Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
"Nampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa ya Mipango na Uwekezaji katika Taifa letu. Rais Samia ameamua kutokuogopa na kusimama kwa utulivu katika kusikiliza wataalamu kulisaidia Taifa letu" - Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga
"Taifa lolote duniani ili litambuliwe kuwa limeendelea au linaloendelea kigezo muhimu cha kuangalia ni kiwango cha Elimu cha watu wake. Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeliona hili na inaamini katika kuwekeza kwenye Elimu"
"Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 katika Elimu imeweka wazi malengo yake kuwa ni ili kuzalisha rasilimali watu bora kwa maendeleo ya watu. Serikali imeelezea matamanio yake ya Kuamini kuwekeza katika watu kama kifaa muhimu nchini kuongeza uzalishaji"
"Naomba Serikali iamue kupanga kuweka mkazo Maalum katika maeneo ambayo kiwango cha Elimu hakiridhishi bila kuathiri maeneo ambayo kiwango chake cha Elimu kinaridhisha. Kujenga madarasa maeneo yote ni wazo zuri la kuleta mpango wa kusaidia maeneo ambayo yapo nyuma kielimu ili kuleta thamani halisi ya kurudisha faida ya kuwekeza katika Elimu"
"Kuhusu uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato naomba pasiwe kama eneo la Vingunguti. Viwanja vinatangazwa maeneo ya Msalato Airport lakini ni kwa namna gani Wizara ya Mipango na Uwekezaji imeshirikiana na Sekta ya Anga, Sekta ya Uchukuzi kuhakikisha kuna matumizi mazuri ya Ardhi katika eneo lote la Msalato"