Mhandisi aswekwa ndani kwa kupuuza maagizo

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,984
11,408
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amemsweka rumande Muhandisi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Simoni Ngagani, baada ya kupuuza agizo lake la kufanya maandalizi mapema ya kununua kokoto na Saruji kwa ajili ya kusimika mapipa 50 ya kutunzia uchafu kwenye mitaa mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga ikiwemo eneo kituo cha mabasi yaendayo wilayani.


Tukio hilo limetokea jana asubuhi mjini Shinyanga wakati mkuu huyo wa wilaya akiwa na msafara wake alipowasili katika eneo la stendi ya mabasi yaendayo wilayani kwa lengo la kufanya uzinduzi wa kusimikwa kwa mapipa hayo na kukuta maandalizi hayajakamilika.


Matiro alimuagiza Mhandisi huyo kufanya maandalizi hayo mapema mbele ya mkurugenzi wake wa manispaa ya Shinyanga Kalinjuna Lewis, kuwa ataandaa vifaa hivyo majira ya saa moja asubuhi ili zoezi kukusimika mapipa hayo likamilike haraka, na baada ya hapo wafanye usafi wa mazingira lakini agizo lake mhandisi huyo akapuuza.
 
Sasa kama kulikuwa hakuna fedha angefanyaje, na baadaye ikionekana sio kosa lake atamlipa fidia kwa kumuweka ndani, mzee wa majipu hili agizo lako litaleta matatizo
 
Um
Sasa kama kulikuwa hakuna fedha angefanyaje, na baadaye ikionekana sio kosa lake atamlipa fidia kwa kumuweka ndani, mzee wa majipu hili agizo lako litaleta matatizo[/QUOTE
Nani kukuambia hela hazikuwepo
 
Back
Top Bottom