• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Mharibu nchi, ni mwananchi mwenyewe

B

Beem

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Messages
1,613
Points
2,000
B

Beem

JF-Expert Member
Joined May 18, 2018
1,613 2,000
Hakuna shaka juu ya huo msemo, mwananchi mwenyewe ndio mwenye uwezo wa kuijenga na kuiharibu nchi. Hata kukitokea mgeni kutaka kuharibu nchi ni lazima apitie kwa mwananchi mwenyewe

Nimeona bandiko la Mjomba Paskali kuhusu alichokiita Security Alert. Alichoandika Paskali kilitakiwa kuonwa na wenye mamlaka ya nchi ambao kila siku ya Mungu hawalali kuhakikisha Taifa liko salama na naamini kabisa wanajua mengi zaidi. Wanasema kazi yao ni kushauri tu japo inapobidi wanaweza kwenda hatua zaidi.

Adui hawezi kujaribu kuharibu nchi kabla uzalendo haujapotea kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wananchi. Suala la Uzalendo limepungua sana kwa kiasi kikubwa kwa mtazamo wangu, na hilo limesababishwa na wanasiasa, uonevu na ubaguzi kwa minajili ya vyama, kesi za kukomoana, utekaji, utesaji HUKU tukiwa tunaangalia tu jinsi taifa linavyomeguka. Ikifikia asilimia 96 ya wagombea wa vyama vya upinzani wanatolewa kwa figisu kwenye chaguzi za serikali za mitaa ni jambo la hatari. Wananchi kususia kujiandikisha na kushiriki Chaguzi lilitakiwa kutushtua. Lakini tumefumba macho hatujui tunatengeneza bomu

Leo hii kuna wenye hisia kuwa wanaonewa na wanaona hawana pa kukimbilia, kwamba kila unapoenda unakutana na maagizo. Kama mbunge anaweza kupigwa risasi, akafungwa jela kwa kesi za kubambikiwa na kuvuliwa ubunge kwa njama za kisiasa na akakosa pa kwenda kutafuta haki vipi kuhusu mwanachama wa kawaida?

Ndio maana leo hii Marekani akitoa tamko linaloonekana kutetea haki anapata sapoti nyingi ya kundi kubwa la watanzania ambao wengine hufurahia maamuzi yanayochukuliwa hata kama yatakuja kutuathiri wote kama taifa. Marekani siku zote anapita humo humo mlikotengeneza nyufa zenu. Nyufa tunatengeneza wenyewe mgeni anakuja kupita humo humo kwenye nyufa kisha tunaanza kulaumu. Lawama ni kwetu wenyewe.

Haya ya mganyiko katika Taifa watu walikuwa wanaonya lakini wanapuuziwa. Majuto ni mjukuu.

Mfano aliotoa Paskali, watu kama Saddam na Gadhaffi hawa walitawala kwa mkono wa chuma, walikandamiza watu kupitia vyombo vya dola matokeo yake nyufa zikatengenezwa ( ndio ni kweli Marekani kuna maslahi yake hivyo hivyo pia bila nyufa hawezi kuingia).

Tuache masuala ya uonevu kwa misingi ya vyama, mikutano ya kisiasa iruhusiwe, watu watoe wa moyoni, tuache mihimili iwe huru, tugawane keki ya taifa kwa usawa. Ukipitia mitandaoni humo utagundua mapenzi kwa nchi yameanza kupungua, inafikia watu wanatoa dhihaka hadi kwenye kurasa za viongozi wa kitaifa, sio jambo lenye afya. Watu washasahau Cybercrime hawaigopi tena.

Nikumbushie kile kilichoitwa 'maandamano ya Mange na kuiweka nchi katika security level ya hali ya juu ( nchi ilikuwa katika tension). Klichotokea ni kwamba watu walitamani, wakaweka nia ila wakawa waoga tu hawakutokea barabarani. Huo uoga siku ukiwatoka adui anapenya humo humo.

