwa mkurugenzi wa utawala BOT... more than 200Billion was wasted under his watch!! Kafungwa miaka mitatu.. na katoka kabla ya muda for good cunduct na anatafuna hela alizokwibwa!!

Where is fairness in this country?
Wote wameiba, mmoja anafungwa 23 yrs; wengine kwa kuwa walikuwa mawaziri na mwingine mkurugenzi wanafungwa miaka mitatu (3), baada ya mwaka unusu wanaachiwa!

Sheria zirekebishwe!!
Hii sio poa kabisa, ila nadhan wanafanya hivo baada ya kupewa zile bilion 16,hizi kesi zinazofanyiwa maamuz baada ya hiyo pesa zina shangaza hukumu zake
 
Moja ya matukio ya kipumbavu zaidi kutokea dunian!! "wenye kuiba fedha kidogo,hukumu zao kubwa.Wenye kuiba kiasi kikubwa cha fedha, hukumu zao ndogo"
 
Back
Top Bottom