Kwa miezi kadhaa sasa mhariri wa Nipashe amekuwa akiendesha kampeni maalum na si bila ya maelekezo ya Dkt Reginald Mengi ya kuhakikisha kwamba Profesa sospeter Muhongo ama anafukuzwa kazi au anajiuzulu. Hili la akaunti ya Escrow limekuja tu katika kipindi ambacho tayari kulikuwapo na kampeni maalum ya kumlazimisha kukimbia nafasi yake hiyo.
Hakuna toleo linalotoka bila ya kuwa na habari ya ukurasa wa mbele kumshambulia Profesa Muhongo. Hakuna urazini hata kidogo kwani katika kampeni ya propaganda ambayo lengo lake ni kumng'oa Muhongo kila silaha hutumika.
Kumekuwapo na maelekezo maalumu kutoka kwa Dkt Mengi kwamba gazeti hilo liongoze vita hadi ushindi yaani ushindi wa Nipashe na ITV ni kung'oka kwa Muhongo na asipong'oka vita hiyo ni ya kudumu.
Muhongo kosa lake ni kuwa mkweli tu na kumwambia Mzee Mengi kwamba gharama za kuwekeza katika utafutaji wa mafuta katika bahari ni kikubwa kwa makampuni ya hapa nchini yaani kwa wazawa. Ukweli ambao Bwana Mengi hautaki hata kidogo kuusikia.
Lakini ndiyo ukweli wenyewe kuwekeza katika utafutaji wa mafuta na gesi kwenye bahari bila ya kushirikiana na makampuni ya wenye fedha kubwa si rahisi kwa makampuni ya humu ndani.
Ni vita ambayo Dkt Mengi anataka ashinde kwa njia yoyote ile iwe kwa kusema ukweli au uongo na haijaanza katika hili la mafuta na gesi hata kwenye suala la uchimbaji mkubwa alizua sokomoko kubwa miaka kadhaa iliyopita na Muhongo hakuwapo.
Bwana Mengi anatumia vibaya vyombo vyake vya habari na anasahau kwamba masafa ni ya umma na kibali cha gazeti ni kwa ajili ya kuhudumia jamii na wala si kikundi cha watu iwe kiuchumi au kisiasa.
Mhariri wa Nipashe anakiuka misingi ya uhariri na uandishi wa habari na kwa kushirikiana na Bwana Mengi ataitumbukiza nchi hii kwenye machafuko.