HATUJACHELEWA

Pascal Mayalla
 
Nyabutoro

Nyabutoro

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Messages
856
Points
1,000
Nyabutoro

Nyabutoro

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2017
856 1,000
Wamarekani hutumia udhaifu wa kufikiri wa viongozi wetu kutuumiza.Jiulize kwa sasa watu wapo tayari kupokea lolote kutoka USA ili mradi tu awatetee na mateso ya viongozi wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
B

Beem

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Messages
1,613
Points
2,000
B

Beem

JF-Expert Member
Joined May 18, 2018
1,613 2,000
Wamarekani hutumia udhaifu wa kufikiri wa viongozi wetu kutuumiza.Jiulize kwa sasa watu wapo tayari kupokea lolote kutoka USA ili mradi tu awatetee na mateso ya viongozi wao

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndivyo inavyokuwa, watu wakiteseka nakuona hawana msaada wanakuwa tayari kushirikiama hata na shetani
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
18,093
Points
2,000
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
18,093 2,000
..historia inaonyesha kwamba vyama tawala vimesababisha maafa makubwa duniani.

..GENOCIDE ilipangwa na kutekelezwa na CHAMA TAWALA cha Ujerumani.

..MAUAJI YA KIMBARI ya Rwanda yalipangwa na kutekelezwa na umoja wa vijana wa CHAMA TAWALA cha nchi hiyo.

..Watanzania tuwe macho na CCM. Miaka inavyozidi kwenda ndivyo makada wa chama hicho wanavyoishiwa uwezo wa kufanya siasa na kushawishi umma.
 
B

Beem

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Messages
1,613
Points
2,000
B

Beem

JF-Expert Member
Joined May 18, 2018
1,613 2,000
..historia inaonyesha kwamba vyama tawala vimesababisha maafa makubwa duniani.

..GENOCIDE ilipangwa na kutekelezwa na CHAMA TAWALA cha Ujerumani.

..MAUAJI YA KIMBARI ya Rwanda yalipangwa na kutekelezwa na umoja wa vijana wa CHAMA TAWALA cha nchi hiyo.

..Watanzania tuwe macho na CCM. Miaka inavyozidi kwenda ndivyo makada wa chama hicho wanavyoishiwa uwezo wa kufanya siasa na kushawishi umma.
Binafsi naona wameshaishiwa.
 
N

Nalanala

Member
Joined
Aug 6, 2019
Messages
35
Points
125
N

Nalanala

Member
Joined Aug 6, 2019
35 125
Na hapo ndipo mzungu alipotushinda. Ni mzalendo wa kweli. Atafanya chochote kwa maslahi ya watu wake. Serikali zao huwalinda watu wake kwa gharama yoyote. Polisi ni rafiki wa raia ila kwa Afrika polisi ni adui mkubwa wa raia.

Magu na serikali yake leo hii ndo wanyanyasaji namba moja wa wananchi.

Hating and killing your own flesh and blood halafu tusingizia wamarekani.

How ridiculous can it get

Sent using Jamii Forums mobile app
 
B

Beem

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Messages
1,613
Points
2,000
B

Beem

JF-Expert Member
Joined May 18, 2018
1,613 2,000
Na hapo ndipo mzungu alipotushinda. Ni mzalendo wa kweli. Atafanya chochote kwa maslahi ya watu wake. Serikali zao huwalinda watu wake kwa gharama yoyote. Polisi ni rafiki wa raia ila kwa Afrika polisi ni adui mkubwa wa raia.

Magu na serikali yake leo hii ndo wanyanyasaji namba moja wa wananchi.

Hating and killing your own flesh and blood halafu tusingizia wamarekani.

How ridiculous can it get

Sent using Jamii Forums mobile app
Well said
 

Forum statistics

Threads 1,406,202
Members 532,237
Posts 34,508,418
Top